Pascal Mayalla: Nilimuuliza Rais swali gumu wakanifungia kufanya kazi ya uanahabari

Pascal Mayalla: Nilimuuliza Rais swali gumu wakanifungia kufanya kazi ya uanahabari

MwanaJF maarufu ambaye pia ni mwanahabari na mwanasheria nguli, ndugu Pascal Mayalla ameonekana akilalamika hadharani kwamba kuna siku alimuuliza marehemu Magufuli swali gumu, akaishia kufungiwa leseni yake ya uanahabari pamoja kufurushwa kwenye ofisi aliyokuwa alifanyia kazi.

Mwanahabari huyo, ambaye pia ni kada maarufu wa CCM, amelalamika kwamba baada ya kumuuliza Rais swali alianza kufuatiliwa na chawa wa CCM na hatimaye kupata misukosuko ya hapa na pale iliyovuruga kazi yake ya uanahabari. Sitaki kukupotezea muda mkuu, hebu msikilize wewe mwenyewe hapo chini ujionee jinsi anavyotia huruma:

​

MAONI YANGU
Pascal Mayalla kuonewa na machawa wa chama chako, amejitakia mwenyewe. Kama unaona huko hakufai si ujiondoe haraka, kwani amefungwa kamba? Kila siku huwa tunakushauri uache msimamo wa kutetea chama ambacho hakina shukrani lakini husikii. Shauri yako!
​
Mkuu nadhani nilisha kupa jibu la swali hili siku mbili zilizopita. Halikuwa swali gumu isipokuwa nadhani Magufuli alichukulua kama ni Kebehi fulani kwake, yaani umemuona hajui anachokifanya na ndio maana akajibu naye kihuni.

Haikupendeza wala haikuwa staha kwa.majibu ya rais, isipokuwa binafsi nilitegemea wewe unajua kwamba Rais anayo madaraka ya kufuta matumizi yoyote ya Mhimili wake (Serikali - Executive)ambayo anaona hayana tija kwa Wananchi. Huitwa Executive order ama Presidential decree.

Marais wengi hufanya hivyo pindi wanapoingia madarakani kupunguza matumizi makubwa ya Serikali na fedha zake huelekezwa sehemu nyingine yenye mahitaji.

Maasalaam
 
Kuzuia vyama vya upinzani kufanya siasa na kunyima uhuru wa habari na kujieleza kunapunguzaji matumizi ya serikali mkuu?
Hili swala jingine nadhani Mayalla aliulizwa swali moja lenye sehemu 3, moja ni Kuzuia viongozi safari za nje mpaka kwa kibali chake. Ndio hapo nilipojibu - Kupunguza Matumizi ya Serikali.

Kuhusu Mikutano na maandamano Kama nilivyosema mwanzo nadhani Magufuli alidhani Mayalla anafanya dhihaka na sio hoja ya kutaja kujua kwa nini kafanya vile haswa alipouliza ninkifungu gani cha Katiba kimempa mamlaka hayo.

Ni hivi, Rais wa Jamhuri ya Tanzania ndiye Mkuu wa mihimili yote mitatu kwa mujibu wa Katiba kama ulikuwa hujui.

Rais ana kiti Bungeni na huwakilishwa na Mawaziri kutoka mhimili wake. Ndiye huchagua viongozi wa juu ngazi zote kwa hiyo unapouliza kapata wapi Mamlaka hayo ina maama hujui muundo wa Serikali ya Jamhuri.

Kwa nguvu alopewa rais wa Janhuri anaweza kuingilia popote, halafu kumbukeni Magufuli alizuia mikutano ya Vyama vya Kisiasa baada ya maandamano ya Chadema ambayo ilitokea msichana mmoja kuuawa kwa risasi.

Kisha nadhani alitambua nchi nyingi duniani baada ya Uchaguzi huwa hakuna tena mikutano ya hadhara wala Maandamano ya vyama vya Siasa. Vyama hutumia njia nyingine za habari kueneza siasa zake iwe magazeti, redio, luninga. Sehemu pekee wanakuwa huru Kisiasa ni Bungeni ambako wawakilishi wa vyama vya Siasa hushiriki kikamilifu.

Binafsi niseme wazi nilimkubali sana Magufuli kwa uwezo wake wa kufikiri na kuongoza. Kuumbuka alipozuia Maandamano na mikutano ya Vyama vya Kisiasa, Polepole na Bashiru walikuwa mbele sana kwenye vyombo vya habari wakati Upunzani wanaendelea kulalamika.

