Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Pata ushauri wa bure wa kesi yoyote, Ardhi, Jinai na Madai (Thanks Giving Days)

Kitu gani napaswa kufata endapo nikiwa sijapewa stahiki zangu na kuonewa ktk kusitisha mkataba wangu Kati yangu na muajili
Unapaswa kufanya juhudi binafsi ikiwemo kuwakumbusha hao waajili wako wakulipe masalia yako na haki zako walizo kukatisha, kama wataonekana hawana Jema basi utaenda Tume ya Usuluhishi na upatanishi CMA kwa ajili ya kupeleleka malalamiko rasmi na kuanza moja kisheria.

Tume hii iko kama mahakama na inafanya kazi kila kitu sawa na Mahakama, lakini inashauriwa kama una hisi kuna haki zako kweli zinanyanganywa basi mtafute wakili yoyote maeneo ya karibu ulipo akusaidie.
 
Unapaswa kufanya juhudi binafsi ikiwemo kuwakumbusha hao waajili wako wakulipe masalia yako na haki zako walizo kukatisha, kama wataonekana hawana Jema basi utaenda Tume ya Usuluhishi na upatanishi CMA kwa ajili ya kupeleleka malalamiko rasmi na kuanza moja kisheria, tume hii iko kama mahakama na inafanya kazi kila kitu sawa na Mahakama, lakini inashauriwa kama una hisi kuna haki zako kweli zinanyanganywa basi mtafute wakili yoyote maeneo ya karibu ulipo akusaidie.
Asante
 
Hizi nyuzi zinanichanganya, kumbe zimesha fika mbili.

Nashauri watu wautumie huu wa december badala ya ule wa February.
 
Mara ya mwisho nilifanya hivi ilikua mwaka jana na wengi niliwasaidia bure tu, lakini hawakushukuru au wengine kuleta mrejesho.

Naam wakili nipo likizo toka hapa kijijini nilipo so naimani naweza kutoa msaada walau ata robo tu tokana na maarifa machache ya sheria niliyo bahatika kuya soma.

Pro bono ya hapa na pale 😀, yasiwe yakuumiza kichwa saanaa wala kufikirisha sanaa, ni hivi vya hapa na pale tu.
Kuna rafiki yangu wa karibu sana amezinguana na mkewe kama wiki 2 zimepita. Kwa influence ya wazazi wa binti imefunguliwa kesi ya kuwa jamaa kampiga mkewe na kumuumiza hivyo kwa madai ya jamaa baada yakuitwa polisi aliambiwa mkewe alifika pale kuchukua pf3 na akaenda hosptal akiwa na kaka zake.

Baadae mkewe aliondoka akamuaga mumewe kuwa anaenda nyumbani kwao na atarudi. Japo aliondoka na kaka zake ila hakusema kuwa ameenda kumshtaki jamaa polisi au hospital.

Jamaa ndo jana kapigiwa simu polisi akaripoti na baada ya kumchukua maelezo jamaa alikana kuwa hajampiga. Mshtaki ambae ni mke wa jamaa hakuwepo ila ajabu jamaa kawekwa mahabusu ndo bosi wake kazini akaenda kumdhamini.

Sasa wadau na wanasheria hii kitu imekaaje nimshauri nn jamaa yangu
 
Kuna rafiki yangu wa karibu sana amezinguana na mkewe kama wiki 2 zimepita. Kwa influence ya wazazi wa binti imefunguliwa kesi ya kuwa jamaa kampiga mkewe na kumuumiza hivyo kwa madai ya jamaa baada yakuitwa polisi aliambiwa mkewe alifika pale kuchukua pf3 na akaenda hosptal akiwa na kaka zake.

Baadae mkewe aliondoka akamuaga mumewe kuwa anaenda nyumbani kwao na atarudi. Japo aliondoka na kaka zake ila hakusema kuwa ameenda kumshtaki jamaa polisi au hospital....
Amewekwa sababu katuhumiwa tu na yeye ni mshukiwa wa jinai, so atulie aone kama atafikishwa kokote then atajitetea tu, kila mtu anaweza kua mtuhumiwa na sio kila mtu anaweza kukutwa na hatia.
 
Mku

Mkuu gharama za upimiwaji viwanja/kiwanja haziwezi kuzidi laki na elf 50, na hii ilishushwa na wizara ya ardhi toka mwaka jana ambako kiasi kilikua ni 250,000. so hakuna anaetakiwa kuzidisha laki na elf 50 na waziri alionya sanaa, tafta haya makampuni huko ulipo yatakuwepo tu Visible Planners au Afro Max, wanafuata bei hio hio ya laki na 50.

Lakini hii nazani hufanyika pale ambapo zoezi la upimaji hufanyika kwa pamoja. Sasa inapokuwa kwamba unahitaji kupimiwa peke yako kwa wakati wako gharama yaweza kuongezeka sababu mahitaji ya rasilimali yanakuwa ni yaleyale kama walivyopimiwa wengi wakati mwingine.

Kwa hiyo bora awaombe wampunguzue gharama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini hii nazani hufanyika pale ambapo zoezi la upimaji hufanyika kwa pamoja.
Sasa inapokuwa kwamba unahitaji kupimiwa peke yako kwa wakati wako gharama yaweza kuongezeka sababu mahitaji ya rasilimali yanakuwa ni yaleyale kama walivyopimiwa wengi wakati mwingine.
Kwa hiyo bora awaombe wampunguzue gharama.

Sent using Jamii Forums mobile app
ni sawa akili njema.
 
Wakuu mimi ni muajiriwa serekalini .Nilijenga nyumba ya kuishi eneo taasisi hiyo ya serekali lakini baada ya miaka minne nikafanikiwa kujenga nyumba yangu binafsi.

