Paul Makonda aipasua CCM, kigogo ndani ya chama atishia kujiuzulu

Paul Makonda aipasua CCM, kigogo ndani ya chama atishia kujiuzulu

View attachment 2793650
SASA ni rasmi kuwa CCM inaingia na iko kwenye mpasuko mkubwa sana baada ya habari za kuaminiki kutoka kwa watu wa karibu sana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana kuwa anajipanga kujiuzulu umakamu mwenyekiti wa chama hicho kikongwe na king'ang'anizi kutoka madarakani.

Kinana ameweka wazi kuwa anapinga uteuzi wa Paul Makonda kama Katibu Mwenezi wa CCM na pia ameweka wazi kwa watu wake wa karibu kuwa hakushirikishwa na kushauriana kabla ya uteuzi wa Makonda kitu ambacho amekitafsiri kuwa anadharauliwa na hayuko tayari kuburuzwa kwenye mambo ndani ya chama na hataki kuwa sehemu ya historia ya hovyo ndani ya chama hicho kumsafisha Paul Makonda ambaye ana uchafu mwingi sana aliofanya akiwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam.

Mtu huyu aliyetupa habari hizi za ndani ndani sana ambaye ni mmoja wa wale wanaofahamika kuwa vijana wa Kinana tena wa karibu sana, amesema tayari Kinana ameomba apointimenti ya kukutana na Mwenyekiti wa CCM kumueleza azma yake hiyo na amesikika kuwa atafanya kwa staili ile ile ya kipindi cha Magufulu alipojiuzulu kupinga ubabe na ukatili wa Magufuli.

Wakati hali ndani ya CCM ikiwa mbaya kiasi hiki tayari kumekuwa na mgawanyiko mkubwa sana ndani ya chama hicho na wazee wa chama na makada wanafikiria kufanya yasiyotarajiwa kwenye uchaguzi wa 2025 na zaidi wamefika mahali kuanza kuunda kambi za kumkwamisha Rais Samia kuwa mgombea mwaka 2025 na bahati mbaya sana kambi ya ya akina JK ile ile ya mwaka 2005 inasemekana imeshaingia kazini na wameweka wazi kuwa hawawezi kuona chama kinachezewa na akina Makonda kwa kiasi hiki na wanapinga kwa nguvu zote maamuzi ya Makonda kuwa Katibu Mwenezi wa CCM.

Mgawanyiko huu umekwanda mbali zaidi na tayari kundi hili la makada wanaanza kushawishi baadhi ya wastaafu wa vyombo vya usalama kuwa sehemu ya mpango huu ili kufanikisha azma yao hiyo ifikapo 2025. Kama jambo hili ni kweli kama tulivyoambiwa basi tunaweza kushuhudia kupasuka na kuzama kwa CCM kwa staili ya KANU kule Kenya na UNIP kule Zambia miaka mingi nyuma. Vyama hivi vilikuwa na nguvu sana toka uhuru wa nchi zao lakini zilikuja kuzama na kufa kimzahamzaha tu na mpaka leo havijanyanyuka tena.

SISI YETU NI MACHO NA TUTAWALETEA TAARIFA KADRI TUNAVYOAMBIWA NA KUZIPATA.. LAKINI KWA SASA TUMEKAAA PALEEEE [emoji1542]

#KigogoMediaUpdates
Yeye Kinana ana usafi gani;kwani aliacha Biashara ya kutorosha Madini ya Tanzanite na kuua Tembo wetu!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Makonda ataipasua CHADEMA. Ujio wa Makonda umefanya Mbowe na wahuni wenzake wafute mikutano yao ya unafiki. Mabeberu waliokuwa wanawapa pesa kupinga mkataba wa bandari wameacha baada ya mkataba kusainiwa. Mbowe na genge lake wamebaki kuhaya haya tu
Bila kumtaja Mbowe huwezi lala.
Jitahidi umzalie Katoto kamoja tu uwe naye karibu zaidi nafsi yako itulie tulii.
 
Rais Samia amechanganyikiwa kwenye hili. Repercussions zake ni mbaya sana. Kuna methali inasema "adui mwombee njaa"

Hapa naona maadui wa Samia wamefanikiwa kumuombea NJAA. Makonda hakufaa kurudi kwenye utumishi wa chama wala Serikali bali alipaswa kuwa gerezani tu. Hii ni DHIHAKA kubwa kwa Watanzania

Ila iko siku Paul Makonda ataingia tu gerezani na kutumikia kifungo kwa maovu yake
Makonda ndiye Makamu wa Mwenyekiti wa CCM ajaye kabla ya 2025 kufika. Na ndiye Waziri Mkuu 2025-2030.
 
Back
Top Bottom