TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Kwa hali niliyokuwa namuona sishangai kufariki kwake. Mungu amjaalie kauli thabiti ana ampunguzie adhabu ya Kaburi. Hakika kwake tutarejea.
Adhabu ya kaburi ndo nini? Akishakufa hamna ajualo ndo ameishia hapo kinachofuata ni Roho kurudi kwa Mungu na ndio itakayo adhibiwa,,mwili wa marehemu hausikii wala hauhisi ni kama udongo so unapoleta imani zako adhabu ya kaburi hata sikuelewi.
 
hii dunia utaijenga na hutaimaliza bali wee ndo utaisha!!
kuna mtu alikuwa na nyumba mtaa mzima,
lakini unazikwa kwenye kashimo kadogo unabanwa hadi mbavu!
kwenye jeneza tunakuona umepiga suti ya bei mbaya kumbe huku chini ndugu zako hawajakuvalisha suruali wala soksi ili kubana matumizi ya pesa zako uliowaachia zisije kuisha!

ukizikwa ndugu ndo wanapofurahi kwamba ndio muda paka kaondoka panya anatawala!!!

baba yangu alikuwa ni tajiri sana ila shida yake alikuwa anatusimanga sana kwa sababu sisi wengine tulichagua kufanyia kazi nyumbani ili faida irudi nyumbani!!

ila alipoanza kuumwa sukari ile ya kinomanoma hapo ndio tukaacha kumuogopa na kumuona ni kama duanzi tuu

ilifikia navuta msuba wangu mbele yake na kumpulizia moshi fuuuuuu!!

god forbid,
i dont give a fkkk

hata alipokufa i didnt care sababu alikuwa ni mkora sana
Hii inahusiana vipi na mada ya kifo cha Mfugale?

Kwamba hakuwa anasaidia watu?
 
Katika kipindi chake hakuna madudu ndani ya TANROADS ambayo hata tetesi tumezisikia.
Barabara zimejengwa kwa mamia ya kilometa nchini kote.
Bw. Mfugale alikuwa ni mtu makini sana.

RIP Boss!

"CAG nakutaka ukakague na huku tanroads na kwenye miradi ya ujenzi. Kote huku ambako siku zote kumekuwa hakukaguliwi." -- Alisikika mama Samia akitoa maelekezo.
 
Daraja la Kijazi.... Daraja la Mfugale.... huku sio kuchuriana? Wazee wa maeneo husika wamekasirika! Turudishe majina ya asili ya maeneo husika! Daraja la Tazara, Daraja la Ubungo, stendi ya Kuu ya Mabasi Mbezi Louis!
 
RIP Patrick Mfugale, Engineer aliyeboboea, mtu asiye na makuu, hakuwa na mdomo wa kubwabwaja kama ma CEO wengi.
Kwenye Elimu, sahihisha alienda Loughborough University of Technology, MidLands , Leicester UK.

Shukrani, na huu hapa wasifu uliosomwa na engineer Ninatubu Lema ambaye ni school mate wake engineer Mfungale katika ngazi mbalimbali za elimu. Wasifu huo ulisomwa wakati wa uzinduzi wa Mfungale Flyover bridge jijini Dar es Salaam mwaka 2018

Source : Azam TV
 
Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.

Injinia Patrick A. N. Mfugale RIP

=====

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.

Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi

Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.

Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.

Apumzike kwa Aman

Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo
  • Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
  • Ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
  • Ni mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi
Anasura ya Wizi wizi ..😂😂😂
 
Daraja la Kijazi.... Daraja la Mfugale.... huku sio kuchuriana? Wazee wa maeneo husika wamekasirika! Turudishe majina ya asili ya maeneo husika! Daraja la Tazara, Daraja la Ubungo, stendi ya Kuu ya Mabasi Mbezi Louis!
Na wamekasirika kwelikweli,lijitu la kuja toka bush halafu lonajimilikishwa stend na madaraja😂
 
Atakuwa ameondoka na hii phase 3, watanzania tujifunze kustaafu umri ukisogea, toka 77 upo kazini kweli jamani hakuna watanzania wengine? angekuwa ametulia na wajuu haya yasingetokea labda

Wee Babati acha lawama. Hakuna anayejua kesho.
 
Tunamshukuru Mungu kwa maisha yako, Mfugale

Hakika uliifanyia kitu Tanzania, na itakuenzi.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Patrick Aron Nipilima Mfugale mhandisi tajwa nchini Tanzania na alikuwa mtendaji mkuu wa Mamlaka ya barabara nchini Tanzania TANROADS.

Injinia Patrick A. N. Mfugale RIP

=====

Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Injinia Mfugale amefariki Jijini Dodoma.

Mfugale jana aliondoka na ndege akiwa na Katibu Mkuu ujenzi kuelekea Dodoma kwa safari ya Kikazi

Amezidiwa leo saa tano asubuhi na kukimbizwa Hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma, Tanzania ambapo ndipo Mauti umemfika muda mchache baada ya kufikishwa.

Tutaendekea kuwapasha kinachoendelea.

Apumzike kwa Aman

Wasifu:
Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Consalata Fathers Primary School mjini Iringa
-1975 Alimaliza elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi.
-1977-Mfugale aliajiriwa katika wizara ya ujenzi
-1983 alijipatia shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Rocky nchini India
-1991 Mfugale alisajiliwa kama muhandisi mtaalam.
-1992- Aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa barabara za mikoa.
-1994-1995-Alipokea shahada yake ya pili katika chuo kikuu cha Loughborough, nchini Uingereza
-2003-Alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment.
-Aliteuliwa kuwa muhandisi mkuu wa madaraja nchini Tanzania wakati huohuo na akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995 alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini.
-Alitengeza mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System
-2014- Alisajiliwa kuwa muhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa chama cha wahandisi Tanzania.
-Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja .
Alibuni daraja la Malagarasi lenye mita 178 kwa shilingi za Tanzania milioni 300.
-Baadhi ya madaraja aliyoweza kusimamia yakakamilika kujengwa ni:
  • Daraja la Mkapa Rufiji
  • Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Mozambique huko Ruvuma.
  • Daraja la Rusumo
  • Daraja la Kikwete huko Malagarasi.
  • Daraja la Nyerere huko Kigamboni
- Mfugale akiwa mtendaji mkuu wa Tanroads amesaidia ujenzi wa madaraja 1400 nchini Tanzania.
Amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takriban kilomita 36,258.
  • Ni Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa SGR inayoendelea kujengwa.
  • Ni mjumbe wa timu ya majadiliano ya miradi mikubwa ya umeme.
-2018 Alituzwa tuzo ya uhandisi ya Engineering Execellency

Picha: Daraja la Kikwete mto Malagarasi Daraja la Kikwete lililopo Mto Malagarasi
Asante Yesu, wewe unatoa uhai na kuuchukua.
 
Back
Top Bottom