Enyi viongozi wa dini mjue sisi sio kondoo tena kama mnavyodhani! dawa yenu ni kuacha kuwapa sadaka tuone kama mtaendelea kujimwambafy!
Natamani waumini wenu wajitambue siku moja wagome kutoa sadaka, kwani naona mnajisahau mnaanza kutugeuka.
Nashangaa makanisa mengi wachungaji ni matajiri wakati waumini wao ni masikini wa kutupwa, mpaka wanajimwambafy kuwa wanapesa kuliko serikali.
Kuna wachungaji wengine hata kujenga kanisa hawawezi huku wengine wanamiliki hadi helicopter magari ya kifahari huku wanaendelea kufyonza waumini ambao wengine wanatembelea kandambili za gesti za mguu mmoja.
Ole wenu nyie wachungaji wanafiki, tutakutana jehanam kwenye ziwa la moto
Kwa matendo yenu ya kinafiki, itakuwa muujiza mchungaji mnafiki kuuona ufalme wa mbinguni!
Serikali hii mnayoiabudu na kuisujudia imekengeuka wala haina utukufu wa Mungu.
Haki za binadamu zinakikwa, watu wanapotea mili ya watu inaokotwa inaelea majini, viongozi wa dini mpo tu mnaendelea kuwakamua waumini sadaka zao zinazopatikana kwa shida!..
Kuanzia leo sitaenda tena kanisani, kwani najua kufa ni lazima.