Passo ikiwa kwenye speed ya 80km/h inakuwa sawa na V8 ikiwa kwenye speed hiyo hiyo?

Passo ikiwa kwenye speed 80 haiwezi kulingana na speed 80 ya V8..
Kwa kifupi V8 ikiwa kwenye speed hiyo basi mwenye Passo itabidi aende Hadi speed 120,
Mfano mzuri ni magari kama discovery 4 kwenye odometer zinasoma speed 140 ndiyo mwisho ila jaribu kuivuata na gari yako yenye speed 180 utaona aibu itakayokupata
 
Hivi jamani Passo ikiwa kwenye speed ya 80km/h inakuwa sawa na V8 ikiwa kwenye speed hiyo hiyo au kuna tofauti? Cse magari madogo mengi ni 180KMh, sawa na haya magarri yetu SUVs.

Sasa tofauti ni wapi?
Vipimo tu ndio muhimu.
Kilo 10 za mawe na kilo 10 za manyoya ya kuku uzito ni sawasawa.
 
Utofauti upo kwenye uwezo wa gari kufika speed fulani ndani ya sekunde au dakika. Kwahiyo V8 itawahi kuchomoka na kutangulia kuliko hiyo Passo.
Swali linasema gari zote mbili zikiwa tayari zipo kwenye hiyo speed.
 
Hivi jamani Passo ikiwa kwenye speed ya 80km/h inakuwa sawa na V8 ikiwa kwenye speed hiyo hiyo au kuna tofauti? Cse magari madogo mengi ni 180KMh, sawa na haya magarri yetu SUVs.

Sasa tofauti ni wapi?
Kama zitaondoka wa pamoja toka ziro speed, passo itaachwa nyuma kwa sababu v8 inafika hio speed ndani ya sekunde 2-5 wakati passo naweza fika hio speed kwa dakika 2au 3 hio ni kutokana na ujazo/mzunguko wa engine
 
naona watu wanachanganya speed na acceleration.

mtoa mada ameassume passo imefikia speed ya 80 tayari na V8 imefikia speed hiyo hiyo.

Basically zitakuwa sawa tofauti ni kwamba engine ya passo itakuwa inazunguka zaidi. Ila speed zitakuwa SAWA na ndio maana tochi za askari wa barabarani ni ile ile kwa passo na kwa V8.

kuhusu Ukubwa wa tairi speed zitakuwa sawa ila tairi za passo zitaxunguka zaidi kwasababu ya udogo wake.
 
Hivi jamani Passo ikiwa kwenye speed ya 80km/h inakuwa sawa na V8 ikiwa kwenye speed hiyo hiyo au kuna tofauti? Cse magari madogo mengi ni 180KMh, sawa na haya magarri yetu SUVs.

Sasa tofauti ni wapi?
Tairi ya V8 lina mzingo mkubwa kuliko ya Passo speed sawa ila V8 itatangulia plus ukubwa wa Injini.
 
Passo ikiwa kwenye speed 80 haiwezi kulingana na speed 80 ya V8..
Kwa kifupi V8 ikiwa kwenye speed hiyo basi mwenye Passo itabidi aende Hadi speed 120,
Mfano mzuri ni magari kama discovery 4 kwenye odometer zinasoma speed 140 ndiyo mwisho ila jaribu kuivuata na gari yako yenye speed 180 utaona aibu itakayokupata
Mkuu nakurekebisha mambo mawili.

1. Km/h ni kipimo cha speed, haijalishi ni kwa miguu, gari au baiskeli. Speed 80 km/h ya Passo ndio hiyo hiyo ya V8. Kama ilivyo kilogramu 1 ya mawe na ile ya manyoya, zote ni sawa. Tofauti ni utulivu tu barabarani.

2. Hakuna discovery 4 yenye speed mwisho 140km/h. Hizo 140 ni Miles per hour (MPH) ambayo ni zaidi ya 220 km/h ambayo ni almost sawa tu.
 
