Paul Kagame katoa onyo kwa Kiswahili, walengwa mmepata ujumbe?

. Binafsi naamini, haivuki miaka miwili (2) kuna mtu kwenye huu ukanda wetu wa maziwa makuu atatoa kilio kikubwa sana
Wacha Bhwanah!
Umezungukaweeee, kidogo nijiondokee zangu!

Hakuna kitu hapo mkuu, asipoangalia huu ndio utakuwa mwisho wa Bwana Fito. M23 ni jiwe litakalomwangamiza.

Lakini kinachonifurahisha ni kuona unafiki/utapeli wa baadhi ya mataifa ya ukanda huu wa kujitwisha mzigo kwa jina la Jumuia, halafu wanafanya ghelesha kupeleka jeshi huko eti kulinda maslahi yao (ya nchi yao) kwa mgongo wa Jumuia.

Haya, jeshi linafika eneo la mapambano, hapo hapo hadithi inabadilika, eti wao wamekuja kulinda amani na siyo kuimarisha amani! M23 anawaangalia tu na kucheka.

Nisitoe hadithi ndefu, lakini sasa ni wazi, waCongo wenyewe sasa wameamua, hawataki kuchezewa na hivi vikaragosi na vinyago.

Kinachonipa moyo kwa upande wetu, ni kutofuata mkumbo wa hao wanaotumia jina la Jumuia kujiingiza na kutumika kama 'tissue' bila ya kujitambua.
Lakini ifahamike, tukiona maslahi yetu yanachezewa, tusisite kuyalinda.
 
..Kagame anawatishia KENYA ambao wamepeleka jeshi lao kupambana na waasi wa M-23.
Hakuna kitu hapo mkuu 'Joka'. Usihadaiwe na utapeli wa hao jamaa, hasa huyo msuluhishi.

Walipiga kelele nyingi za vitisho vya kwenda kuwamaliza vikundi vinavyofanya fujo. Jeshi linafika huko kwenye mapambano hadithi za pembeni zinaanza, badala ya kufanya kweli kama walivyokuwa wakipiga kelele hapo kabla.
Na inaonekana huu mchezo hujausoma vizuri: Kenya anamkingia kifua Kagame kiaina. Wewe soma vizuri kelele nyingi zinazotoka huko utauelewa mchezo wanaocheza.

Sasa Mkongo mwenyewe kaamua kufanya kazi, na nina hakika ataifanya na kuimaliza ipasavyo.
 
Kuwa dhaifu kuwashinda wadhaifu wengine wakati una nguvu zaidi yao unawezaje kujisifia..labda km huelewi dhana ninayoisema, muhimu sio kushinda wengine, muhimu ni hicho ulichopata kulinganisha na unachostahili kupata..
Wamekuwa dhaifu Tena si unawaona wa maana wewe au? Huna msimamo na hata huelewi unachosimamia.
 
Hujamuelewa naona katumia Kiswahili ili kuongea na wakongomani wa kunako uwanja wa mapambano maana wanazungumza Kiswahili cha ‘kwa fasi ya’
 
Tanzania kuviacha vinchi vidogo vidogo vinashambulia mshirika wetu kibiashara inaonyesha ni jinsi gani tusivyoijua safari yetu.

Nilimwelewa sana Mkwere alipoenda kuwapiga M23
 
Uwepo wa vurugu Congo ni aibu kwa majirani zake....huwezi kusema haikuhusu.
Huu ni ukweli mtupu, Mkwere alipopeleka jeshi DRC hawa wahuni walisambaratika wakabaki kubwatukia vyumbani mwao.

Kama DRC ameshakuwa mwanachama wa EAC nchi wanachama angalau basi zionyeshe kupambana na hali anayoipitia mwanachama mwenzao.

DRC ni soko kubwa sana kwa Tz.
 
Kwanini mwanajumuia mkubwa kuliko wote amekaa kimya ?
 
..Kagame anawatishia KENYA ambao wamepeleka jeshi lao kupambana na waasi wa M-23.

You are my hero.
Quote Tweet
Muhoozi Kainerugaba
@mkainerugaba
·
Nov 6
As for M23, I think it is very, very dangerous for anybody to fight those brothers of ours. They are NOT terrorists! They are fighting for the rights of Tutsi in DRC.


Je wajua kwa nini Kagame na Museven hawatoki madarakani? Wajua kwa nini wanapigana kule DRC? The answer is said by Museven son!!
 
Kuna tofauti gani kati ya means na methods
 
Uko sahihi hatuna vijana wenye hoja siku hizi wamebaki kusifia tu. Nchi haina development plan kila siku ni kusifia asante raisi kwa kutuletea blah blah.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…