Pascal Mayalla: Tanzania sasa inajenga Mifumo na sio kujenga watu kama enzi za Hayati Magufuli

Pascal Mayalla: Tanzania sasa inajenga Mifumo na sio kujenga watu kama enzi za Hayati Magufuli

una uwezo wa kujijua lakini si kujiona waliokuzunguka ndo wanakuona kuwa usoni una tongotongo
Kuna tofauti kati ya kujiinua, kujikweza, kujimwambafy na kujitambua, mimi najitambua na sio kujiinua, kuhikweza au kujimwambafy.
P
 
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alifanya mabadiliko ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kumuondoa aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi Dokta Bashiru Ali na kumteua kuwa mbunge.

Je, wachambuzi wanazungumzia vipi hatua hii?

Msikilize mchambuzi wa siasa za Tanzania, Pascal Mayalla akichambua kwa kina kuhusiana na kile kinachoonekana kama anguko la msomi huyo.
View attachment 1817783
unasemea yule paschal mayalla aliyepiga mapambio yote kwa mwendazake?
 
Nakubaliana na mchambuzi 100% kwa Bashiru, but what has Mulamula done?

Just another hopeless human being winnning public support based on her qualifications but useless professional..
Mkuu, ikikupendeza tujumlishie mapungufu ya balozi Mulamula.
 
What do you know about penetrating the us market in any industry?

Ukitaka kuuza bidhaa yoyote ya Tanzania, US unamjua wholesaler yoyote atakaenunua, how to approach them and his quality demands? Based on Tanzania government information...
Huyu mama alikutibua wapi/ lini?
 
Unakuta mbunge anajisifia kusema watu wangu. Huku hao watu wakiteseka, fukara. Shule majengo shida, huduma za afya tabu. Mtu mmoja analipwa mamilioni.
Hakuna haki.

Wabunge wenyewe majimboni hawaonekani. Wakienda Bungeni maswali ni yale yale toka nazaliwa hakuna linalo badilika. Utasikia korosho, Pamba, ufugaji, madini, elimu. Hivi haya yote hayajapata ufumbuzi toka wakati wa Nyerere hadi Leo! Miaka 60 tunaongelea jambo lile lile!

Ulaya ya miaka ya hamsini na tisini ilikuwa masikini si kama ya Leo. China, Malyasia, India, Korea na nyinginezo walikuwa masikini.

Je sisi watanzania tumelaniwa nini? Nyerere alitupatia viwanda leo vyote hakuna.

Shida ni nini? Nilibahatika kufanya kazi serikalini, nilipo ingia nilishangaa mengi. Hapo nikajua Tanzania kwendelea ni kazi. Tutapiga mark time.

Tunahitaji kubadili mfumo wa kiutumishi. Tunahitaji kubadili matumizi ya fedha na mshahara. Tunahitaji kubadili mfumo wa utekelezaji wa miradi.

Pia kubadili mfumo wa Bunge. Na kuwa na wabunge wachache. Kufuta viti maalum. Na wabunge wawajibishwe mara wanapokuwa si wawajibikaji.

Hivyo tunahitaji muundo mpya wa serikali. Hata baraza la mawaziri hatuhitaji utitiri wa mawaziri.

Kuna mtaalamu wa ujenzi ni Afisa mkubwa walijenga barabara isiyo na kiwango ktk kumhoji akanambia akijenga ya kiwango yeye na familia yake watakula nini?
Anajua hyo isiyo na kiwango baada ya muda itahitaji matengenezo hivyo atapata fedha. Nilichoka!

Afisa mmoja mkubwa anateuliwa na Rais akanambia usipo kula fedha ya serikali wengine wanakula. Usiangalie kuendeleza nchi. Jiendeleze mwenyewe.

Baada ya muda niliona niache kazi ya serikali na kufanya kazi katika mashirika ya kimataifa.

Tuombeni na kudai Katiba mpya. La sivyo hata vyama shindani vikiingia bado ni yale yale.
 
Nakubaliana na mchambuzi 100% kwa Bashiru, but what has Mulamula done?

Just another hopeless human being winnning public support based on her qualifications but useless professional.

What has Mulamula done, kuna namna tumejifunza ya kupambana na US politics or influence in Tanzania kwa ushauri wake.

How best to attract US investors in Tanzania based on her advice?

How to influence our policies in US government for the benefit of Tanzania?

Mulamula is just another useless diplomat.
Umemu- attack personally kama Mulamula kwa sababu zako binafsi za zamani kati yako na wewe.

Back kiofisi tangu awe Waziri in less than 80 days aliyoyafanya kwenye duru za kimataifa ni kubwa sana. Mwendazake alikuwa amei dogosha Tanzania kimataifa ikawa kama Somalia kwa namna yeye na Kabudi walivyokuwa wana handle ovyo diplomasia. Angalia mawasiliano na EU, UNHCR, COVID 19 na issues za Watanzania kuzuiwa kwenda US.

