Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola

For sure sijaona kosa la Paschal. Unless Kama alikuwa anatumiwa.

Ukisoma mabandiko yake mengi Paschal amekuwa mtu mchokonoz tu lkn huwa hatoi hukumu Bali ana speculate hidden agenda
Mfuatilie vizuri kwenye shambulio la Tundu Lissu
 
Mimi nitaendelea tu kumkubali Pascal Mayala.Hivi jamani Pascal anamchongea vipi Erick ? Basi nampa pongezi nyingi Paschal kwa kuweza kuwa na capacity ya kushawish watu wenye taaluma zao. Big up Paschal. Keep it up.
Bado wewe
 
Si sawa kumsingizia Paskali kwa kuitetea Tanzania dhidi ya gazeti la the Economist.

Tanzania ni kubwa kuliko sisi sote. Wimbo wa Taifa moja ya ubeti unatamka ... Mungu ibariki Afrika...Wabariki Viongozi wetu....
Rais ni kuongozi wetu. Ni ujasiri na uzendo kumtetea Rais ambae ni kiongozi wa nchi dhidi ya tuhuma za uongo unaofanywa the the Economist.

Mayala asihukumiwe kwa suala la kisheria lililo mahakamani.

Ikithibitika Eric hajafanya kosa, mahakama itamuachia huru. Ila sio sawa hata kidogo kumsusia Mtanzania mwenzetu Paskali dhidi ya tuhuma nyepesi kuwa ni yeye kamchomea Eric.
 
Akili ndogo tu ndio inaweza kumchukia Paschal, kwangu mimi atabaki kuwa mwana JF bora kabisa kuwahi kumsoma makala zake.

Ni huyu huyu Paschal alieuliza swali pekee kwa Rais kuhusu mipaka yake ya uongozi

Sidhani kama kuna mwandishi anaweza kuuliza swali lenye uzito kama ule kwa muda wote ambao Magufuli atakuwa madarakani
 
Niombe wasomaji wangu muelewe kuwa sina nia mbaya ninapojaribu kuja na uchambuzi wa namna hii. Lengo langu ni kuoneshana kuwa nchi yetu iko hatarini hasa pale taaluma moja ambayo Taifa linawategemea wanaposigana katika jamii nani anayeumia zaidi!

Nakumbuka siku za hivi karibuni gazeti la the Economist lilikuja na habari ambazo Mkuu Pascal aliziita kuwa ni habari za uongo dhidi ya Rais wetu wa Tanzania.

Gazeti ilo liliwahi kuja na habari kuwa "Rais wa Tanzania hapendi kukosolewa"

Gazeti ilo baada ya kuchapishwa Pascal Mayalla alikuja na bandiko la kupinga habari ile huku akionesha jinsi ambavyo sio kweli Rais wetu anapenda kukosolewa.

Alikwenda mbali zaidi akamnukuu Rais wetu kuwa aliwahi kuwaambia wanahabari kuwa yeye anapenda kukosolewe ila akosolewe kwa Staha na kwa hoja.

Pascal Mayalla kwenye andiko lake anatolea mfano kuwa yeye Pascal Mayalla ni moja ya wanahabari ambao waliwahi kumkosoa Rais na Rais alikubali kukosolewa kwa kumjibu huku akimtania.

HOJA.

Kwanza lazma watu mjue kuwa andiko la Pascal kupinga habari ya the Economist ndio iliyoamsha watu na kuanza kufuatilia ni nani na yuko wapi anae ripoti habari hizo katika gazeti la the Economist?

Hapa naomba nieleweke,hata watumishi idara nyeti walianza kufatilia gazeti ilo baada ya kusoma bandiko la Pascal Mayalla hapa JF, na ndipo wakaja kugundua kuwa kumbe mwandishi wa habari zile na nyeti kupitia gazeti lile ni ndugu yetu Erick Kabendera.

