Pre GE2025 Pascal Mayalla amshauri Lissu kutumia jukwaa la JamiiForums kusoma maoni ili kuondokana na siasa za harakati na kufanya siasa za mikakati

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Imekuwaje tena kipindi kile anamtwanga maswali 'Jiwe' alimwagiwa misifa kedekede 🀣🀣🀣.Leo mbona mnambagaza huyu nguli wa habari🀣🀣🀣
 
Ngoja Nami niweke mawazo yangu, kwa upande wangu ajitambulishe kama member wa JAMII FORUM na sio MUWAKILISHI WA JAMII FORUM Kwa sababu mbili zifuatazo .


MEMBER WA JAMII FORUM.

mwanachama unachangia chochote unachojisikia kuwa upo free kuchangia kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kama inavyosema kuwa Una Uhuru wa kutoa maoni yako ila usivunje sheria za nchi.

Kwa hiyo hapo unaweza sema hata uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa huru na Haki na hakuna wa kukuzodoa ni maoni yako umeyatoa kwa kuwa ni upo huru kwa mujibu wa KATIBA.

Lakini pia unaweza sema uchaguzi wa 2020 ulikuwa ulikuwa huru na wa Haki hatuwezi kukupinga Sana ni maoni yako binafsi.

MUWAKILISHI WA JAMII FORUM.

Hapo kwenye muwakilishi wa JAMII FORUM ndiyo napinga pia kwa maoni yangu kwa sababu MUWAKILISHI ni mtu au watu Fulani rasmi waliotumwa au kuagizwa na familia, au taasisi au kikundi chochote kile ambacho walikaa wakasema sasa Nenda sehemu Fulani katuwakilishe.

Swali Je Sisi JAMII FORUM tumemtuma Nani akatuwakilishe? Hata Maxence Melo mwenyewe huwa hasemi muwakilishi wa JAMII FORUM Huwa anasema muanzilishi wa JAMII FORUM na sio MUWAKILISHI.

Muwakilishi huwa anasema Yale tulivyokubaliana au mliyokubaliana akaseme kwa niaba sasa humu JAMII FORUM tupo vyama tofauti kuna TLP, CCM, CHAUMA, CHADEMA N.K sasa mtu mmoja akasemee hivyo vyama vyote? Lakini pia

JAMII FORUM kuna ambao hawana vyama humu pia wanasemewa na mtu ambaye hawajamtuma?

Kwa hiyo hata siku akisimama mbele ya hadhara akisema kwa niaba ya member wote wa JAMII FORUM tunamuunga MKONO LISU au kwa niaba ya member wote wa JAMII FORUM tunamuunga MKONO mama Samia hamuoni kuwa atakuwa anawakosea watu wa CCM au watu wa CHADEMA kwa kuonesha JAMII imesima upande mmoja na JAMII FORUM inapande zote?

Ushauri wangu kila mtu akitaka kujitambulisha ajitambulishe ni MEMBER WA JAMII FORUM NA SIO MUWAKILISHI WA JAMII FORUM vinginevyo uongozi wa JAMII FORUM uje ujibu kuwa huwa wanamtuma muwakilishi wetu hapa jukwaani bila Sisi kujua ila sasa tujue rasmi kuwa tunamuwakilishi Maxence Melo.

Hoja hupingwa kwa Hoja , siku zote Hoja hujadiliwa kwa Hoja na Hoja huwa haipigwi Rungu.

Kwa upande wangu naunga mkono hoja ya mtoa hoja na nawasilisha.
 
Hahaha! Hatari sana. Labda kwa kuwa yeye Mayala ni verified member mkongwe kaona ajipe uwakilishi!
 
Wazazi wake wanahusika vipi? Naomba tuishie kutukanane wenyewe kwa wenyewe bila kuingiza ndugu na jamaa zetu.

Aidha, kumuita Pascal mjinga sio sahihi maana anajua kusoma na kuandika.

