Uchaguzi 2020 Paul Makonda achukua fomu ya Ubunge Kigamboni, kupitia CCM

Uchaguzi 2020 Paul Makonda achukua fomu ya Ubunge Kigamboni, kupitia CCM

Issue ya cheti ni simple coz anaweza kujaza sehemu hiyo ya Elimu kuwa anajua Kusoma na kuandika. Au Cheti cha darasa la 7.. coz ubunge sifa no.1 ni kujua kusoma na kuandika.
Kwa kupenda sifa,lazima ajaze elimu yake ya chuo kikuu Ushirika. Sasa hapo ndo patamu. Maana itabidi athibitishe alifikaje huko. Ila idea yako akiifuata basi ndo itakuwa pona yake.
 
Kwa mtazamo wangu juu ya suala hili la Makonda Paul kuchukua fomu ya kugombea Ubunge katika jimbo la kigamboni ni kwamba yawezekana kabisa Mzee Mkulu alishapanga kutengua uteuzi wake mapema hivyo ili kumfichia hilo kwa mtoto mpendwa ni ikaonekana ni bora akachukue fomu katika jimbo ambalo Ndugulile ndye Gavana.

Mwisho wa siku Makonda atakatwa na atapitishwa Ndugulile hivyo itaonekana Makonda alitenguliwa kwasababu ya kwenda kugombea na sio Makandokando yake.


AKILI KUBWA SANA HII
Any thing is possible in politics. Asubiri uteuzi mwingine baada ya uchaguzi.
 
Makonda kajipeleka kwenye moto. Akishinda ubunge yatamkuta ya Kihiyo. Sasa itabidi atoe cheti chake cha form four.
Lakini ili uwe mbunge kipindi hiki huhitaji kuwa na cheti chochote. Ili mradi ujue kusona na kuandika kiswahili... INATOSHA SANA
 
Kwa kupenda sifa,lazima ajaze elimu yake ya chuo kikuu Ushirika. Sasa hapo ndo patamu. Maana itabidi athibitishe alifikaje huko. Ila idea yako akiifuata basi ndo itakuwa pona yake.
Bashite muhuni sana sidhan kama atashindwa ng'amua kitu kidogo hivyo.. pia mwenye vyeti vyake hali Gwajima now wako Chama moja anaweza kuzikana hizo nyaraka.
 
Bashite muhuni sana sidhan kama atashindwa ng'amua kitu kidogo hivyo.. pia mwenye vyeti vyake hali Gwajima now wako Chama moja anaweza kuzikana hizo nyaraka.
Tatizo sio kukana. Atatakiwa awasilishe vyeti vyake. Hapo ndo itakuwa balaa atakapowasilisha cheti cha form four kisicho chake.
 
Issue ya cheti ni simple coz anaweza kujaza sehemu hiyo ya Elimu kuwa anajua Kusoma na kuandika. Au Cheti cha darasa la 7.. coz ubunge sifa no.1 ni kujua kusoma na kuandika.
Suala la cheti ni zito sana kutokana na Mkulu alivyo chukulia kwa wengine. Lakini uzuri wa Makonda katika kila cheti chake amekaa darasani na kufaulu. Kuna picha tunapewa kuwa hakuingia darasani, picha hii sio kweli.

Ndio maana amekuwa kiongozi wa vyuo ambavyo amepitia. Na tukumbuke amekuwa Rais nwa vyuo vyote vikuu vya Tanzania. Yeye na Mwigulu hakuna tofauti.
 
Sawa ila ukijaza data za uongo,imekula kwako. Kwenye Elimu aache wazi. Na aandike anajua kusoma na kuandika basi.
Kwan amekwambia atajaza data za uongo? Hebu mwambie akutumie usafiri uende masaki kumsaidia kujaza form bi kigagula[emoji2][emoji2]
 
Duuh, ni wewe pekee umefanikiwa kupost hii kitu, hongera mkuu, utakua jiniaz balaa.
Yaani JF ukitaja Makonda na Kigamboni Posta inadakwa juu kwa JUU siju Makonda kato Kiasi gani.Binafsi ningepata Milioni 3 tu ningetia kambi pale Kigamboni ni hakikishe nachukua jimbo
 
Tatizo sio kukana. Atatakiwa awasilishe vyeti vyake. Hapo ndo itakuwa balaa atakapowasilisha cheti cha form four kisicho chake.

