Pato la kila Mkoa: Dar es Salaam yazidi kuongoza ikifuatiwa na Mwanza, Njombe na Katavi zashika mkia

Pato la kila Mkoa: Dar es Salaam yazidi kuongoza ikifuatiwa na Mwanza, Njombe na Katavi zashika mkia

Hapo ndo shangaa, low minded pwaniz leo wawa suppress akili kubwa kutoka lake zone just kwa cheap politics......
Ukiondoa takwimu hizi za mapato kimkoa ambazo bado Pwanis wanaongoza, takwimu za umaskini wa kimapato kwa mtu mmoja mmoja kimkoa mikoa ya Kanda ya Ziwa inaongoza kwa kuwa na maskini wengi huku huku mikoa ya Pwani na Dar ikiingia tatu Bora kwa mikoa yenye unafuu. Kwa hiyo mkuu mnahitaji kupigania ili mfikie kwenye uhalisia wa kuwa na akili.
 
**** watu roho inawauma sana tena nataka niwaambie mimi niko dar! Bila bandari Dar kwa mwanza wanapambana tu! Maana ukiangalia nyumba mitaani za makazi mtaa mingi ya mwanza ina nyumba kali kuzidi dar! Maana makazi mengi dar ni ya zamani isipokuwa mitaa ya kinyerezi mbezi,tegeta na kigamboni,
Sasa mkuu bas na ninyi bila ziwa na madini mwanza Ingekuwaje umejaribu kuwaza hayo?

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Ruvuma no.10 ni mkoa wangu lakini naomba wadau nijue kwa kigezo kipi imeshika iyo no.10 sabab najua tunategemea Sana kilimo Cha zao moja ( mahindi) na masoko nowdays yameyumba Hali ni mbaya Sana
 
Ofisi ya taifa ya takwimu imetoa pato la kila mkoa nchini Tanzania, mkoa wa Dar es salaam wazidi kuongoza ukifuatiwa na Mwanza.

Mikoa ya Katavi na Njombe imeshika mkia kwa kua na pato dogo sana ukilinganisha na mikoa mingine.

Kwenye kumi bora kanda ya ziwa imeingiza mikoa 3, Mwanza, Shinyanga na Geita kwa jumla ya Trilioni 25 sawa na mkoa wa Dar es Salaam.

Kanda ya kaskazini, pato la mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ndio inafikia pato la mkoa wa Mwanza. Utajiri wa Arusha, Kilimanjaro na Tanga ni sawa na utajiri wa Mwanza na Shinyanga.

Kwa Takwimu za NBS, ukitoa Dar, kanda inayofuatia kwa utajiri ni anda ya ziwa, ikifuatiwa na Kaskazini huku Kusini kwa Lindi, Mtwara na jirani yao Pwani wakishika mkia.

Kanda ya nyanda za Juu kusini Mbeya inawabeba ila imezungukwa na mikoa choka mbaya kama Katavi na Njombe hivyo kuchangia kanda hiyo kuonekana ni choka mbaya mbavu za mbwa.

Watu wa Mara tukomae tuiondoe kilimanjaro ama Ruvuma hapo juu tuingie top 10.

Tunataka mapato ya per Capita income,GDP haitakusaidia Sana mkuu ni kujifariji.

GDP yenyewe ya huko Kanda ya Ziwa ni madini ya dhahabu amvayo huishia Kwenye makampuni, serikali na kiduchu ndio huenda kwa watu wachache..

Huko Njombe ambako unadai WA Mwisho ukileta GDP Per Capita income inashindana na Dar tuu.

Mwisho Takwimu za Shinyanga na Mwanza zinahusisha Mkoa was Simiyu kiasi kwamba Kama Mbeya isingegawanywa kuunda Songwe basi ingekuwa no.2 nyuma ya Dar na huko hakuna Migodi huko ndiko Kuna watu waliostawi Sasa.

Tunataka Takwimu independent za Simiyu,tuone aibu ya baadhi ya mikoa hapa.
 
Ukiondoa takwimu hizi za mapato kimkoa ambazo bado Pwanis wanaongoza, takwimu za umaskini wa kimapato kwa mtu mmoja mmoja kimkoa mikoa ya Kanda ya Ziwa inaongoza kwa kuwa na maskini wengi huku huku mikoa ya Pwani na Dar ikiingia tatu Bora kwa mikoa yenye unafuu. Kwa hiyo mkuu mnahitaji kupigania ili mfikie kwenye uhalisia wa kuwa na akili.
Kwa hiyo ubuyu wa mia mia na vitumbua ndo vifanye watu wa Dar na Pwani wawe matajiri, unajivunia utajiri wa watu wa kuja.....
 
Naona ma yakhee wa waja leo warudi leo wanakimbiza arachuga na kwa kina mangi
 
Dodoma vipi?

Mwaka Kama iliongoza kwa makusa yo ya Kodi kuliko mikoa yote Tanzania.
Kuna sehemu mtu mmoja alisema wana jf wengi wana uelewa mdogo sana wa mambo na si wafatiliaji bali ni wafata mkumbo....
Habari inazungumzia pato la kimkoa wewe unaongelea makusanyo ya halmashauri.... inabidi urudishwe shule ufundishwe maana ya pato na utofauti wake na makusanyo....
 
Tuna Ziwa, tunauza zaidi ya 90% ya samaki zinazouzwa nje ya nchi.

Tunauza zaidi ya 90% ya pamba inayozalishwa Tanzania, tunazalisha sisi.

