Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Passport ya Tundu Lissu iliibwaje akiwa Ujerumani?

Mtu anapopaza sauti ya msaada kwa boss Mkuu, maana yake wa chini walishamkwamisha!!!

Hapa kwenye jukwaa nimewahi kumsoma Mwanakijiji akiomba msaada wa kupata passport yake mpya,baada ya mwaka sasa kuzungushwa hapo USA.

Wote tuliona Mange Kimambi pia akipata passport baada kufanya kazi ya Mama ilihali zaidi ya mwaka hakupewa.

Kati ya hao watu wawili na ukiwaunganisha dhidi ya Lissu,yupi CCM hawampendi?!!
Well said [emoji106][emoji106]
 
Ninachokiona hapo ni kuwa Tudu Lissu hakutegemea kama mama atakutana nae, alipoomba kukutana nae alikuwa katupa turufu na alishakuwa na jibu la kukataliwa kuonana nae kwa 100%, ili apayuke kisiasa. Mama kamziba mdomo na akawa hana la kusema hajui amwambie nini, akaanza kubwabwaja.
Si kweli, amejibu hilo kule space kwamba agenda alizoongea walikubaliana na viongozi wenzake plus hizo zake mwenyewe.
 
Afrika kuna ukiritimba.

Miguna Miguna alikua deported kwa madai ameishi Kenya kama raia wa Canada.

Inawezekanaje mtu aliyezaliwa Kenya na kuishi uhamishoni miongo miwili kwa kukimbia utawala dhalimu unasema sio raia?

Miguna alipoenda tofauti nao wakatumia loophole sasa kumfanyia deportation kwa madai ameukana uraia wa Kenya hivyo afanye kuomba upya.

Katiba mpya ya Kenya ya 2010 inaruhusu uraia pacha sasa kwanini hawamruhusu?

Katika majaribio yake 2 ya kurudi yamegonga mwamba kuanzia 2018 mpaka 2021, na mahakama zimeruhusu aingie ila serikali inakataa hii ndio Afrika na anaambiwa akiingia ataingia kwa tourist visa.

Kuomba hati ya kusafiria mpya inapopotea ya zamani inajulikaka , Lissu na Miguna Miguna ni wanasheria na raia halali wa mataifa yao na hatua hizo wanazifahamu ila watanyimwa tu mwisho wa siku

Tatizo kubwa wamawekewa ngumu sababu ni wakosoaji wakubwa na wa wazi kwa serikali na Africa taasisi zinanyenyekea serikali sio kufuata sheria.
Well said.
 
Tuache siasa, hujui hata alisema atarudi lini. Waacheni wapinzani wahoji serikali, ambako kuhoji kwake waita kuropoka, uliyepo madaraka uwe waleta majibu sahihi.

Kuihoji Serikali ni muhimu sana. Cha ajabu ni kwamba kuna watu wanakuwa mafundi sana wa kuhoji wakiwa huko space, lakini wakikutana na wanaopaswa kuwabana ili wapate majibu ya hoja zao hawatumii hiyo fursa ipasavyo. Wanalialia tu kuhusu kiinua mgongo na maslahi mengine binafsi.

Tukisema politicians siku zote wanapigania maslahi yao binafsi, baadhi ya watu hawaelewi na wako tayari kutumika kama makarai!
 
Aliondoka bila passport. Alishikwa mkono na balozi wa Ujerumani na balozi wa Marekani.
 
Pia Lissu kasema marehemu Sitta alivyoumwa huko UK alitibiwa na bunge wakati alikuwa si mbunge na hakukuwa na nongwa.
Daah hiyo zambi itamtafuna sana hela ni kodi za Wananchi na pia zipo hutaki kumtibu mtumishi mwenzio kisa mpo vyama tofauti na kwa hili inaonekana kabisa alikuwepo kwenye njama ya wapiga risasi...
 
View attachment 2122152

Angalia jinsi anavyomdharau! Hakuna cha Barakoa wala nini, sasa nani ana-Covid hapo?

