RC MAKONDA ACHUKUWA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KIGAMBONI.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 15 amechukuwa Fomu ya kuomba ridhaa ya Kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi CCM.
Jimbo hilo lilikuwa chini ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile
USHAURI WA BURE KWA WAGOMBEA UBUNGE-2020
Kwanza nichukue nafasi kuwapongeza wote waliojitokeza kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali hususani Boazi Mwakasaka mtia nia jimbo la ubungo kupitia SAU- Sauti ya Umma, Mh Paul Makonda jimbo la Kigamboni kupitia CCM, Mchungaji Josephat Gwajima jimbo la Kawe kupitia CCM, Mh Boniphace Jacob jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA. Orodha ni ndefu.
Kugombea Ubunge si dhambi bali ni haki ya kikatiba kwa mtanzania yoyote anayekidhi vigezo kwa mujibu wa katiba Jamhuri ya Tanzania kuwania nafasi hizo kwa lengo la kuwawakilisha wananchi na kuleta maendeleo.
Wagombea wote wasiwe na hofu bali waelewe kuwa ushindani wa mwaka huu ni mkubwa sana kuwahi kutokea tangu taifa hili liasisiwe hii ni kutokana na kuongezeka kwa uelewa Mwamko na tekinolojia za upashanaji habari.
USHAURI WA KWANZA: SERA
Wagombea wanatakiwa kutengeneza sera makini za kiuchumi na kijamii na kimaendeleo, zinazotekelezeka na zinazopatana na akili za wapiga kura.
ikumbukwe kwamba utengezaji wa sera ni suala la kitaalamu, hivyo ni muhimu sana kwa wagombea kuhakikisha wanawashirikisha wataalamu wa masuala ya kiuuchumi, kisiasa, kijamii na kimaendeleo ili waweze kutengeneza sera zinokubalika katika masikio na mioyo ya wapiga kura pasipo shaka yoyote.
USHAURI WA PILI: MBINU NA MIKAKATI
Wagombea wanapaswa kutengeneza mbinu na mikakati kabambe sana ya kuhakikisha sera zao zinawafikia walengwa kwa wakati na zinaeleweka vizuri. Wagombea wanapaswa kutumia mbinu za kisasa na tekinolojia ya hali ya juu sana kuhakikisha wanfikisha ujumbe kwa wapiga kura. Wapiga kura wakielew sera zako basi ujue wewe hakuna kitu cha kukuzuia kuingia bungeni au mjengoni kama wasemavyo vijana wengi.
Kuna njia mbalimbali zinazoweza kutumiwa na wagombea katika kunadi sera zao kwa wapiga kura;
1. Kampeni shirikishi (interactive Compaigns)
2.Kampeni za wazi (public compaigns)
3.Machapisho-Printed media
4. Kampeni za kidigitali nje ya mtandao-TV, redio, simu, flash, CD, Memory Cards nk
5. Kampeni za kidigitali ndani ya mtandao-Google search, Google compaigns, facebook compaigns, instagram broadcasting, Youtube Ranking, Whatsapp compaigns, email compaigns na nyingine nyingi.
Ni muhimu wagombea wakashirikisha wataalamu wa mawasiliano hususani mawasiliano ya kidigitali katika kuhakikisha kuwa wanawafikia watu sahihi na wengi zaidi na kwa muda uliopangwa
USHAURI WA TATU: USHAWISHI
Jambo la mwisho ni ushawishi
Unaweza kuwa na sera nzuri, mbinu na mikakati mizuri ya kufikisha sera kwa wananchi lakini iwapo hutakuwa na ushawishi basi hutaweza kupenya katika kinyanganyiro cha mwaka huu. Ushawishi ni suala la kisaikolojia hivyo ni vema wagombea watumia watalamu wabobevu wa saikolojia kupenyesha ujumbe ndani ya miyo ya wapiga kura.
MWISHO
NInawatakia afya njema wagombea na wapiga kura wote. Tukutane mjengoni baada ya octoba 2020