tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
MwanaJF maarufu ambaye pia ni mwanahabari na mwanasheria nguli, ndugu Pascal Mayalla ameonekana akilalamika hadharani kwamba kuna siku alimuuliza marehemu Magufuli swali gumu, akaishia kufungiwa leseni yake ya uanahabari pamoja kufurushwa kwenye ofisi aliyokuwa alifanyia kazi.
Mwanahabari huyo, ambaye pia ni kada maarufu wa CCM, amelalamika kwamba baada ya kumuuliza Rais swali alianza kufuatiliwa na chawa wa CCM na hatimaye kupata misukosuko ya hapa na pale iliyovuruga kazi yake ya uanahabari. Sitaki kukupotezea muda mkuu, hebu msikilize wewe mwenyewe hapo chini ujionee jinsi anavyotia huruma:

MAONI YANGU
Pascal Mayalla kuonewa na machawa wa chama chako, amejitakia mwenyewe. Kama unaona huko hakufai si ujiondoe haraka, kwani amefungwa kamba? Kila siku huwa tunakushauri uache msimamo wa kutetea chama ambacho hakina shukrani lakini husikii. Shauri yako!