TL ni mwongo, huwezi kupata asylum nchi yoyote ile ukabaki na passport ya nchi uliyokimbia. Huyu Mama mwacheni, angoje atakachovuna. Ni aibu na fedheha kwa rais aliye madarakani kukutana na raia wa nchi yako ambaye ni mkimbizi nje ya nchi yako.
Shida mnadanganywa sana mimi nilianza kupata asylum SA ili nipate kibali cha kusoma na kufanya kazi walinipa na passport waliniachia passport ni mali yangu sio yao soma nyuma ya passport utaelewa yupo bwana mdogo mmoja nilimsafirisha mwenyewe kutoka SA kwenda UK alipofika akachukua asylum ya Kongo DRC maana alikua anaijua DRC vizuri baadae tukafuta mambo ya asylum tukachukua Passport ya SA na ID yake ili kuifanyia kazi na ishu zingine za Safari ila hii ya sasa hivi kwa mfumo waliouweka ni ngumu kufoji maana unaonekana tofauti na mwanzo ilivyokua Watanzania wengi waliopo UK walikua na ukimbizi wa Pemba enzi zile za Mkapa na passpprt zao wanazo ukikidhi vigezo ndio utapewa passport ya kikimbizi ila pia passport yako unabaki nayo wao passport sio big deal maana hata sio kigezo cha kupata ukimbizi...watu walikua wanakaa Camp ya Namibia ya wakimbizi na passport zao maisha yakiwa ok wanakimbia na passport zao popote pale maana mipakani wanachukua hela kurudisha tarehe au kupeleka tarehe mbele kuonyesha ulitoka mpaka kesho mipaka mingi ndio ishu zao hizo ila unawalipa...
 
Hayo yote yalitokea Kenya ambayo ni mfano bora wa democrasia kwa mujibu wa chadema?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
Umeelewa hata nilichoandika
Shida mnadanganywa sana mimi nilianza kupata asylum SA ili nipate kibali cha kusoma na kufanya kazi walinipa na passport waliniachia passport ni mali yangu sio yao soma nyuma ya passport utaelewa yupo bwana mdogo mmoja nilimsafirisha mwenyewe kutoka SA kwenda UK alipofika akachukua asylum ya Kongo DRC maana alikua anaijua DRC vizuri baadae tukafuta mambo ya asylum tukachukua Passport ya SA na ID yake ili kuifanyia kazi na ishu zingine za Safari ila hii ya sasa hivi kwa mfumo waliouweka ni ngumu kufoji maana unaonekana tofauti na mwanzo ilivyokua Watanzania wengi waliopo UK walikua na ukimbizi wa Pemba enzi zile za Mkapa na passpprt zao wanazo ukikidhi vigezo ndio utapewa passport ya kikimbizi ila pia passport yako unabaki nayo wao passport sio big deal maana hata sio kigezo cha kupata ukimbizi...watu walikua wanakaa Camp ya Namibia ya wakimbizi na passport zao maisha yakiwa ok wanakimbia na passport zao popote pale maana mipakani wanachukua hela kurudisha tarehe au kupeleka tarehe mbele kuonyesha ulitoka mpaka kesho mipaka mingi ndio ishu zao hizo ila unawalipa...
Umeelezea vizuri kuna watu wamesafiri sana ila nashangaa hawajui vitu exposure bado zero licha ya kusafiri.
 
Taratibu za kupata passport mpya kama uliyokuwa nayo imepotea, zipo wazi.

Kwanini uombe msaada wa Rais?

Kama alikuwa anakataliwa, alikuwa anakataliwa kwa misingi gani?

Bado sielewi aisee!
Wakati mwingine kuna mambo yanachekesha!!Hivi kweli TL ni raia wa kawaida wa Tanzania?Je mmesahau ya kuwa alipelekwa uwanja wa ndege kwa mwavuli wa ubalozi wa nje?Ni kweli kuwa balozi za nje zilikuwa haziujui ukweli?
 
Yawezekana alifuatilia wakamgomea
Sijaelewa kabisa!

Tundu Lissu kasema kuwa amemuomba Rais Samia amsaidie kupata passport mpya kwa sababu aliyokuwa nayo iliibwa mwezi uliopita huko Ujerumani.

Aliyeiiba hiyo passport ni nani? Na iliibwa au yeye aliipoteza na anachanganya kupoteza na kuibwa?

Na kama iliibwa, kwa nini hilo liwe suala la Rais kumsaidia yeye aipate tena passport yake?

Kwani hakuna taratibu za kufuata pale passport yako inapoibwa au inapopotea mpaka yeye amtumie Rais kuipata mpya?

Kwa kweli kwenye hili sijamuelewa!
 
Back
Top Bottom