TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Basi tulia kama na wewe kumbe ni Binadamu na siku moja utakufa,kilichokuwa kinakufanya hadi ukashifu kisa Fly Over imepewa jina la Mfugale ni nini basi? Yes,he is Gone,but na wewe utakufa ni swala la muda tu,weka akiba ya maneno na usijitoe ufahamu kisa unatumia fake ID hapa.Uwe na wakati mzuri wa kutafakari maisha yako na si kuwa Judge wa maisha ya wengine.

Umeshindwa kupata hata simango 1 pamoja na kukumbusha kwa mara nyingine?

IMG_20210630_001851_566.jpg

Kwa sababu hiyo nisiache kukwambia sasa, shut up!
 
Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.

Injinia Patrick A. N. Mfugale RIP

=====

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.

Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi

Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.

Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.

Apumzike kwa Aman

Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo
  • Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
  • Alikuwa Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
  • Alikuwa mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi
Je hakuwemo kwenye bandari ya Bwagamoyo?
 
Upumzike kwa amani mhandisi Mfugale umeacha alama zenye kuonekana.

Kule Mwanza ukimuelezea juu ya ujenzi wa daraja mheshimiwa Rais ikakutoka “Hapana” halafu ukagundua unaongea na bosi wako ghafla ukageuza shingo kumcheki kama aina fulani ya kuomba msamaha. Rais alilielewa somo.

Wasalimie wote mliokuwa mnajenga Taifa pamoja.
Alitaka kuleta madharau
 
Hilo jengo porini linazalisha nini, Tanroad huwa wanakaguliwa
Na waliliita jina la huyu marehemu ili unapoenda kukagua ujue unamkagua Nani, wahuni sana. Magu na team yake alihakikisha miradi yake anaipa majina ambayo by any means huwezi kukagua kwa Uhuru na ukatoa reports waziwazi kwa umma.
 
Jiwe, Kijazi, Mfugale hawa wametupiga sana kwenye kujenga barabara, Mungu fundi bado wengine
Barabara ya mwendo kasi ilitolewa report kwamba wamepunguza centimeters kadhaa na ukipiga hesabu ya zile centimeters unapata hela iliyopigwa ni ndefu sana, hakina aliyeongelea walikaa kimya Hawa marehemu mabingwa wa barabara.

Hii ilifuata taarifa za kiintelijensia baada ya kuona Ile barabara ni nyembamba sana magari yanapita kwa shida mno especially kwenye Kona na mikunjo.

Huu uhuni haijawahi kuongelewa tena Ila tunaendelea kudanganyana kwamba hawa watu ndio mashujaa kabisa wakati ndio walikuwa wanapiga hela huko?

Tujibu hoja kwa hoja, leteni upana wa barabara uliowekwa kwenye mchoro na upana uliopo sasa na tuambiane Nani alipunguza na kwa sababu gani ???

Hawa wazee waamue either wastaafu au wajifie kwa aibu. Enough with kujimilikisha mapesa ya umma as if wakifa wanaenda nazo kaburini.

Kibabu kimekaa hapo miaka yote as if hakuna maengineer kabisa?????? Kwamba hatuna engineers?? Ndugu zangu engineers mmeamua kukubali kwamba nyie ni vilaza? No way.

Apumzike tu.
 
Moderator - Naona leo umekwenda kulala mapema sana!
Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale amefariki dunia leo Jumanne Juni 29, 2021 jijini Dodoma.

Katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Joseph Malongo amesema Mfugale atakayekumbukwa kwa kusimamia ujenzi wa barabara na madaraja zaidi ya 1000 nchini amefariki dunia leo saa 5 asubuhi katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Amebainisha kuwa taratibu nyingine za msiba huo zitatolewa baadaye.

Taarifa zilieleza kuwa Mfugale akiwa katika moja ya kikao kazi alijisikia vibaya na kukimbizwa hospitalini ambako akiwa njiani hali yake ilizidi kuwa mbaya.

Awali Waziri wa Ujenzi, Dk Leonard Chamuliho na naibu waziri wa wizara hiyo, Mwita Waitara alieleza kuwa hawana taarifa za kifo cha Mfugale
 
KUNA KAHOPT PALE MADODO KANA JINA LA MTU AKIMALIZIKA HUYO TUNHAMIA WAB MJIANDAE
AUG TO NOV TUTAZIKA SANA KULE UGANDA
 
Umeshindwa kupata hata simango 1 pamoja na kukumbusha kwa mara nyingine?

View attachment 1835045

Kwa sababu hiyo nisiache kukwambia sasa, shut up!

Mpaka unajionea aibu,si urudi kwa posts zako za mwanzo? Wewe kinakuuma nini daraja kuitwa la Mfugale? Huko nyuma ulivyokuwa unaropoka kisa tu Daraja limeitwa la Mfugale ni nini haswa? Punguza makasiriko na hasa kwa Marehemu, hata kama unatumia ID fake but maandishi yako yanakudefine wewe ni mtu wa aina gani.
 
Covid ya tatu hiyo

Jamaa alikuwa mwizi sana na anajua ufisadi wote waliofanya na jiwe kwenye miradi..

Aende kunakostahili.
Very stupid...wewe humfahamu Mfugale...ungekuwa unamfahamu usingetapika ujinga huo..this was a clean man....hajawahi kuchukua hata tone la rushwa...Alipata taabu Sana pale ujenzi kwa msimamo wake wa kutokula rushwa...umewahi kusikia uchafu wowote
 
Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.

Injinia Patrick A. N. Mfugale RIP

=====

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.

Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi

Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.

Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.

Apumzike kwa Aman

Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo
  • Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
  • Alikuwa Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
  • Alikuwa mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi
Oh what a sad day....Mungu ampumzishe salama peponi AMEN.
 
Kama kila mmoja wetu angeamini Kifo kipo basi 'wenye viburi dharau majivuno wajitafakari'
Tujindae
Tutende yaliyo mema
Mungu wetu ni wa visasi na hasira
Hatuijui Kesho
Tuwe waungwana
Tuwe na kiasi
Kufa kupo

Mungu akuepushe na adhabu ya kaburi!
 
Back
Top Bottom