Pasco Mayalla ana vielement vya unabii afungue kanisa

Pasco Mayalla ana vielement vya unabii afungue kanisa

Nilianza kumuona miaka ile na kipindi chake cha Kitimoto.

Nikaja kukutane nae UDSM akisoma LLB na mimi nikisoma kozi ngumu kuliko zote pale chuoni, namkumbuka akinesanesa na pikipiki lake viunga ya UDSM au Mabibo Hostel nilipokuwa naishi.

Mwaka 2005 Au 2006 NIlikuwa napata lunch Hill Park, tukajikuta tuko meza moja, ila kwa vile alikuwa star sikumshobokea, Kama ilivyo desturi yangu ya kuwakaushia mastaa so hanijui, simjui.

Kwa bahati mbaya wote tulidisco chuo,Mimi nilidisco sababu ya ugumu wa masomo ila mwenzangu nasikia ilikuwa ni figisu figisu tu za prof mmoja sio sababu ya uwezo mdogo.
Baada ya kudisco nikakimbia nchi tena kwa mara ya pili. Sikuwahi kumuona tena zaidi ya kumsoma JF na mimi siangalii TV sijui yuko TV gani siku hizi.

Kupitia JF Nimekuwa nikifuatilia maandishi yake, nara kadhaa, niseme tu maandishi yake yana unabii ndani yake, orodha ni ndefu sana nikiweka hapa hapatoshi, vitu vingine huchukua miaka hata mitano kutokea, hakuna mwana JF anayemfikia kwa hilo.

Kama hana pepo wa utambuzi basi ana roho mtakatifu. Nafahamu yeye ni mkatoliki Mzuri ila afungue tu kanisa atapata wafuasi. Nafahamu pia anapenda siasa, madhabahuni pia ni sehemu sahihi ya kupiga siasa kama akina Mama Rwakatale, Kakobe, Gwajima, Pengo, Mtikila, Sheikh Ponda, Alhad Musa wote hao wanapiga siasa kwenye mimbari.

Atumie hilo pepo la utambuzi au roho mtakatifu aliyenae kuwafikia wengi.

Maana kila utawala unamsukumia kambo utadhani hana kitu kichwani na kwa umri wake sitegemei kuona akipata teuzi,

Ni ushauri tu.
Basi kwa kuwa na wewe unauwezo wa utabiri fungua kilinge🏃🏃
 
Mayalla namkubali sana. Mimi mtu aliyesoma Ilboru huwa nampa heshima. Sema huyu dingi atakuja na reference ya kuelezea kuwa alishasema kuhusu huu uzi wa mdukuzi. Mwaka jana aliongoza kwenye wanaJF walioleta nyuzi bora.
 
Ukisoma uzi uliotabiri nani rais 2015 hakika utakubaliana na mwandishi. Jf kuna manabii. Mh. Magufuli aliwekwa namba 10 akiwa wa mwisho. Mwandishi akataja jinsi serikali namaisha yatakavyokuwa. Sote tuliamini kuna kitu nje ya ujuvi wa wengi.
Mkuu robert sendabishaka, if ni mtaa, Shule na darasa, wana JF wapabdisha nyuzi ni waalimu na wasoma nyuzi ni wanafunzi, unapozungumzia bandiko lolote la zamani, ili kuwasaidia wanafunzi wapya, unaweka na references.
*Uzi haukuwa wa paschal.
Mimi uziwangu huu Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli wa mwaka 2014, haukuwa utabiri, nilishikwa sikio na wale 'jamaa zetu' na nilioutoa kwa angalizo fulani, it's very unfortunately hawa jamaa zetu wa siku hizi ni hakuna kitu!.
P
 
Unadhani mechanical au civil engineering ni sawa na fine and performing arts?
Japo ni kweli kozi za sayasi za medicine na engineering zote, mechanical, chemical, nuclear, etc. ni kozi ngumu kuliko kozi za sheria, or arts zote be it social science or fine and performing arts, lakini tukija kwenye maokoto, ukiondoa nchi ya Marekani, sehemu nyingine kote duniani wanaoongoza kwa maokoto ni waliosoma hizo kozi nyingine!.