Nilipotaka kuhamia kwangu mkuu wa ile taasisi akaniambia nitalipwa fidia ,hiyo ilikuwa 2018 lakini mpaka sasa nimeshadai lakini sioni dalili ya kulipwa maana imekuwa ni danadana tu .

Naomba mnisaidie nichukue hatua gani za kisheria ili niweze kupata haki yangu
 
Hebu andika ueleweke!

Kujieleza tu mtihani!

Hapa naona nyumba zaidi ya tatu lakini umejikoroga hueleweki hata unazungumzia nini!
 
Hebu andika ueleweke!

Kujieleza tu mtihani!

Hapa naona nyumba zaidi ya tatu lakini umejikoroga hueleweki hata unazungumzia nini!
Kwa kifupi ni hivi nilijenga nyumba eneo la taasisi ili niweze kupata pa kujisitiri huku nikiwa na mpango wa kujenga nyumba nyingine kwenye eneo langu binafsi. Na nilifanikiwa kufanya hivyo mwaka 2018 nikahamia na kuiacha nyumba niliyojenga eneo la taasisi niliyoahidiwa kufidiwa

SAsa tangu 2018 nadai lakini imekuwa ni danadana.Je nichukue hatua gani niweze kupata haki yangu?
 
Amewekwa sababu katuhumiwa tu na yeye ni mshukiwa wa jinai, so atulie aone kama atafikishwa kokote then atajitetea tu, kila mtu anaweza kua mtuhumiwa na sio kila mtu anaweza kukutwa na hatia.
Inawezekana kesi iliyofutwa mahakamani kufufuliwa na kuanza kusikilizwa upya endapo mlalamikaji akiamua hivyo? Yan assume mshtaki alipigwa ila akaamua kufuta kesi baadae ameona hali yake ya kiafya imekuwa mbaya je anaweza kwenda kuifufua hiyo kesi?
 
Kesi za madai ina ruhusiwa inaitwa 'Restoration', kama ilikua madai ambayo hayakufikia ukomo, mdai alipotea tu. Kama hio alifuta mahakamani kabisa kwamba hakua na nia ya kuendelea nayo tena hio haiwezekani. Labda aianzishe upya na malalamiko mengine.
 
Kwenye kufuta kuna walaka wowote unatolewa kwa mshitaki au mshtakiwa?
 
Mara ya mwisho nilifanya hivi ilikua mwaka jana na wengi niliwasaidia bure tu, lakini hawakushukuru au wengine kuleta mrejesho.

Naam wakili nipo likizo toka hapa kijijini nilipo so naimani naweza kutoa msaada walau ata robo tu tokana na maarifa machache ya sheria niliyo bahatika kuya soma.

Pro bono ya hapa na pale 😀, yasiwe yakuumiza kichwa saanaa wala kufikirisha sanaa, ni hivi vya hapa na pale tu.
Kuna njemba imemporomoshea my wife wangu matusi kupitia text messages, njemba hii ilianzisha mawasiliano yasiyo na kichwa wala miguu wife akalionya lisiendelee kutuma ujumbe,

likakiri halitorudia, baada ya muda flani likarudi kwa texts tena kitendo kilichopelekea wife kwa jazba ktk kumtaka ajitambulishe na kusudi lake ni lipi maana hakusave namba yake, wife akamuita mjinga na mpumbavu. (alikuwa anajibu upuuzi) Njemba baada ya kuona hivyo likaporomosha matusi ya kidhalilishaji. Naomba kujua kama kisheria lina mlango wa kutokea maana mkakati uliopo ni kumfikisha mbele ya sheria.

NB. Utetezi wake ilikuwa ni kuwa yeye amereact baada ya kutukanwa.
 
Kuna njemba imemporomoshea my wife wangu matusi kupitia text messages, njemba hii ilianzisha mawasiliano yasiyo na kichwa wala miguu wife akalionya lisiendelee kutuma ujumbe, likakiri halitorudia, baada ya muda flani likarudi kwa texts tena kitendo kilichopelekea wife kwa jazba ktk kumtaka ajitambulishe na kusudi lake ni lipi maana hakusave namba yake, wife akamuita mjinga na mpumbavu. (alikuwa anajibu upuuzi) Njemba baada ya kuona hivyo likaporomosha matusi ya kidhalilishaji. Naomba kujua kama kisheria lina mlango wa kutokea maana mkakati uliopo ni kumfikisha mbele ya sheria. NB. Utetezi wake ilikuwa ni kuwa yeye amereact baada ya kutukanwa.
Ilo ni shambulio la aibu, ila kuitwa mjinga au mpumbavu sio tusi ni hali ya ufikiria anayoidhania yule unae wasiliana nae, kila mtu anayo haki ya kuonekana mjinga au mpumbavu kwa watu wengine.
 
Ilo ni shambulio la aibu, ila kuitwa mjinga au mpumbavu sio tusi ni hali ya ufikiria anayoidhania yule unae wasiliana nae, kila mtu anayo haki ya kuonekana mjinga au mpumbavu kwa watu wengine.
Shukrani mkuu, na je ninaweza kufungua kesi kwa niaba ya wife ili mimi binafsi nisimame na huyo mtukanaji wa mali za watu?
 
Shukrani mkuu, na je ninaweza kufungua kesi kwa niaba ya wife ili mimi binafsi nisimame na huyo mtukanaji wa mali za watu?
Hapana, ila unaweza kua unaenda na mkeo mahakamani kila mara na uka mkampani hatua kwa hatua ikiwezekana ukamuandikia vya kusema, ina ruhusiwa, ila mwende mahakama ya mwanzo.
 
Back
Top Bottom