Wengi hawajaelewa unachotaka kujua ila kiufupi swali lako majibu yake ni ya Physics ila nitakujibu kiswalihi kufupisha, jibu ni kwamba inaweza kuwa sawa au mmoja wao anaweza kuwa mbele ya mwenzake, usishangae passo akiwa mbele ya V8 kwa speed hiyo hiyo, wengi naona wamefikilia passo hawezi kumzidi V8 kitu ambacho sio kweli,passo anaweza kumzidi V8 kwa speed hiyo hiyo,Mfano kama passo itakuwa imefungwa turbo itapata support ya turbo na kuongeza mzunguko wa engine hivyo itakuwa na acceleration kubwa kuliko V8, ndio maana wengi wanajiuliza why volkuswagen na audi gari ndogo kabisa zenge cc1300 lakini zinamzidi V8 yenye cc4000 mbali katika mwendo? Jibu ni moja tu teknolojia iliyotumika katika gari hizo inaongeza nguvu ya mzunguko katika engine na kufanya kuwa na speed kubwa na haraka zaidi ya engine zisizokuwa na hiyo teknolojia.Teknolojia hizo ni kama Turbo, Grand Tursimo(GT),Gti Gte,Twin turbo,Super charger n.k, jibu ni kwamba Zinaweka kuwa sawa au zisiwe sawa kutoka na factor mbalimbali.
 
Haziwezi kuwa sawa hata kama speed ni sawa, kuna tuvituvitu tunaleta tofauti
Screenshot_20240629_100446_Facebook.jpg
 
Hivi jamani Passo ikiwa kwenye speed ya 80km/h inakuwa sawa na V8 ikiwa kwenye speed hiyo hiyo au kuna tofauti? Cse magari madogo mengi ni 180KMh, sawa na haya magarri yetu SUVs.

Sasa tofauti ni wapi?
tofauti ni pale utakapokutana na tuta. Ndio utajua ipi ni ipi katika kulipita hilo tuta kwa speed hiyo
 
Wengi hawajaelewa unachotaka kujua ila kiufupi swali lako majibu yake ni ya Physics ila nitakujibu kiswalihi kufupisha, jibu ni kwamba inaweza kuwa sawa au mmoja wao anaweza kuwa mbele ya mwenzake, usishangae passo akiwa mbele ya V8 kwa speed hiyo hiyo, wengi naona wamefikilia passo hawezi kumzidi V8 kitu ambacho sio kweli,passo anaweza kumzidi V8 kwa speed hiyo hiyo,Mfano kama passo itakuwa imefungwa turbo itapata support ya turbo na kuongeza mzunguko wa engine hivyo itakuwa na acceleration kubwa kuliko V8, ndio maana wengi wanajiuliza why volkuswagen na audi gari ndogo kabisa zenge cc1300 lakini zinamzidi V8 yenye cc4000 mbali katika mwendo? Jibu ni moja tu teknolojia iliyotumika katika gari hizo inaongeza nguvu ya mzunguko katika engine na kufanya kuwa na speed kubwa na haraka zaidi ya engine zisizokuwa na hiyo teknolojia.Teknolojia hizo ni kama Turbo, Grand Tursimo(GT),Gti Gte,Twin turbo,Super charger n.k, jibu ni kwamba Zinaweka kuwa sawa au zisiwe sawa kutoka na factor mbalimbali.
Angalau wewe unajua maana ya hii forum. Maelezo ya kitaalamu angalau nimepata cha kufanyia homework. Thanks9🙏🙏
 
Ukienda kimahesaba za pysics na law zake zote ziko speed moja ila practically haziwezi kua sawa kwa sababu hii
1. Kwenye mlima passo ataanza kusieze kwa sababu engine ni ndogo na hivo itaachwa
Sidhan hata kama physics ina support hilo.
Consider circumference ya tyre ya V8 na circumference ya tyre ya passo..

1 revolution for each of those two will cover different metres (un-equal distances)
 
Back
Top Bottom