Duniani kuna type 4 za kuishi top life kwa upande wa maokoto
1. Top Brains,
2. Top Talents
3. Top Inheritors
4. Top Fixers
P
 
Dunia yote wasanii wakubwa wanashobokewa zaidi sema tu hawana power
It's true, sio tuu wanashobokewa, bali pia wanaongoza kwa maokoto!.
Kuna event fulani ilifanyika Jamhuri Jamhuri Stadium, Dodoma, mgeni rasmi ni JK, mburudishaji ni Diamond Platnum na Media Partner ni kampuni ya PPR.
1. MC alipotangaza, mgeni rasmi anawasili, watu walibaki wamekaa tuu, hadi MC kuwaomba wasimame wampokee JK, ndipo watu wakasimama na kumshangilia JK.
2. Diamond Platinum akachelewa hivyo kabla hata hajaingia uwanjani, alizuiwa kuingia uwanjani na msafara wake, akaambiwa rais akiisha ingia mahali, hakuna tena gari nyingine inaruhusiwa kuingia, hivyo akaambiwa ashuke na kuingia kwa miguu. Diamond aliposhuka tuu, ilikuwa balalaa!, watu walipagawa na kupiga kelele kumshangilia utadhani vichaa!. Sasa ile tembea yake na mabodi guards 6!, ni ma bouncer wa 6 pack, wamevaa suti nyeusi za kuwabana ili vifua vionekane!, huku wamevaa miwani nyeusi za security zenye earphones, wawili mbele, wawili katikati na wawili nyuma!, hata rais halindwi hivyo!, alipoingia uwanjani, uwanja ulichachawa, watu walilipuka kuchachawa na kupagawa utadhani wamepandwa mapepo!. Diamond alipata attention kubwa kuliko Rais!.
3. Tukija kwenye maokoto, baada ya event jamaa wakalipa cash, wakati nasaini fungu langu la media, nikaona fungu atakalosaini Diamond Platinum!, ni mbingu na nchi!. Mimi ambaye nimelitangaza tukio mwenzi mzima kabla, na siku ya mwisho kuwatangazia live, kuwaandalia kipindi, ku manage media, nikilinganisha the hassles nilizopitia na bado natakiwa kufanya media monitoring, kufanya media deliveries na mwisho kuwaandikia media report yenye kila kilichoripotiwa, newspapers clips, tv clips, online links!, nikilinganisha na alicholipwa Diamond Platinum kwa kupanda tuu jukwaani ku perform hardly 5 minutes!, kiukweli nilichoka!.

Yaani mtoto wa Tandale, Standard Seven drop out, alilipwa 20 times a University graduate, aliyefanya media Consultancy!.
P
 
It's true, sio tuu wanashobokewa, bali pia wanaongoza kwa maokoto!.
Kuna event fulani ilifanyika Jamhuri Jamhuri Stadium, Dodoma, mgeni rasmi ni JK, mburudishaji ni Diamond Platnum na Media Partner ni kampuni ya PPR.
1. MC alipotangaza, mgeni rasmi anawasili, watu walibaki wamekaa tuu, hadi MC kuwaomba wasimame wampokee JK, ndipo watu wakasimama na kumshangilia JK.
2. Diamond Platinum akachelewa hivyo kabla hata hajaingia uwanjani, alizuiwa kuingia uwanjani na msafara wake, akaambiwa rais akiisha ingia mahali, hakuna tena gari nyingine inaruhusiwa kuingia, hivyo akaambiwa ashuke na kuingia kwa miguu. Diamond aliposhuka tuu, ilikuwa balalaa!, watu walipagawa na kupiga kelele kumshangilia utadhani vichaa!. Sasa ile tembea yake na mabodi guards 6!, ni ma bouncer wa 6 pack, wamevaa suti nyeusi za kuwabana ili vifua vionekane!, huku wamevaa miwani nyeusi za security zenye earphones, wawili mbele, wawili katikati na wawili nyuma!, hata rais halindwi hivyo!, alipoingia uwanjani, uwanja ulichachawa, watu walilipuka kuchachawa na kupagawa utadhani wamepandwa mapepo!. Diamond alipata attention kubwa kuliko Rais!.
3. Tukija kwenye maokoto, baada ya event jamaa wakalipa cash, wakati nasaini fungu langu la media, nikaona fungu atakalosaini Diamond Platinum!, ni mbingu na nchi!. Mimi ambaye nimelitangaza tukio mwenzi mzima kabla, na siku ya mwisho kuwatangazia live, kuwaandalia kipindi, ku manage media, nikilinganisha the hassles nilizopitia na bado natakiwa kufanya media monitoring, kufanya media deliveries na mwisho kuwaandikia media report yenye kila kilichoripotiwa, newspapers clips, tv clips, online links!, nikilinganisha na alicholipwa Diamond Platinum kwa kupanda tuu jukwaani ku perform hardly 5 minutes!, kiukweli nilichoka!.