Kwanini walifuatilia,kiukweli kilichoandikwa na mwandishi huyo wa habari kilikuwa na ukweli wa 100%ingawa huyu Ndugu Mayalla alikipinga kwa lengo la kujipendekeza kwa msukuma mwemzake.

Je, Pascal Mayalla alijua tangu awali kuwa Kabendera ndie anayeandika habari nyeti na kuziripoti The Economist na alishindwa kumuita kama mdogo wake na kumpa onyo?

Kimsingi kifungo cha Kabendera nadhani ni furaha kwa Mayalla kwani alimjua tangu awali na alishindwa kabisa kumuita na kumuonya ingawa wote wanatoka kanda ya ziwa.

Je, Pascal alijua Erick akifungwa tegemezi wake watalia na kusaga meno na wengine watajitokeza mitandaoni wakimlilia kwa kukosa hata fedha ya kununua Dawa?

Nadhani yote aliyajua ndio maana tangu Kabendera awekwe korokoloni hajawahi jitokeza popote kulaani kukamatwa kwa kijana huyu zaidi inasemekana ndio kwanza anatafuta makala zote zilizoandikwa huko nyuma na kuzisoma na kuzifafanua kwa vijana wa idara nyeti ili kijana azidi kubanwa.

Andiko la Mayalla dhidi ya kumtetea ndugu yake liko hapa JF linaudhi linaumiza kwani humo ndani anawataja wakosoaji wakubwa wa nchi hii ambao leo hii wamegeuziwa rangi ya unga wa ndere wao wanaita unga mweupe sasa huku wakila kuku kwa mirija.

Nasisitiza waandishi wa habari mtengeni Mayalla na waandishi wote wenye vinasaba vya ukabila na wanaoshindwa kusimamia taaluma badala yake wanaishia kujipendekeza kwa kuhofia uhai wao.

Natoa rai kwa Serikali ya Jamhuri kumwachia huru Kabendera. Tusipomdai kwa kiswahili tutawataka kwa kilugha, na hapo ndipo tutakapozuia kiongozi yeyote kuingia mkoa wa Kagera mpaka "omwana weitu mumutaishure.""
Wewe ni lijinga na lilimbukeni. Yaani huo uongo wa erick wewe unauhalalisha, yaani amtukane rais wetu sisi wapiga kura wake tumuache, tena bora yupo huko mahabusu, inakera sana tena sana unapokuwa na lijitu linasema uongo juu ya kiongozi mkubwa ambaye watanzania tunaona kazi yake anavyojitoa kwa moyo then atokee mpuuzi mmoja tu aungane na mabeberu wataka vyetu vya uvunguni. Yaani kila anayepinga maendeleo yetu bora ahame nchi.
 
Kesi ni iliyo sajiliwa mahakama na sio zile zenu za twitter.
Kumbwe ile kwamba alikamatwa na Immigration ilikuwa ya twitter, so spokesperson aliyeitisha press conference naye ni polisi wa twitter pia, so that implies na system yote ya utawala ni ya twitter pia which concludes kuwa hata "kesi iliyosajiliwa na mahakama" ni ya twitter pia kama "zile zetu za twitter".
 
Muda utahibitisha!!

Watu mjifunze kwa Kinana,Mzee Makamba,January na Nape kama mambo ya aina hii yanalipa in case kuna ukweli katika hili lisemalwo hapa.
Wananzengo na wachawi 900 kwa ajili ya akina Mayala na Jiwe
 
For sure sijaona kosa la Paschal. Unless Kama alikuwa anatumiwa.

Ukisoma mabandiko yake mengi Paschal amekuwa mtu mchokonoz tu lkn huwa hatoi hukumu Bali ana speculate hidden agenda
Ili umuelewe vyema itategemea unamtafsiri vipi.

Positively pasco alikuwa msambazaji wa Hilo Jarida alilodai linamtusi Mkulu kwani kupitia Yeye wengi wetu ndio tulikuwa tunapata fursa ya kusoma kile alichokiita "Matusi dhidi ya Pombe".

