Okay, unajua sport cars, lengo lake kubwa ni kufurahia kuendesha. Ndio maana zinaitwa drivers cars, kuliko kutoa comfortability. So, ili kupata that feeling ya kuwa connected na barabara, kuna vitu huwa vinafanyika kwenye tuning ya gari. Kwanza kabisa, lazima urefu au height ya gari iwe lowered. Ndo maana unaona gari kama BMW 3 Series ziko chini. Kina Ferrari, Lamborghini hizo siongelei kabisa, maana ni kama zinagusa barabara kabisa.
Sasa ukishafanya hivyo, lengo ni kuhakikisha gari halilalii upande mmoja wakati unakata kona. So unaweza kata kona ya kulia then ukarudi kushoto na gari bado limetulia njiani. Vile ni fupi, na suspension hazinesi saana. Hii ndio tunaita handling. Sasa suspsion kuwa comfortable, inamaana ile coil spring yake, ni ndefu, ili iweze kunepa saana. So inapokata kona za ghafla, gari likinepa kushoto na kurudi kulia linakosa balance, so inakuwa rahisi kupinduka. Sawa na mtu mrefu na mfupi kwenye kupiga kona za ghafla.
Suspension ikiwa comfortable, gari inakuwa na grip kubwa, meaning inashika barabara saana. Sasa hii sio nzuri kwa sport cars, maana ikishika barabara inamaanisha gari linakuwa halikimbii saana au linatumia nguvu kubwa kukimbia.