Paul Makonda akutana na Viongozi wa madhehebu na Taasisi za dini, asema anayoyafanya Rais Magufuli yanazidi maelekezo ya ilani ya CCM

Huyu anatakiwa apumzike kama mstaafu lakini ukada inamfanya aingilie majukumu.ambayp sio ya kwake. Yeye sio kiongozi tenaila tunamsamehe huenda kichwa chake hakiko vuzuri
 
hehe hii imenikumbusha kesi ya vijana songea boys waliopasua vioo vya daladala.
walikamatwa na walifikishwa mahakamani, ile kesi ndio nilijua mahakama haitoi haki ila mshindi wa hoja.[emoji23][emoji23][emoji23]

konda wa daladala, aliulizwa lakini akizugwa kwa lugha ya ishala(mikono).
Aliulizwa nilirusha jiwe nikiwa umbali wa kilomita moja(akinyosha mkono mmoja) au mbili ( akinyosha mikono yote kuelekea kulia na kushoto)

konda, akifikiria, akajibu ulirusha jiwe umbali wa kilomita 7[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Musa Salum amewataka viongozi wa dini kutoa azimio la kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo

Hayo ameyaeleza wakati wa mkutano uliowakutanisha viongozi wa dini kwa ajili kuwaeleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeo tangu Rais Magufuli aingie madarakani.
 
Kukutana na viongozi lazima iwe live! Awamu hii kutafuta sifa za kijinga kumezidi. Unakutana na watu live, wamekuwa bidhaa unataka kuzitangaza?

Hakuna mjadala wowote wa maana huwa unafanyika live.
Ukiwaambia onyesheni Bunge LIVE hawataki wananchi waone madudu yao,
 
So baada ya kupotezewa kupewa mkono katafta kiki ili akioneshe kuwa anamsifia mkuu. Sasa 2020 mambo yatabadilika. Watakaopewa shavu ni wale watakaokuwa wakimyooshea kidole na kumwambia ukweli.

Magufuli kashawavutukia wasaka tonge. Hawana maslai na nchi wao wanajipendekeza ili wale.
 
Viongozi wa dini makanjanja, wanadhani watasaidia kuhamasisha uchaguzi feki. Ili kuondoa aibu ya kukosa wapiga kura
 
Enyi viongozi wa dini mjue sisi sio kondoo tena kama mnavyodhani! dawa yenu ni kuacha kuwapa sadaka tuone kama mtaendelea kujimwambafy!

Natamani waumini wenu wajitambue siku moja wagome kutoa sadaka, kwani naona mnajisahau mnaanza kutugeuka.
Nashangaa makanisa mengi wachungaji ni matajiri wakati waumini wao ni masikini wa kutupwa, mpaka wanajimwambafy kuwa wanapesa kuliko serikali.

Kuna wachungaji wengine hata kujenga kanisa hawawezi huku wengine wanamiliki hadi helicopter magari ya kifahari huku wanaendelea kufyonza waumini ambao wengine wanatembelea kandambili za gesti za mguu mmoja.

Ole wenu nyie wachungaji wanafiki, tutakutana jehanam kwenye ziwa la moto

Kwa matendo yenu ya kinafiki, itakuwa muujiza mchungaji mnafiki kuuona ufalme wa mbinguni!
Serikali hii mnayoiabudu na kuisujudia imekengeuka wala haina utukufu wa Mungu.

Haki za binadamu zinakikwa, watu wanapotea mili ya watu inaokotwa inaelea majini, viongozi wa dini mpo tu mnaendelea kuwakamua waumini sadaka zao zinazopatikana kwa shida!..
Kuanzia leo sitaenda tena kanisani, kwani najua kufa ni lazima.
 
Daaah!
Nimejifunza nikipata mkate cha kwanza kuwaona ni family yangu ya watu wangu wa karibu.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1] Kwahiyo 2020 upinzani hamna mpango wa kushinda kabisa?
 
Kesho kutwa machinjio ya kisasa ya nguruwe yakitangazwa kujengwa Dar, waislamu tutataka viongozi wetu wa BAKWATA watangaze pia kuunga mkono.
Dhamira ni kuunga mkono kila kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…