Ngoja Nami niweke mawazo yangu, kwa upande wangu ajitambulishe kama member wa JAMII FORUM na sio MUWAKILISHI WA JAMII FORUM Kwa sababu mbili zifuatazo .
MEMBER WA JAMII FORUM.
mwanachama unachangia chochote unachojisikia kuwa upo free kuchangia kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, kama inavyosema kuwa Una Uhuru wa kutoa maoni yako ila usivunje sheria za nchi.
Kwa hiyo hapo unaweza sema hata uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa huru na Haki na hakuna wa kukuzodoa ni maoni yako umeyatoa kwa kuwa ni upo huru kwa mujibu wa KATIBA.
Lakini pia unaweza sema uchaguzi wa 2020 ulikuwa ulikuwa huru na wa Haki hatuwezi kukupinga Sana ni maoni yako binafsi.
MUWAKILISHI WA JAMII FORUM.
Hapo kwenye muwakilishi wa JAMII FORUM ndiyo napinga pia kwa maoni yangu kwa sababu MUWAKILISHI ni mtu au watu Fulani rasmi waliotumwa au kuagizwa na familia, au taasisi au kikundi chochote kile ambacho walikaa wakasema sasa Nenda sehemu Fulani katuwakilishe.
Swali Je Sisi JAMII FORUM tumemtuma Nani akatuwakilishe? Hata
Maxence Melo mwenyewe huwa hasemi muwakilishi wa JAMII FORUM Huwa anasema muanzilishi wa JAMII FORUM na sio MUWAKILISHI.
Muwakilishi huwa anasema Yale tulivyokubaliana au mliyokubaliana akaseme kwa niaba sasa humu JAMII FORUM tupo vyama tofauti kuna TLP, CCM, CHAUMA, CHADEMA N.K sasa mtu mmoja akasemee hivyo vyama vyote? Lakini pia
JAMII FORUM kuna ambao hawana vyama humu pia wanasemewa na mtu ambaye hawajamtuma?
Kwa hiyo hata siku akisimama mbele ya hadhara akisema kwa niaba ya member wote wa JAMII FORUM tunamuunga MKONO LISU au kwa niaba ya member wote wa JAMII FORUM tunamuunga MKONO mama Samia hamuoni kuwa atakuwa anawakosea watu wa CCM au watu wa CHADEMA kwa kuonesha JAMII imesima upande mmoja na JAMII FORUM inapande zote?
Ushauri wangu kila mtu akitaka kujitambulisha ajitambulishe ni MEMBER WA JAMII FORUM NA SIO MUWAKILISHI WA JAMII FORUM vinginevyo uongozi wa JAMII FORUM uje ujibu kuwa huwa wanamtuma muwakilishi wetu hapa jukwaani bila Sisi kujua ila sasa tujue rasmi kuwa tunamuwakilishi
Maxence Melo.
Hoja hupingwa kwa Hoja , siku zote Hoja hujadiliwa kwa Hoja na Hoja huwa haipigwi Rungu.
Kwa upande wangu naunga mkono hoja ya mtoa hoja na nawasilisha.