Mwisho, Magufuli alizuia Maandamano na kwa miaka 6 alokuwa madarakani hakuuawa mtu, lakini Samia amefungulia wameuawa zaidi ya wa 500 kama sio 1,000.
Najiuliza Magufuli alijuaje kama Mikutano ya Kisiasa na Maandamano ni chanzo cha mauaji ya Wananchi wasiokuwa na hatia?

Mimi sijui..
 
Hili swala jingine nadhani Mayalla aliulizwa swali moja lenye sehemu 3, moja ni Kuzuia viongozi safari za nje mpaka kwa kibali chake. Ndio hapo nilipojibu - Kupunguza Matumizi ya Serikali.

Kuhusu Mikutano na maandamano Kama nilivyosema mwanzo nadhani Magufuli alidhani Mayalla anafanya dhihaka na sio hoja ya kutaja kujua kwa nini kafanya vile haswa alipouliza ninkifungu gani cha Katiba kimempa mamlaka hayo.

Ni hivi, Rais wa Jamhuri ya Tanzania ndiye Mkuu wa mihimili yote mitatu kwa mujibu wa Katiba kama ulikuwa hujui.

Rais ana kiti Bungeni na huwakilishwa na Mawaziri kutoka mhimili wake. Ndiye huchagua viongozi wa juu ngazi zote kwa hiyo unapouliza kapata wapi Mamlaka hayo ina maama hujui muundo wa Serikali ya Jamhuri.

Kwa nguvu alopewa rais wa Janhuri anaweza kuingilia popote, halafu kumbukeni Magufuli alizuia mikutano ya Vyama vya Kisiasa baada ya maandamano ya Chadema ambayo ilitokea msichana mmoja kuuawa kwa risasi.

Kisha nadhani alitambua nchi nyingi duniani baada ya Uchaguzi huwa hakuna tena mikutano ya hadhara wala Maandamano ya vyama vya Siasa. Vyama hutumia njia nyingine za habari kueneza siasa zake iwe magazeti, redio, luninga. Sehemu pekee wanakuwa huru Kisiasa ni Bungeni ambako wawakilishi wa vyama vya Siasa hushiriki kikamilifum

Binafsi niseme wqazi nilimkubali sana Magufuli kwa uwezo wake wa kuongoza. Kuumbuka alipozuia Maandamano na mikutano ya Vyama vya Kisiasa, Polepole na Bashiru walikuwa mbele sana kwenye vyombo vya habari wakati Upunzani wanaendelea kulalamika.

Mwisho, Magufuli alizuia Maandamano na kwa miaka 6 alikuwa madarakani hakuuawa mtu, lakini Samia amefungulia wameuawa zaidi ya wa 500 kama sio 1,000.
Najiuliza Magufuli alijuaje kama Mikutano ya Kisiasa na Maandamano chanzo cha mauaji ya Wananchi wasiokuwa na hatia?

Mimi sijui..
Kumbe wewe unashabikia mauaji ya raia wasiokuwa na hatia eeh? Sawa mkuu, Mungu anakuona.
 
MwanaJF maarufu ambaye pia ni mwanahabari na mwanasheria nguli, ndugu Pascal Mayalla ameonekana akilalamika hadharani kwamba kuna siku alimuuliza marehemu Magufuli swali gumu, akaishia kufungiwa leseni yake ya uanahabari pamoja kufurushwa kwenye ofisi aliyokuwa alifanyia kazi.

Mwanahabari huyo, ambaye pia ni kada maarufu wa CCM, amelalamika kwamba baada ya kumuuliza Rais swali alianza kufuatiliwa na chawa wa CCM na hatimaye kupata misukosuko ya hapa na pale iliyovuruga kazi yake ya uanahabari. Sitaki kukupotezea muda mkuu, hebu msikilize wewe mwenyewe hapo chini ujionee jinsi anavyotia huruma:

​

MAONI YANGU
Pascal Mayalla kuonewa na machawa wa chama chako, amejitakia mwenyewe. Kama unaona huko hakufai si ujiondoe haraka, kwani amefungwa kamba? Kila siku huwa tunakushauri uache msimamo wa kutetea chama ambacho hakina shukrani lakini husikii. Shauri yako!
​
shida sio mkuu wa nchi hata kidogo, shida ni wale wasaidizi wakati mwingine huchukua sheria mkononi wakidhani watamfurahisha boss mkubwa na matokeo yake kuchafua taswira yote katika taasisi hasa kiti cha Mh rais
 
Back
Top Bottom