Pascal Mayalla adai Waziri Mpango alitumia muda mwingi katika kusifu alipowasilisha bajeti. Asema yeye siyo MATAGA na hatafuti uteuzi!

Pascal Mayalla adai Waziri Mpango alitumia muda mwingi katika kusifu alipowasilisha bajeti. Asema yeye siyo MATAGA na hatafuti uteuzi!

Waziri wa Fedha tena akiwasilisha bajeti ya nchi hapaswi kutoa sifa za kuhudhuria misiba, kuwaona wafungwa, kushiriki michezo, kwenda makanisani nk na kuonesha mh Rais ni kiumbe cha kipekee. Akikuwa amebakiza kidogo sana kuinama chini na kumsujudia Rais.

Tujifunze kupongeza vitu na kusonga mbele. Ni ajabu mpk sasa tunazungumzia bwawa la umeme, ndege, SGR, elimu bure, uhakiki wa wafanyakazi. Ilitosha kupongeza mambo hayo wakati yalipoanza. Tujifunze tunapoanza au kukamilisha jambo fulani, lingine hutokea au mahitaji huenda ngazi nyingine ya juu. Ni vema kusifia lakini si vema kutumia nguvu zote kusifia na kushindwa hata kuona mambo mengine.

Rais amefanya mambo mazuri, tumsifie kidogo na tumuoneshe mahitaji mengine hata kama itabidi kumkosoa kwa namna alivofanya aliyoyafanya tayari.

Ukimsifia sana mtu, unakosa uhalali wa kumwambia amekosea. Unaanza kumwogopa!! Huenda hizi sifa ni uoga!!
Ulitakaje? Akapige deki lami kama mnavyofanya nyinyi????
 
Ni katika mjadala wa waandishi kwenye kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari.

Pascal anasema bajeti ya nchi inatakiwa kuwasilishwa kitaaluma lakini juzi waziri wa fedha Dr Mpango ametumia muda mwingi katika kusifu ukilinganisha na kuifafanua bajeti.

Mwandishi Moses Methew alimpinga Pascal kwa madai kuwa Dr Mpango alizitumia vizuri dakika 60 za mwanzo hivyo hakuna ubaya wowote kutumia dakika 135 zilizobaki kusifiana.
Moses amesema hata Pascal Mayalla mwenyewe katika dakika 10 alizopewa kwenye mjadala huu ametumia dakika 7 katika kusifu na mgeni wake kamwachia dakika 3 tu.

Katika kujibu Pascal amedai yeye husifu kimantiki siyo kama wafanyavyo wale Mataga na wala hatafuti Uteuzi kama rafiki zake wa Jf wanavyomzushia.

Mwisho mwandishi Moses Methew amevilaumu vyombo vya habari na bunge kwa kutumia muda mwingi kujadili mambo binafsi na faragha za Mbowe.

Amesema inasikitisha kuona bunge zima linajadili " maisha binafsi " ya Mbowe kana kwamba Mbowe ndio bajeti ya serikali.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Kutumia dakika 60 za mwanzo kuongea vitu muhimu na kutumia dk 135 za mwisho kuongea vitu vya kitoto (kusifia kuliko pitiliza kama mapenzi ya zamani eti nikinywa maji nakuona kwenye glass) ni sawa na kutumia dakika zote 60+135 kuongea upuuzi kwasababu lazima dk 60 zitamezwa na ulichoongea mwishoni kwa dk135

Mtu makini Kama alihisi kusifia ndo bora zaidi na ndio kuna mambo mengi sana, angetumia dk 135 za mwanzo kuimba masifu ya mkuu na akamalizia ns dk 60 za mwisho kueleza vitu muhimu kwenye bajeti yake
 
Nimekuelewa bwashee!
 
Kuna anaeweza fafanua 'mataga' maana yake?

MATAGA NI KIFUPI CHA MANENO
MAKE TANZANIA GREAT AGAIN

Ni slogan ambayo kuna wehu wameiiga kutoka kwa utawala wa Trump, kule the Us wao slogan yao ni MAGA i.e MAKE AMERICA GREAT AGAIN.

Sasa wapambe wa Magufuli ili waweze kupata loophole ya upigaji wa fedha za Magufuli wakasema wabuni ki project cha propaganda kwa jina la MATAGA.

Malengo yake makuu ni
Kusifia chochote kinachofanywa na serikali be it kizuri au kibaya
Kuponda wale wote wenye mawazo mbadala mfano Chadema.
 
Nimegundua bunge la Tz ni la hovyo Afrika mashariki na kati.Bajeti imesomwa badala ya kuchambua na kuishauri serikali nimeona 85% ya wabunge wanasifia mpk kinyaacunaona hyu ni empty set,wanatoa vijembe,wanashindana kijinga kasoro 25% ndio wanaongea kisomi

Tizameni bunge la kenya linavyojadili bajeti unafurahi mwenyewe
Raia wa Kenya kwa ujumla wao wapo smart, huwezi kuwafananisha na raia wa tanganyika walio kama misukule
 
Kutumia dakika 60 za mwanzo kuongea vitu muhimu na kutumia dk 135 za mwisho kuongea vitu vya kitoto (kusifia kuliko pitiliza kama mapenzi ya zamani eti nikinywa maji nakuona kwenye glass) ni sawa na kutumia dakika zote 60+135 kuongea upuuzi kwasababu lazima dk 60 zitamezwa na ulichoongea mwishoni kwa dk135

Mtu makini Kama alihisi kusifia ndo bora zaidi na ndio kuna mambo mengi sana, angetumia dk 135 za mwanzo kuimba masifu ya mkuu na akamalizia ns dk 60 za mwisho kueleza vitu muhimu kwenye bajeti yake
Yes ukiongea utopolo dakika za mwisho hapo manake huo utopolo unaenda kufuta ata zile hoja chache ulizozitoa,ni bora angeanza na utopolo kisha aje kumaliza na hoja kwani hoja ndo zitabaki angalau
 
Hii kumfananisha binadamu na yesu , kumuomba Mungu amshukuru binadamu , kumsifia kuliko hata Muumba.
Ni Bora lingeanzishwa kanisa waanze kumuabudu ili tuelewe moja.
 
Kuna mbunge kujadili maisha binafsi ya Mbowe kama Mbowe. Na kuna maisha binafsi ya Mbowe kama KUB ambae ni kiongozi wa umma. Sasa kama kiongozi wa umma ndio anaruhusiwa kulewa chakari na kula bata na vimada, sijui kama inakubalika.
Huo ushaidi wa kulewa chakari uko wapi?unajua maana ya kulewa chakari wewe?
 
Star Tv ipo nyakati za mwisho hivi bado mnaiangalia tu! Hata watu wenye akili timamu hawawezi kuitikia mwaliko,imebaki inaokoteza hawa wehu.
 
Back
Top Bottom