Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

Hiki kitisho sio cha Tanzania Rais Samia Suluhu ameimarisha diplomasia kwa majirani zetu wote Tanzania kwa sasa hatuna adui
 
Kwani umesahau majeshi yaliyopo chini ya UN walivyovamiwa hivi karibuni, na jana/juzi tu Mai mai kachukua mapanga kupambana na M23?
Hayo unayoyasema ya akina M7, sasa yamefikia kikomo. Usitegemee tena hivi vikabila kuji-'impose' katika kuwawala wengine.
Israel?
EEeeeh! Mfano huo usiutumie kabisa katika maswala ya eneo hili. Rwanda hawezi kuwa Israel wa Mafrika Mashariki.
 
Mnampa sifa sana Kagame
Hapana, anastahili Sifa za kipekee kabisa,kwanza alikomesha mauaji ya raia wa Rwanda waliokuwa wanauliwa na Serikali yao pili ameituliza Rwanda tatu kawaunganisha Wanyarwanda nne kaenda kuwapiga Magaidi kwa siku chache tu na kuwatoa katika Miji ya Jimbo hilo la Msumbiji kaskazini.
 
Ni bora Joseph Kabila arudi kuiongoza Kongo huyu Tishekedi Nchi imemshinda.
 
Katika speech ya Kagame amegusia point moja ya maana sana kasema "Amani ikipatikana Mashariki ya Kongo, Rwanda na Kongo zitafaidika kibiashara".

Angalia Vision ya Kagame halafu Muangalie Tishekedi Vision yake ni kuuchochea huu mgogoro ili azidi kubaki Madarakani acheleweshe Uchaguzi kwa kusema DRC iko Vitani na Rwanda.

Tishekedi ni Zero IQ bora haya Fally Ipupa angepewa hiyo Nchi.
 
Bila shaka unamaanisha udhaifu wa kijeshi, Congo ni nchi kubwa, yenye rasilimali nyingi, lakini bahati mbaya isiyo na uwezo wa kujilinda, ndio maana huyu Kagame anautumia huo udhaifu.

Kagame anachofanya kwa hizi kauli zake, ni kucheza na akili za watu, hasa kuwatisha wale waliokwenda kukisambaratisha kikundi chake cha wahuni, anashindwa kutoa kauli za moja kwa moja kwa kuogopa ataonekana yeye ndie mfadhili wao, sasa anachofanya ni kuwatisha wale wanaowapiga kwamba kombora lao lisitue Rwanda, huku ni kuwalinda waasi wa M23 kijanja.
 
Muoga sana huyu. Kila msimu ana vitisho na hatujawahi kuona akimsumbua mtu. Mission zake na operation zake zimekuwa zikifeli hadi kule DRC dhaifu.
Kauli nzuri aliotoa ni ile kwamba amani ni bora kuliko vita, kwamba yeye anafahamu vita sio kitu kizuri.
 
Well explained.
 
Aaaah, nawe una lako jambo. Huishi kushangaza!
 
Kwahiyo tuseme Kiswahili ni lugha muhimu Afrika kuliko hata kingereza ,maana hata rais wa Rwanda ameamua kutumia Kiswahili kwenye issue nzito na muhimu ya usalama wa nchi yake.
 
Kamba ya Kagame imefika mwisho, hana njia tena ya kujifanya yeye anamadaraka yoyote ya kufanya maamuzi ya nchi jirani.

Wakongo safari hii wakimpa mwanya tena wa kuendelea kuwasumbua wajilaumu wenyewe.
 
Kunguni ya mama ipo kazini.
Endeleeni kumpamba tu ila ukweli ata nyie mnauona. Tumekuwa madaraja kwa watawala wanafanya tu kila wanachojisikia ata kama kinaliumiza Taifa.
Ipo siku mwenyezi Mungu atawapigia wale wasio na nguvu ya kutenda.
huo muda wa kumsikiliza kagame umeupata wap? ......Umbeya tu kwenye nchi zawatu
 
Ukisoma comments hapa utaelewa kweli jiwe limetupwa gizani, na wanaenjoy tunavyo onyesha hofu zetu, na kuthibitisha kuwa PK anatisha.
Amtishe Nani?Sisi Tanzania tuna uwezo wa kuifanya hiyo nchi sehemu ya mkoa wetu kwa muda mfupi.nchi hiyo masikini.
 
Wanamwacha massawe, wanaenda Kwa mwesiga
 
Hivi yule jamaa wa mabakamabaka mwenye asili ya Tall aliyechomoka na kompyuta mpakato yenye mabaka alipatakina? Hata hvyo kuna wenye mabakamabaka wenye asili ya Tall kadhaa tunajumuika nao halafu hatushituki. Tall anaweza kuwa na info nyingi sana za wananchi wa uswahilini kuliko tunavyodhani. Uswahilini tumejiachia sna hadi kwenye sehemu nyeti. Tall huwa yupo smart sana kwenye data/info na anajua azitumie vp. Hivyo usije ukashangaa Argentina kufungwa Saudi Arabia.
 

Bahati nzuri mibongo ni VIAZI waioumbiwa kusahau.
 
Chonde wadau tusishabikie sanaa hili swala bali tumuombe Mwenyezi Mungu aingilie kati, DRC ameharibu sanaa kwanza aliaza kutuhumu mashirika yakimataifa kwamba yanachochea vita na uvunjifu wa amani DRC,Pili akamfukuza balozi wa Rwanda harshly wakati EAC ipo ndo mahali pakusemea, Tatu akaituhumu serikali ya Rwanda directly kuwa wanajihusisha na M23,wazungu wanaweza kuwa nyuma ya Rwanda maana na wao walituhumiwa pia kupitia mashirika yao ya UN(vita sio ukubwa wa nchi vita ya sasa ni technology) Tusali na kuswali tuombe Mungu atuepushe na hili pepo Viongozi wetu wajazwe hekima na busara aminaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…