Lakini pia kupitia Yeye ndio amelifanya Jarida Hilo kujulikana sana humu JF na Makala husika kusomwa na wengi pasipo ku reveal Yeye Yuko upande upi (japo deep down ulikua ukimsoma between lines utagundua kwamba he was mocking someone)

Negativity kupitia Pasco ndio Kama alikuwa anasambaza ama kuchochea hasira za huyo/hao aliodai ametukanwa ikizingatiwa kwamba Yeye Pasco ndiye aliyekuwa kila uchwao akitusogezea "Matusi" hayo tuyasome hapa JF (motive ya kufanya hivyo atakua anaijua Yeye Mwenyewe). Hivyo mtukanwaji anaweza kujihisi kwamba Matusi aliyotukanwa yameonwa na wengi hivyo ghazabu zake kuongezeka.


Tuhuma Kwamba amemchongea Muandishi mwenzie inajiegemeza tu katika nadharia kadhaa mfano Yeye alikua akijua fika Kwamba Kabendera ndiye anaandika Makala zake kwenye Jarida la The economist openly or annonimously (ikizingatiwa kwamba Hawa wanafahamiana vizuri) hivyo kwa kutuletea Ujumbe humu JF kuwa Jarida Hilo linamtusi Mheshimiwa Rais kwa kuandika aliyoyaita "Mauongo na Matusi" kwa Lugha nyepesi Ni kwamba alikuwa akifikisha Ujumbe kwa Erick Kabendera ambaye Ni Muandishi anamtusi Rais wetu.


Vyovyote iwavyo tukubaliane kwamba Pasco ametumia Uhuru wake kupinga kilichoandikwa na Hilo Jarida same as alivyotumia Uhuru wake ndugu Erick kwa Kumkosoa Rais wetu hivyo hastahili lawama zozote.
 
Ha ha ha ha ha, Pascall Mayalla Mungu anakuona eti. Wakati bwana Erick Kafrag akipambana kutoa shombo zake kupitia gazeti la Mabeberu wewe ulikuwa busy kuzipandisha shombo zake kwa mbwembwe na nakishi za kutosha humu jamvini. Ona sasa mwenzako yuko nyavuni. Mungu anakuona bro.
Tulia wewee
 
Unaandika article unaiweka public, mtu anaisoma, anaichambua, unakamatwa.

Badala ya kujilaumu mwenyewe unamlamu aliyeisoma. Ungetaka si ungeiacha kwenye Local Disk yako isiende public!

We should learn how to be accountable for our actions, otherwise it's bullshit.
 
Vipi lakini umeshatoka kwenye kupush box mkuu!?. Bado unaendelea na tabia yako ya kuwakonyeza waliovaa mabuibui!?
Hahaha Aiseee chalii yangu ndio nimerudi Ghetto sasa hivi. Juzi kati nilimkonyeza mmoja mbibi yeye hakuvaa kininja ni buibui tu akatabasamu na kutingishika kichwa
 
Akili ndogo tu ndio inaweza k
umchukia Paschal, kwangu mimi atabaki kuwa mwana JF bora kabisa kuwahi kumsoma makala zake.

Ni huyu huyu Paschal alieuliza swali pekee kwa Rais kuhusu mipaka yake ya uongozi

Sidhani kama kuna mwandishi anaweza kuuliza swali lenye uzito kama ule kwa muda wote ambao Magufuli atakuwa madarakani

Ni hiyo hiyo siku niliona comments nyingi za kumsifia Paschal, hiyo hiyo siku nilijua kwisha yeye msemo wa wakenya, baada ya hapo nilijua in future kama atashindwa kuleta maada ya kuitukana serikali lazima atahusishwa na ukanda, ndicho kilichotokea , na bado tunajidanganya eti sisi ni great thinker's wa kulazimisha maoni yako siku zote ni sahihi, ya wengine sio sahihi, how do we measure ur shahihi maoni? tuna compare na nani? nothing.
 
Back
Top Bottom