Huyu Mulamula kwa siku chache tumeanza kuona mwanga wa mafanikio katika eneo hili.
 
Hakuna assumptions mkuu kikutokacho mdomoni ndio wewe sasa hii nchi ikiwa na watu vigeu geu kama wewe tutafika kweli alafu huoni aibu kusema unavyosema ? hivi hizi shule mnadomaga zinawasaidia nini kama mtu huwez simama na jambo lako moja ulilosema.
Samahani mkuu... hivi wewe ni mrangi?

Angalizo:
(Nauliza mrangi kabila na wala siyo 'mrangi' member maarufu wa JamiiForums)
 
Hii ni yesterdays news!

P
Ni vizuri mkuu ukaandika summary ya hayo mazungumzo tukasoma hapa wote
 
Ni vizuri mkuu ukaandika summary ya hayo mazungumzo tukasoma hapa wote
Kwa vile mimi ni mwandishi wa habari wa print, habari ninazoandika ndizo naleta humu in print format.
Kwa vile mimi ni mwandishi wa habari mtangazaji wa redio, habari ninazoandika kwa ajili ya redio, siandiki summary, bali huleta audio clip, anayetaka kusikia nimesema nini ni lazima asikilize hiyo audio clip- Ubunge wa Bashiru Ali, wachambuzi wanasemaje? | DW | 01.04.2021
Kwa vile mimi ni mwandishi wa habari mtangazaji wa TV, habari ninazoandika kwa ajili ya TV, naleta humu in video format, anayetaka kusikia nimesema nini kwenye TV, ni lazima aangalie Video Clip.
P.
 
Maisha yanaenda kasi saaana
wale waliokuwa wanamsifia Mwendazakee enzi ilee yuko kwenye peak
ndo hawa hawa wanaotoa maoni ya kumkosoa Mwendazakee baada ya kwenda zakee
kweliii usimwamini mwanadamu ambae fikra zake daima zinabadilikaa
 
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alifanya mabadiliko ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kumuondoa aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi Dokta Bashiru Ali na kumteua kuwa mbunge.

Je, wachambuzi wanazungumzia vipi hatua hii?

Msikilize mchambuzi wa siasa za Tanzania, Pascal Mayalla akichambua kwa kina kuhusiana na kile kinachoonekana kama anguko la msomi huyo.
View attachment 1817783
Mkuu

Mwambie huyo jamaa mwanzoni niliamini sana mabandiko yake lakini kimsingi hana uhalisia anajipendekza akitumaini kuteuliwa ndio maana kwa ajabu kabisa kipindi cha JPM alikuwa anauma na kupuliza akijua mziki wake hadi akathubutu kutaka kugombea ubunge Kawe na wajumbe wakamwangamiza bila huruma.

Muulize hupo mfumo ambao anadai ndio unaojengwa unatokana na sheria ipi ilitungwa hivi karibuni yenye kuupa nguvu mchakato wa utengenezaji wa mfumo?

Mwanasiasa yeyote anayejaribu kuharibu taswira ya JPM na kumpaka urembo Mh SSH ni ubatili mtupu na mwisho wake majuto mjukuu.
 
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania alifanya mabadiliko ya kiutendaji ikiwa ni pamoja na kumuondoa aliyekuwa Katibu Mkuu kiongozi Dokta Bashiru Ali na kumteua kuwa mbunge.

Je, wachambuzi wanazungumzia vipi hatua hii?

Msikilize mchambuzi wa siasa za Tanzania, Pascal Mayalla akichambua kwa kina kuhusiana na kile kinachoonekana kama anguko la msomi huyo.
View attachment 1817783
Mnafiki tu huyu na msaka-uteuzi. Enzi za mwendazake alikuwa akisifu na kuabudu kuwa hajawahi kutokea kiongozi mwenye maono kama huyo. Leo anaponda utawala wake na kumsifia Mama aliyeko madarakani!

Hana msimamo, opportunist tu huyu!!
 
Kwa vile mimi ni mwandishi wa habari wa print, habari ninazoandika ndizo naleta humu in print format.
Kwa vile mimi ni mwandishi wa habari mtangazaji wa redio, habari ninazoandika kwa ajili ya redio, siandiki summary, bali huleta audio clip, anayetaka kusikia nimesema nini ni lazima asikilize hiyo audio clip- Ubunge wa Bashiru Ali, wachambuzi wanasemaje? | DW | 01.04.2021
Kwa vile mimi ni mwandishi wa habari mtangazaji wa TV, habari ninazoandika kwa ajili ya TV, naleta humu in video format, anayetaka kusikia nimesema nini kwenye TV, ni lazima aangalie Video Clip.
P.
Sawa
 
Back
Top Bottom