Pre GE2025 Pascal Mayalla amshauri Lissu kutumia jukwaa la JamiiForums kusoma maoni ili kuondokana na siasa za harakati na kufanya siasa za mikakati

Pre GE2025 Pascal Mayalla amshauri Lissu kutumia jukwaa la JamiiForums kusoma maoni ili kuondokana na siasa za harakati na kufanya siasa za mikakati

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwandishi wa Habari Pascal Mayalla amshauri Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu kutembelea jukwaa la JamiiForums kusoma maoni ili kuondokana na siasa za harakati na kufanya siasa za mikakati.

Kama ulifanyika ulaghai yakajirudia kwenye serikali za mitaa kweli mkuu na heshima zote ulizonazo unaamini ma vegetables watakua tayari kiwepesi bila mashinikizo? Na kwa nini watu wanapokua na madai ya Haki mna term kama vurugu na kuchukulia kama vita? Chama kinachokubalika kinapataje ugumu wakufanya reforms wao siwanauhakika wakukubalika fanyeni reforms wananchi wakawakatae kwenye uchaguzi hauoni vegetables watakua wameshinda kihalali kwa wananchi wameamua? Lakini ushauri kibao mnawaambia CDM mngeutumia hata robo tu kuishauri serikali kikubali mabadiliko ya kweli hamuoneni mngekua mmelisaidia Taifa?
 
Kesho Magazeti
CCM Yamponza Pascal Mayala



Ila Nikikumbuka Merry Mwanjelwa Ali~Log In JF Oops
Halafu Kulikuwa Na Ile Kashfa Ya Mataulo Kule Belgium

Vumbi JF Lilitimka Kama Kwenye Hii Thread
 
Kuna mtu kasema mnyika kampangua my learned brother adv. Mayalla, hamna hoja ya mayalla iliyojibiwa. Jamaa ni wanaharakati wale hamna mwanasiasa pale. Ilikua ninyamaze. Amenikera sana. Yaani lissu ananafasi safi kabisa kuwajibu waulizaji, whatever the question ila jamaa kila siku ni vumbi tu. Wazee mnaipendaje chadema na viongozi wake?

Nb:
Ila nimependa aisee sikuhizi lisu ule weupe unatokaga akiongea hamna. Nadhani alisoma ujumbe wangu.
 
Pascal Mayalla mara nyingi kwenye midahalo ya kisiasa umekuwa ukijitambulisha kwamba wewe ni mwakilishi wa JamiiForums.

JamiiForums ipi unayoiwakilisha, ilihali wewe ni kada wa CCM? Je, JamiiForums, ina mrengo wowote wa kisiasa?

Kama unaenda kwenye midahalo hiyo, jitambuloshe kwa jina la taasisi yako ya PRRRR.

Iwapo ukaendelea kufanya utambulisho wa uakilishi wa JamiiForums, kuna watu watakaofanya mambo ya hovyo na kusema nao pia ni wawakilishi wa JF.

Tunaomba Maxence Melo akemee mara moja Jambo hili kwani linafanya JF ionekane ni Mali ya chama cha siasa
Yule ni chawa wa mama kwani hujui
 
Back
Top Bottom