It's true, sio tuu wanashobokewa, bali pia wanaongoza kwa maokoto!.
Kuna event fulani ilifanyika Jamhuri Jamhuri Stadium, Dodoma, mgeni rasmi ni JK, mburudishaji ni Diamond Platnum na Media Partner ni kampuni ya PPR.
1. MC alipotangaza, mgeni rasmi anawasili, watu walibaki wamekaa tuu, hadi MC kuwaomba wasimame wampokee JK, ndipo watu wakasimama na kumshangilia JK.
2. Diamond Platinum akachelewa hivyo kabla hata hajaingia uwanjani, alizuiwa kuingia uwanjani na msafara wake, akaambiwa rais akiisha ingia mahali, hakuna tena gari nyingine inaruhusiwa kuingia, hivyo akaambiwa ashuke na kuingia kwa miguu. Diamond aliposhuka tuu, ilikuwa balalaa!, watu walipagawa na kupiga kelele kumshangilia utadhani vichaa!. Sasa ile tembea yake na mabodi guards 6!, ni ma bouncer wa 6 pack, wamevaa suti nyeusi za kuwabana ili vifua vionekane!, huku wamevaa miwani nyeusi za security zenye earphones, wawili mbele, wawili katikati na wawili nyuma!, hata rais halindwi hivyo!, alipoingia uwanjani, uwanja ulichachawa, watu walilipuka kuchachawa na kupagawa utadhani wamepandwa mapepo!. Diamond alipata attention kubwa kuliko Rais!.
3. Tukija kwenye maokoto, baada ya event jamaa wakalipa cash, wakati nasaini fungu langu la media, nikaona fungu atakalosaini Diamond Platinum!, ni mbingu na nchi!. Mimi ambaye nimelitangaza tukio mwenzi mzima kabla, na siku ya mwisho kuwatangazia live, kuwaandalia kipindi, ku manage media, nikilinganisha the hassles nilizopitia na bado natakiwa kufanya media monitoring, kufanya media deliveries na mwisho kuwaandikia media report yenye kila kilichoripotiwa, newspapers clips, tv clips, online links!, nikilinganisha na alicholipwa Diamond Platinum kwa kupanda tuu jukwaani ku perform hardly 5 minutes!, kiukweli nilichoka!.
Yaani mtoto wa Tandale, Standard Seven drop out, alilipwa 20 times a University graduate, aliyefanya media Consultancy!.
P