Uchaguzi 2020 Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Uchaguzi 2020 Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Hongera kwake,mimi naamini kuwa chochote alichokifanya au kuzungumza kwenye kujinadi alishajua kitapokelewa namna gani.

Basi ikitokea ya kwamba kimepokelewa ndivyo sivyo,basi hilo lilikuwa ndilo lengo lake,haingii akilini kwangu kwamba Pascal afanye tu jambo bila kufanya tathmini ya hatima ya jambo hilo.

Hata hivyo kwake yeye kupata au kukosa vinalandana kimizania,na vyovyote itakavyokuwa kwake ni sawa. amethubutu,anastahili kupongezwa zaidi kuliko vinginevyo.
 
Ndugu yangu Mayalla, mimi ni mshabiki wako toka siku nyingi. Huwezi kunijua.
Kwa ufupi wewe ni mpole, mkarimu na kazi yako ya mwanahabari una karama nayo.

Kama mwandishi wa habari mzuri, utakuwa unaijua sana falsafa ya Mwalimu Nyerere kuhusu pesa.

Alisema, Ukitaka kumsaidia maskini somesha MTOTO wake, tena mpe elimu nzuri.
Pesa si msingi wa maendeleo bali ni matokeo yake.

Mwalimu Nyerere wakati wake hakuna mtu angefolenisha maskini na kuwagawia pesa, huyu angemweka ndani.

Alisema Ikulu si pango la walanguzi na akashangaa ni kwa nini watu wanatoa pesa ili waende Ikulu.

Ikulu kuna biashara gani? Vivyo hivyo Ubunge si pango la walanguzi, kwenye ubunge kuna biashara gani hadi mtu atoe pesa au atoe ahadi ya kugawa pesa baada ya kuchaguliwa?
 
Jamaa yangu Pascal Mayalla lazima amwagwe kwa kishindo uchaguzi maoni CCM Kawe baada ya kujiita KITIMOTO eti kwa vile aliendesha kipindi cha KITIMOTO miaka zaidi ya 20 iliyopita wakati wengi walikuwa hawajazaliwa miongoni mwa wapigakura humo ukumbini.

Nani mshauri wa huyu mtaka ubunge aliyempotosha? Mayalla asije ambulia kura 2 akatulilia hapa JF

Uchaguzi 2020 - Wana JF, Nipeni Pole!, Msinicheke, Wala Msinibeze, Nimegombea Ubunge Kawe Kupitia CCM, Nimeambulia Kura 0!. Ama Kweli CCM Ina Wenyewe!
Duh we jamaa una roho mbaya sana,tazama sasa dua lako limemkuta jamaa.

Nimeukumbuka ule uzi wake wa prophets of the dooms.

Tuache kunena mabaya kwa wenzetu. Midomo huumba.

Paschal Mayalla pole mkuu.
 
Jamaa yangu Pascal Mayalla lazima amwagwe kwa kishindo uchaguzi maoni CCM Kawe baada ya kujiita KITIMOTO eti kwa vile aliendesha kipindi cha KITIMOTO miaka zaidi ya 20 iliyopita wakati wengi walikuwa hawajazaliwa miongoni mwa wapigakura humo ukumbini.

Nani mshauri wa huyu mtaka ubunge aliyempotosha? Mayalla asije ambulia kura 2 akatulilia hapa JF

Uchaguzi 2020 - Wana JF, Nipeni Pole!, Msinicheke, Wala Msinibeze, Nimegombea Ubunge Kawe Kupitia CCM, Nimeambulia Kura 0!. Ama Kweli CCM Ina Wenyewe!
Kapewa kura sita.
 
Wajumbe hapo ukitaka wakuelewe vibaya taja miaka hiyo 20 iliyopita unayoongelea kinachowajia wajumbe kichwa ni kuwa huyu mayala ni kibabu kizee kinaongelea mambo ya miaka 20 iliyopita kizee kikongwe hiki watakunyima kura .Hakujiandaa.

Halafu nimefuatilia mitandaoni hicho kipindi kilifutwa sababu Mayala alikuwa akialika watu wanaiponda serikali ya CCM.MZEE MENGI AKAAMUA KUKIFUNGA ASIGOMBANE NA SERIKALI

Lakini mkuu nadhani umefuatilia vibaya. Kipindi cha KITIMOTO hakikuwa kinarushwa na TV ya Mengi Bali DTV hivyo hangeweza kukifunga.
 
Kwa akili yako ya ufipa unadhani mtu aliyepo kwenye kamati ya siasa ya wilaya asifahamu kipidi cha kitimoto?? Tafadhali sana.
We umekula maharage ya wapi? Kwani hapo ni kwenye kamati ya siasa ya wilaya?
Kumbe ushabiki tuu hata mipango ya vikao vya lichama lako hujui?
 
Amepata kura 2,
Alieongoza kura za maoni kawe ni 1.Furaha Jacobo 101,2.Angela Kiziga 85,Askofu Gwajima 79[emoji6]
Askofu Gwajima, Mungu amejibu maombi yako uliyoyakiri mbele ya Kondoo wake. Kugombea Ubunge ni kujishusha. Wewe endelea tu kuwa Mtumishi wa Bwana na walinde vyema kondoo wake.
 
Ila bado najiuliza mbona Pascal Mayalla alikuwa anatuambia hana chama? Kwamba yeye yuko neutral?
Sasa kumbe CCM unaweza kuwa huna chama lakini siku ya kutoa fomu unaenda kununua fomu (kama gazeti) unatoa laki na kadi unapewa hapo hapo?
Kweli Magufuli kamuharibia Nyerere chama chake! Kile ambacho kujiunga ulikuwa unaomba miezi 3 ndio unapata.
 
Askofu Gwajima, Mungu amejibu maombi yako uliyoyakiri mbele ya Kondoo wake. Kugombea Ubunge ni kujishusha. Wewe endelea tu kuwa Mtumishi wa Bwana na walinde vyema kondoo wake.
Bado ana nafasi kwa kuwa ameingia tatu bora, anaweza kuteuliwa na Kamati Kuu kupeperusha bendera Kawe, maneno haya tuyaweke akiba mpaka mwisho wa Mchakato.
 
Jamaa yangu Pascal Mayalla lazima amwagwe kwa kishindo uchaguzi maoni CCM Kawe baada ya kujiita KITIMOTO eti kwa vile aliendesha kipindi cha KITIMOTO miaka zaidi ya 20 iliyopita wakati wengi walikuwa hawajazaliwa miongoni mwa wapigakura humo ukumbini.

Nani mshauri wa huyu mtaka ubunge aliyempotosha? Mayalla asije ambulia kura 2 akatulilia hapa JF

Uchaguzi 2020 - Wana JF, Nipeni Pole!, Msinicheke, Wala Msinibeze, Nimegombea Ubunge Kawe Kupitia CCM, Nimeambulia Kura 0!. Ama Kweli CCM Ina Wenyewe!
Wasioijua CCM...
 
Back
Top Bottom