Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.
Injinia Patrick A. N. Mfugale
RIP
=====
Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.
Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi
Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.
Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.
Apumzike kwa Aman
Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
- Daraja la Mkapa Rufiji
- Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
- Daraja la Rusumo
- Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
- Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
- Alikuwa Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
- Alikuwa mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency
Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi
Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi