Pascal anafikiri vitu vilivyopo na vinayotakiwa kufanyika kisheria basi vyahitaji huruma.Najikuta nikiendelea kushiriki kwenye mada mbovu kama hii; hata hivyo ninakushukuru mkuu 'Matrix' kwa kuleta kumbukumbu zinazoonyesha uhafifu wa mijadala yetu siku hizi hapa JF.
Hebu tazama mameno yanayotamkwa kama haya yafuatayo: "Acha Siasa za Harakati - Badilika - Huyu Mama Anakupenda - Ana Huruma"
Haya maneno anaambiwa Lissu, bila shaka na huyo huyo mwenye njaa! Na kwa kweli sasa hivi hata sura yake inaonyesha njaa imekaza zaidi. Haya maneno sina shaka analenga akina Abduli wayasikie au wayasome!
Huyo mama kama wanavyomwita, huo umama ni kwake huko akiwa na mumewe na wanaye, hapo yuko ofisini na analipwa pesa za walipakodi.
Kama mtu hawezi kufanya forecasting ya kujua madhara ya uchaguzi kuwa mbovu ambao madhara yake ni kikundi cha watu kuwaamulia wananchi nani wa kuwaongoza matokeo yake ni kuwaletea mtu wasiyemtaka hii ina madhara makubwa kuliko kuzuia uchaguzi hadi pale utakapopata suluhu ya kuwa na tume iliyo huru kimfumo ila sio hii tume iliyobadilishwa jina na kuongezewa neno huru ila sio huru kimfumo bali ni chupa mpya mvinyo ule ule.
Nikirudi katika kuelezea madhara ya uchaguzi usio huru na wa haki nitatumia mfano mdogo kuwa baada ya Kibaki kuwa mhanga wa uchaguzi wa 1997 , hadi 2002 aliposhinda aliwaahidi wananchi katiba mpya ndani ya siku 90 hata zilipofika alikuwa kipofu wa madaraka hadi pale alipofanya uhuni wa kujitangazia ushindi mezani na kujiapisha haraka haraka sababu yeye ndio amiri jeshi mkuu ndipo alijionea madhara yake na katika vitu ambavyo ungemwambia arudishe nyuma kujisahihisha basi ilikuwa ni kuwapa wananchi wa Kenya katiba mpya kitu ambacho aliamua miaka 3 mbele yaani 2010 kujisahihisha na Kenya kupata katiba mpya na mifumo yote mipya na taasisi huru kama polisi, ofisi mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai, tume huru ya, tume ya uchaguzi, tume ya maadili na uthibiti rushwa , bunge , mahakama n.k
Hivyo mimi nikiwa kama watu wachache tuliobahatika kushuhudia kwa macho yale yalitokea Kenya December 2007 basi nimkumbushe Pascal ni bora kuzuia uchaguzi au kususia uchaguzi kuliko wananchi kuchaguliwa viongozi wasiowapenda sababu ya kuwa tume 100% iko mfukoni mwa rais.