Patrobas Katambi: Vijana waache kulalamika na kuchagua sana kazi

Sawa watufanyie unafuu kidogo ya reseni ya udereva.
Reseni kisheria ilikuwa 40,000 ila kuipata ilikuwa shughuli Sasa hivi wamepandisha ni 70,000 na bado kuipata lazma utumie zaidi ya 150,000
 
Wapinzani wanasemaje, mbona points za bure hizi?
 
Hapa anadanganya uma kuwa serikali inatoa ajira kwa wingi tatizo ni vijana wanachagua kazi!πŸ’πŸ’πŸ’
Your browser is not able to display this video.
 
Hizo ambazo zipo wazi baada ya kukosa kuchaguliwa na Vijana 'Wabaguzi wa kazi' ni zipi?, maana wapo wanaozitaka.
 
Katambi mwambie mama afanye yafuatayo kisha mje mtulaumu na sio kuropoka sababu mmeshiba.
Nyie ndio chanzo cha tatizo la ajira nchini kwa kukosa ubunifu.
Nawapa ubunifu kisha ropokeni tena vijana hawataki Kazi.
Ndani ya miaka 3 jinsi ya kuleta maendeleo na kumaliza tatizo la ajira nchini.

1.Ondoa futa kodi zote za kuingiza magari ya mizigo na abiria nchini kodi yake utaipata mara mbili yake kupitia indirect tax.Kwenye mafuta,leseni za udereva,fine za traffic, parking fee,ushuru wa stand,spare za magari,leseni na vibali mbalimbali.Gari moja uajiri si chini ya vijana 3.

2.Toa ruzuku kwenye viwanda vya kuzalisha matrekta wazalishe matreka mengi waje watuuzie wakulima kwa robo bei trekta moja uajiri zaidi ya watu wanne.

3.Jenga schemes za umwagaliaji KILA kijiji upitapo mto pande zote mbili watu walime mwaka mzima ni aibu sana kwa maji ya mito kumwaga maji yake baharini badala ya mashambani.Soko la mazao nje ya nchi lipo tele

4.Jenga vyuo vya ujuzi kila kata kopesha vijana ujuzi baada ya kumaliza darasa la saba wakapate ujuzi wautakao.

Kukopesha vijana waende chuo kikuu kisha warudi mtaani kuendesha bodaboda na kuwa machinga ni upotevu Mkubwa Sana wa kodi zetu na kuongeza idadi ya masikini nchini.

5.Fungua mipaka watu wauze watakapo nje ya nchi kuna masoko tele.Legeza masharti ya vibali Ili export ikue.

Ni sekta mbili tu zingine takataka hazifikii kilimo na madini kwa kuajiri vijana wote nchini na kuongeza pato la taifa bila kutegemea kukopa na kukamua kodi wananchi.

6.Peleka KILA kijiji mashine za kutengeneza interlocking block na vigae Ili watz wote wajenge nyumba bora kwa gharama nafuu kabisa

Mjerumani kwa miaka 15 alituletea maendeleo makubwa Sana ccm imeshindwa nini.
 
Vikwazo kibao tza Ili ufanikiwe msilaumu vijana ninyi mmefanya nn kuwafanya vijana wasimame.
Mfano TISS wa wenzetu wapo bize kuiba fursa za uchumi nje ya nchi kwa ajili ya vijana wao na sio kushiriki kuiba kura.
 
Kuna ukweli hapa. Vijana wengi siku hizi hawataki kazi za kipato cha chini. Kazi za kulipwa laki 1 au laki 2 hawazitaki, wako tayari kubaki bila kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…