Uchaguzi 2020 Paul Makonda achukua fomu ya Ubunge Kigamboni, kupitia CCM

Mwaka 1995 pale Temeke tulipiga kura na kumchagua msambaa mmoja anaitwa Kihiyo, kumbe jamaa alikua amefoji cheti tena cha VETA, wapinzani walipokwenda mahakamani jamaa akapigwa uchaguzi ukarudiwa 1996 ambapo Augustino Lyatonga Mrema wakati huo akiwa NCCR-MAGEUZI akagombea na kushinda, Temeke tukawa na mbunge lakini anaishi Masaki
 
Wewe mikedean vipi!? Viongozi wote katika Serikali ni WANACHAMA NA MAKADA WA CHAMA TAWALA, CCM, kwa mantiki hiyo basi ni "KUONESHA KUWA UNAENDA KUJIHUSISHA NA CHAMA FULANI CHA SIASA"; hayo kwenye mabano ni maneno yako! Kwa mantiki hiyo basi waachie kazi na madaraka yao! Hawa ni makada na ni watumishi wa umma wanaweza kutia nia wakati wakiwa kazini na watahudumia ofisi zao hadi hatua ya UTEUZI WA CCM na hatimaye NEC! Huo ndio ukweli na utaratibu HASA HASA kwenye nafasi za KUTEULIWA. Kwa WAAJIRIWA , utaratibu ndio huo unaosema wewe. Kumbuka kuna political appointments as opposed to employments.
 
Huo waraka unawahusu watumishi wanyonge,watumishi dizaini ya Makonda,Mnyeti huo waraka kwao ni kama kijarida tu kama cha gazeti la Shigongo.
Huo Waraka unawahusu employees wa kawaida na SIYO POLITICAL APPOINTEES jamani mbona mnataka kulazimisha mambo. Hebu nendeni mkausome sawasawa na kujua ukweli wa mambo yalivyo.
 
Soon mtaona Barua kutoka ikulu mawasiliano. Lazima watakuwa replaced.
 
Hatujasikia akifanyiwa replacement, na Mnyeti pia kachukua form hatusikii replacement yao.

Wengine wakigusa tu unasikia wametumbuliwa.

Mshikaji kwa double standard hajambo.

Mnyeti na Makonda ni wasukuma.

Sisi wasukuma taifa kubwa tulieni hivyo hivyo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Dah hapa ndo jiwe hua anajichanganya. Mbona wengine wote walilazimika kujiuzulu nyadhifa nyingine ili wagombee ubunge huyu imekuaje? Naanza kushawishika kuna jambo la ziada nyuma ya uswahiba wa hawa watu wawili
 
Daudi Bashite Niko tiyari kufa ila ubunge atumpi kilaza mpaka atuonyeshe vyeti
[emoji3][emoji3][emoji3] mkuu huyo atapitishwa tu, tena na unaibu waziri atapewa..just wait and see
 
Watanzania wote tupinge kwa nguvu zetu zote huu Ukabila la sivyo itakuwa kama Kenya...itikadi pembeni tupingeni Ukabila
 
Magufuli hizi double standards iko siku utalipa gharama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…