Amandla...
Kabisa,wazazi wake walikuwa waadilifu sana,hata yeye pia ingawa sasa amekengeuka kwa sababu zilizo wazi.Hakuna kosa lolote kuvaa uwakilishi wa JF ingawa sikumbuki leo kama alidai yeye ni mwakilishi wa JF
 
Hapana Tindo, mimi Mag3 haniwakilishi, period! Maoni yake ni maoni yake na maoni yangu ni maoni yangu na mara nyingi ni kama maji na mafuta.
Nakuunga mkono kabisa. Hii ni forum huru kabisa kila mtu na mawazo yake pia na ayapendayo yeye. Kuna watu wamo humu hata siku moja jukwaa la siasa hawaligusi wao ni udaku au michezo tuu. Ni hiari.
Sasa hivi hatuoni HATARI ya mtu kujipa "uwakilishi" bila ridhaa yetu?
Hivi siku mtu akilewa zake huko na ni maarufu akaanzisha mada ya KIHAINI huku akisema anatuwakilisha tutabeba hatima ya alilolianzisha? Serikali hii ichunguzayo mambo kama fire brigade si mtasikia JF imefutwa?
Hili jambo lisichukuliwe kwa udogo maana ni kubwa, mawazo ya Pascal Mayalla hayawezi kuwa uwakilishi wa Jamii Forums hata kidogo.
 
πŸ‘€
"ATAKUSANYA NGANO YAKE GHALANI, LAKINI MAKAPI ATAYATEKETEZA KWA MOTO USIOZIMIKA"

"He will gather the wheat into the barn, while the chaff will be burned with unquenchable fire"

Mathew 3:12

πŸ‘†
Kitendo hicho kinaashiria mchakato wa kuchanganua watu wakweli kutoka kwa waongo, wenye manufaa na wahovyo, na wenye mawazo mazuri na mabaya.

Kama ambavyo amekuwa akitukumbusha wana JF, Vijana na Wazee kila mara katika posti zake, Pascal Mayalla huwa anatoa angalizo

Wanabodi,

Naomba kuanza na angalizo!
Simple Mind Discuss People
Ordinary Mind Discuss Events
Great Minds Discuss Ideas。
Highlighting the importance of focusing on what trully matters.

Kwa maoni yangu, huu Uzi ni wa hovyo kuwahi kutokea JF, kwani unamlenga mtu badala ya mambo muhimu ambayo huwa anabandika.

Amidst this, tukizingatia the overwhelming tide of vile, disparaging language, underhanded scheming, and despicable expression of dislike, nina mashaka na JF yetu ya kesho.

Hakika, katika uzi huu, ndipo tunapo tofautisha Ngano na Makapi yake.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ yawezekana pia hii ni mbinu mahususi ya kuwatambua mahasimu wake, wanafki na wapumbavu alike.

Upo uwezekano pia hawa wanataka kumdiscredit ili nyuzi zao ndio ziwe zinapanda kwa propaganda wanazo zieneza. Tambua tunaelekea kwenye Uchaguzi mwingine muhimu kwa Taifa hili. There is a lot of foreign and domestic playets waaiotutakia mema na nchi hii.

Pascal ni mtu muhimu sana likija suala la Taarifa zilizo kuwa Objective.

Sio hivyo tu, Pascal ni kati ya Waandishi wachache ambao unaeza kumkuta kwenye maandiko(articles) katika magazeti ya Tanzania na hata nje za nchi.

Hiyo inaampa credibility kubwa, ni credibility ambayo sidhani hata mleta mada anayo. IjS

Nevertheless, you're right, this qualifies as a Cyber Bullying Rally
 
Huu uzi umeonyesha namna gani mlivyo na chuki binafsi kwa Pasco
 
Yule Abihudi ni mlevi πŸ˜‚πŸ˜‚, yupo ugaibuni ila kama yupo Meru-Arusha.
Ila jamaa ana jua kuwamudu sana , akiona unamzidi ana kutweza utu kabisa πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Reactions: Exy
Taarifa za habari unazo zisikiliza kwenye Luninga nyingi chanzo ni humu jamii forum
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…