Yaani mtoto wa Tandale, Standard Seven drop out, alilipwa 20 times a University graduate, aliyefanya media Consultancy!.
P
Ahaa Michele Obama aluwahi kusema kuwa anatamani angekuwa Beyonce
 
Kama udsm kuna kozi ngumu na kozi laini, ndio maana wanazalisha maprofesa wenye uwezo mdogo wakufikiri....
Kusoma ni jambo moja na uwezo wa kufikiri ni jambo jingine!. Uwezo wa kusoma ni aquired knowledge unapatikana kwa kufundishwa, wakati uwezo wa kufikiri ni inborn abilities mtu unazaliwa na akili zake!.

Ni kama akili, hekima na busara, mtu akili unazaliwa nazo lakini hekima na busara ni aquired. Kuna mtu ana akili sana, kama JPM was a genius, lakini kwenye hekima na busara, very unfortunately... ndio maana kwanza tuliwashauri asaidiwe kupata busara Je, aachwe aseme tu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?

Kisha tukawashauri wasaidizi wake wamsaidie Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Akili ni mtu unazaliwa nazo lakini hekima na busara is acquired.

P
 
Pasco huwa ana "inside info"
Hata plan ya Tec kumtaka Philip Mpango mwaka 2025 ..Pasco anaijua lakini huwezi jua kama anajua..
Mkuu The Boss!, nimesisimka!, you are a genius!. Japo watu humu wananiona kama nina akili, lakini kuna watu wanaona mbali mpaka!. Believe it or not, hili ndio nimelijua leo!.

Mimi ni Mkatoliki, lakini baada ya ule waraka wa TEC, niliuliza Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa? Wakatoliki wakanijia juu!.

Jumapili iliyofuata Waraka ukasomwa madhabahuni kwenye makanisa yote, misa zote, kisha ukashushwa ngazi ya Jumuiya, nikauliza tena Je, Wajua Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Ili Kuepuka Kuchanganya Dini na Siasa, Kuna Haja Waumini Tuambiwe Ukweli Waraka wa TEC Sio Neno la Mungu? Wakatoliki walizidi kunijia juu!.

Nikamtafuta Father Kitima, ili nifanya nae mahojiano ya just 5 minutes!, aliingea for 30 minutes!, mimi si unanijua ni mtu wa maswali magumu ya kumbananisha, nikawa kila nikimbananisha Father Kitima, anachomoa!, nikamnote kama ananipiga piga chenga fulani!. Sasa leo baada ya kukusoma wewe ndio naelewa!.

Naelekea 60 soon, hivyo najiandaa kwa a honorable media exist ili ni venture on something else, nitakutumia sana ili tulisaidie taifa letu hili!.

Huko nyuma niliwahi kuuliza, kwanini akiwa ni Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki?!, nikauliza ni inatokea tuu coincidentally au ina coincidentishwa?. Bandiko lile lilifutwa fasta, maana hata Mkuu wetu humu pia ni Mkurasini mzuri mtiifu, ukibeza chochote cha Kurasini...!, jua..., baada ya waraka kuna bandiko nilipandisha humu,... dakika sifuri!. Kuna wakati nilishauri humu mamlaka ya modes kufuta bandiko lolote, yasiingiliwe, ila bandiko la mtu likifuta at least thread starter ajulishwe reasons!.