Na kwanini apeleke cheti ambacho sio chake?

Unafikir yeye ni mjinga wa kiasi hicho.
 
RC MAKONDA ACHUKUWA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KIGAMBONI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Julai 15 amechukuwa Fomu ya kuomba ridhaa ya Kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya Chama cha mapinduzi CCM.

Jimbo hilo lilikuwa chini ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile

USHAURI WA BURE KWA WAGOMBEA UBUNGE-2020

Kwanza nichukue nafasi kuwapongeza wote waliojitokeza kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali hususani Boazi Mwakasaka mtia nia jimbo la ubungo kupitia SAU- Sauti ya Umma, Mh Paul Makonda jimbo la Kigamboni kupitia CCM, Mchungaji Josephat Gwajima jimbo la Kawe kupitia CCM, Mh Boniphace Jacob jimbo la Ubungo kupitia CHADEMA. Orodha ni ndefu.

Kugombea Ubunge si dhambi bali ni haki ya kikatiba kwa mtanzania yoyote anayekidhi vigezo kwa mujibu wa katiba Jamhuri ya Tanzania kuwania nafasi hizo kwa lengo la kuwawakilisha wananchi na kuleta maendeleo.

Wagombea wote wasiwe na hofu bali waelewe kuwa ushindani wa mwaka huu ni mkubwa sana kuwahi kutokea tangu taifa hili liasisiwe hii ni kutokana na kuongezeka kwa uelewa Mwamko na tekinolojia za upashanaji habari.

USHAURI WA KWANZA: SERA

Wagombea wanatakiwa kutengeneza sera makini za kiuchumi na kijamii na kimaendeleo, zinazotekelezeka na zinazopatana na akili za wapiga kura.
ikumbukwe kwamba utengezaji wa sera ni suala la kitaalamu, hivyo ni muhimu sana kwa wagombea kuhakikisha wanawashirikisha wataalamu wa masuala ya kiuuchumi, kisiasa, kijamii na kimaendeleo ili waweze kutengeneza sera zinokubalika katika masikio na mioyo ya wapiga kura pasipo shaka yoyote.

USHAURI WA PILI: MBINU NA MIKAKATI

Wagombea wanapaswa kutengeneza mbinu na mikakati kabambe sana ya kuhakikisha sera zao zinawafikia walengwa kwa wakati na zinaeleweka vizuri. Wagombea wanapaswa kutumia mbinu za kisasa na tekinolojia ya hali ya juu sana kuhakikisha wanfikisha ujumbe kwa wapiga kura. Wapiga kura wakielew sera zako basi ujue wewe hakuna kitu cha kukuzuia kuingia bungeni au mjengoni kama wasemavyo vijana wengi.

Kuna njia mbalimbali zinazoweza kutumiwa na wagombea katika kunadi sera zao kwa wapiga kura;
1. Kampeni shirikishi (interactive Compaigns)
2.Kampeni za wazi (public compaigns)
3.Machapisho-Printed media
4. Kampeni za kidigitali nje ya mtandao-TV, redio, simu, flash, CD, Memory Cards nk
5. Kampeni za kidigitali ndani ya mtandao-Google search, Google compaigns, facebook compaigns, instagram broadcasting, Youtube Ranking, Whatsapp compaigns, email compaigns na nyingine nyingi.
Ni muhimu wagombea wakashirikisha wataalamu wa mawasiliano hususani mawasiliano ya kidigitali katika kuhakikisha kuwa wanawafikia watu sahihi na wengi zaidi na kwa muda uliopangwa

USHAURI WA TATU: USHAWISHI

Jambo la mwisho ni ushawishi
Unaweza kuwa na sera nzuri, mbinu na mikakati mizuri ya kufikisha sera kwa wananchi lakini iwapo hutakuwa na ushawishi basi hutaweza kupenya katika kinyanganyiro cha mwaka huu. Ushawishi ni suala la kisaikolojia hivyo ni vema wagombea watumia watalamu wabobevu wa saikolojia kupenyesha ujumbe ndani ya miyo ya wapiga kura.

MWISHO

NInawatakia afya njema wagombea na wapiga kura wote. Tukutane mjengoni baada ya octoba 2020
 
Back
Top Bottom