Tunazalisha na kuuza 100% ya dhahabu nje na ndani ya nchi.

Tunazalisha na kuuza 100% ya almasi ndani na nje ya nchi.

Tunazalisha na kuuza zaidi ya 50% ya kahawa nje na ndani ya nchi.

Tuna Serengeti, ambayo inavutia zadi ya 80% ya watalii wanaoitembelea Tanzania kila mwaka. Serengeti ndio utalii wa Tanzania. Bila Serengeti wazungu Tanzania tungeishia kuwaona kwenye tv.

Hivyo kwa kuleta zaidi ya 80% ya watalii Tanzania, tunaingiza zaidi ya 80% ya mapato ya utalii Tanzania.

Mifugo, usisahau tunafuga na kuzalisha zaidi 50% ya mifugo na mazao yake kama ngozi, maziwa, pembe, mapumbu, nk😂. Tanzania.

Tuna wanaume jasiri kuliko wanaume wa makabila yote Tanzania, wako Mara.

Tuna wanawake warembo, weusi, walioumbika na wenye shape nawanaomwaga maji Tanzania nzima wako Kagera. Wanawake weupe warefu wa kisukuma na wanawake jasiri roho ngumu wa Mara😂.

Wanawake wa mara kwa ujasiri wanazidi wanaume wa mikoa ya pwani na Iringa.

Wife anaona ametoka bafuni na taulo tu hapa ameniita, narudi.
Kwa kuongezea Kuna yule mwanamke wa Mara alimnyang'anya jambazi smg kabisa ikiwa na risasi zimejaa kwa magazine.
Yaani ulivyoipamba lake zone.
Wangekuwa ndugu zetu ukanda Fulani wangekomaa wajitenge Mana wananyonywa na wakanda wengine.
Na ndo Mana wanataka kuleta Sera ya ukanda.
Jana nacheki itv Siro Mara,mabeyo simiyu wote walikuwa wanaongea sijui Nini.
Lake zone Askari wengi ndio wametokea huku ,tukidai nchi yetu nadhani wengine mtakufa njaa Mana chakula kingi kinatokea huku
 
Mkuu nikusahihishe..

Kanda ya Ziwa Mara,Mwanza,Kagera,Geita na Shinyanga.

Kanda ya Mashariki
Dar,Pwani na Morogoro.

Kanda ya kati
Dodoma,Singida na Tabora

Kanda ya Kaskazini
Kilimanjaro, Arusha,Tanga na Manyara.

Kanda ya kusini
Lindi,Mtwara,Ruvuma

Kanda ya Magharibi
Kigoma,Katavi, Songwe..

Nyanda za juu Kusini
Mbeya,Iringa,Njombe
..............

So obviously Kanda ya Mashariki ndio kinara.
Simiyu umeiacha wapi..usisahau na mkoa wa chato ambao siku si nyingi utatangazwa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ukiondoa takwimu hizi za mapato kimkoa ambazo bado Pwanis wanaongoza, takwimu za umaskini wa kimapato kwa mtu mmoja mmoja kimkoa mikoa ya Kanda ya Ziwa inaongoza kwa kuwa na maskini wengi huku huku mikoa ya Pwani na Dar ikiingia tatu Bora kwa mikoa yenye unafuu. Kwa hiyo mkuu mnahitaji kupigania ili mfikie kwenye uhalisia wa kuwa na akili.
Hapo inshu ni population density.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa mihemko hawatakuelewa.

Wewe nae ni mpumbavu mwenzake! Eti mihemko! Hivi kweli mji unaoongoza kwa mbali sana mapato kwa nchi hii uje kupitwa na mkoa ambao hata mapato yake sio ya 3 kitaifa?

Angalia hili hapa! Walilinganisha asilimia za makusanyo dhidi ya malengo. Na kwa kuwa namuelezea mbwiga nitatoa mfano hapa. Lengo la Dar ni kukusanya 100m na Dodoma 70m. Dodoma mwisho wa mwaka kakusanya 68m sawa na 97% Dar kakusanya 90m sawa na 90%. Ukilinganisha ufanisi utaona Dom kaizi Dar kwa 7% lakini alizokusanya Dar ni 22m zaidi!!

Ni malengo ya makusanyo ndio Dodoma alikuwa wa kwanza. Sio kiasi cha makusanyo! Ukianza kuelewa tofauti hiyo utamsaidia mwenzako.
 
Tunataka mapato ya per Capita income,GDP haitakusaidia Sana mkuu ni kujifariji.

GDP yenyewe ya huko Kanda ya Ziwa ni madini ya dhahabu amvayo huishia Kwenye makampuni, serikali na kiduchu ndio huenda kwa watu wachache..

Huko Njombe ambako unadai WA Mwisho ukileta GDP Per Capita income inashindana na Dar tuu.

Mwisho Takwimu za Shinyanga na Mwanza zinahusisha Mkoa was Simiyu kiasi kwamba Kama Mbeya isingegawanywa kuunda Songwe basi ingekuwa no.2 nyuma ya Dar na huko hakuna Migodi huko ndiko Kuna watu waliostawi Sasa.

Tunataka Takwimu independent za Simiyu,tuone aibu ya baadhi ya mikoa hapa.
Huna lolote wivu tu unakusumbua..ingeongoza njombe ungeomba hizo GDP..kaa utulie kanda ya ziwa inaendelea kuupiga mwingi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom