Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,774
- 47,866
Hicho kitendo cha serikali kumuongezea mkataba mtu ili itafute replacement ambacho umekiita cha kawaida, sisi wasomi wa Human Resource Management tunaita ni Poor succession plan.Katika hali ya kawaida serikali inaweza kumuongezea muda wa utumishi serikalini mtumishi ye yote wakati ikijipanga kuandaa watumishi wengine wanaoweza kuchukua nafasi ya mtumishi anayestaafu. Kitendo cha Mhandisi Mfugale kuongezewa muda wa utumishi wa serikalini kwa muda usiojulikana hadi anafariki dunia ni dharau iliyopindukia kwa watumishi wengine wa TANROADS na kuna kila dalili za ufisadi na wizi wa fedha za umma kupitia TANROADS.
Haingii akilini kuwa hakuna Mtanzania mwingine ye yote ambaye angeshindwa kuchukua nafasi ya Mfugale baada ya kupata mafunzo stahiki! Kuna haja na sababu muhimu kufanyika kwa uchunguzi kwa nini Mfugale akaongezewa muda mrefu kiasi hicho. Aidha kuna haja ya kufanya uchunguzi kwa watumishi wote walioongezewa muda kupindukia uhusiano wao na watawala. Mfano mwingine wa mtumishi aliyeongezewa muda kupindukia ni marehemu Kijazi.
Uchunguzi huu ni muhimu na hasa kipindi hiki ambacho vijana wengi wanakosa ajira na hivyo kuwanyima fursa za kuonyesha vipaji vyao.