TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

TANZIA Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Huyu alipandishwa sana chat na JK. Alipokuwa kwa JPM akazidi kumpandisha chati na inasemekana akamgeuka hata JK. Sasa undani wa kifo chake ukoje? Mbona ilikuwa ghafla vile! Ni corona kweli ile?
Hapa naona unataka kujenga hoja kuwa JK anahusika na kifo chake! Ushindwe na ulegee!
 
Mwili wa aliyekuwa mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), mhandisi Patrick Mfugale umewasili katika viwanja vya hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuagwa.

Viongozi mbalimbali wamewasili katikahospitali hiyo akiwemo naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya, katibu mkuu wa Wizara hiyo, Joseph Malongo, mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri na wabunge mbalimbali.

Pia wapo viongozi mbalimbali wa Tanroads, wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini pamoja ndugu, jamaa na marafiki.

Kwa mujibu wa ratiba mwili wa Mfugale utapelekwa Uwanja wa ndege wa Dodoma saa 10:00 jioni kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea jijini Dar es Salaam ambapo utaagwa tena katika ukumbi wa Karimjee kesho.

Mfugale alifariki dunia Jumanne Juni 29, 2021 saa 5 asubuhi katika hospitali ya Benjamin Mkapa.

PIA SOMA:
- TANZIA - Patrick Mfugale wa TANROADS afariki dunia Jijini Dodoma

Source: Mwananchi
RIP
 
Back
Top Bottom