Sasa leo ndio umenifungua macho!.
Kumbe...!. Hawa Jamaa viboko!.
P
 
Habari nyeti hawezi pata mtu back,unaweza kuwa unatumiwa na system Kwa kujua au kutojua Kwa kutumia hiyo hiyo career Yako Kwa sababu maalumu
Mkuu ChoiceVariable , kwanza you are absolutely right, kazi ya system is to get info, hivyo mtu unaweza usiwe mtu wao, wakawatumia watu waliokaribu na wewe, and sometimes hadi vimada wako, wana nam recruit as an informer. Sisi ma journalists watu wa kazi mbili mbili, wenzetu wengi wapo.

Enzi za Corona, baada ya JPM kuigomea chanjo, 'jamaa' wakaileta chanjo ya Sputnik ya Urusi kimya kimya kwa siri, wakawapeleka watu wao muhimu kuchanjia Zanzibar!, kwenye baadhi ya newsrooms zetu, waandishi wenzetu walikwenda kuchanja Zanzibar, kimya kimya ndio sie wengine nikaelewa. If you are their target, then they'll recruit hadi msichana wako wa kazi za ndani!, madereva ndio usiseme!.

Mimi nikiwa TBC, nilitumiwa jamaa 2 wa GSU, ofisini kwa Mkurugenzi, kwa jinsi walivyomfanya Mzee wangu ( Rip), nikawa sitaki hata kuwasikia. Japo Mkurugenzi wa TBC alinitambulisha kwa majina tuu bila vyeo, kiukweli niliwajibu mbovu!. Baada ya mahojiano ndipo nikaelezwa kumbe mmoja wa wawili wale ndie Mkuu wa GSU!. I felt sorry for nilivyowajibu makavu live, (ila kutokujali kabisa is bad sometimes!), mimi tukija kwenye ukweli ni sijali kitu wala sijali mtu ni nani!, nitasema ukweli daima!, na huo nadhani ukawa ndio mwanzo wa mwisho wangu serikalini!.

Sisi wengine ni masikini jeuri, tuko kama Kozi mwana mandanda kulala njaa kupenda!, tuko radhi kulala njaa huku umesimama wima, kuliko kupiga magoti ili upewe mkate!.
P
 
Kwani dunia hii ina siri, baada ya magu kufa kuna ambaye hakujua kuwa amekufa, kabla ya kitangazwa rasmi
Kwenye siku halisi ya kifo cha JPM, kuna vitu viwili,
1. Ukweli Halisi
2. Utii.

Siku zote ni Mwanamke pekee ndie mwenye kuujua ukweli halisi wa Baba wa mtoto ni nani, hivyo wewe kama mtoto mtiifu ukiisha ambiwa na Mama yako kuwa huyu ni Baba yako, anakuwa ndie Baba yako hata kama wewe hufanani nae, unafanana na watoto wa jirani, au unafanana na bosi wa kazini kwa mama, huruhusiwi kuhoji!. Baba yako ni yule uliyeambiwa!.

Kungekuwa na mandatory DNA tests kwa kila familia, familia zingeparaganyika sana!, ndio maana tunapowaambia wanawake wana akili kuliko wanaume, Wanawake Wana Akili Kuliko Wanaume? Hata kwenye Siasa na Uongozi, Wanawake Wameonyesha Uwezo Kuliko Wanaume, mtuelewe na huu ndio ukweli wenyewe.

Siku halisi ya tukio ilitangazwa kwenye mitandao na kijana wao Jasusi ilikuwa ni tarehe 12 March, na mimi kwasababu ni mtu wa kuhoji nilihoji Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5?

Toka ile tarehe 12, Rais wa Zanzibar alifuta all hizi public engagements ziara zilifutwa mikutano iliahirishwa akisubiria taarifa rasmi.

Wakati wa hizo siku tano, huku bara ndio tukaelezwa Mtu yuko fit anapiga kazi!, mara taarifa za hali ya JPM zinatolewa na Balozi wetu wa Zimbabwe!. Mara Mama anapangiwa ziara ya ghafla Tanga!.

Maadam tumetangaziwa rasmi ni tarehe 17, March, kanuni ya utii, inatuelekeza utii kwa mamlaka halali, hivyo tukio limetokea tarehe 17 Machi 2021.
P.
 
Back
Top Bottom