Kiukweli hakuna Rais aliyewahi kufanya mambo makubwa hivi katika kipindi kifupi. Yawezekana wapo walioumizwa katika kuyafikia haya but kiukweli mambo mengi yaliyolalamikiwa rais huyu ameweza kuyarekebisha,kumi bora kwangu no;.
1. Afya - vituo vya afya 300+ na hospitality kadhaa,bima ya afya kwa kilamtu nk.
2. Elimu - elimu bure na kukarabati shule kongwe,mikopo vyuoni kutoleta tashwishwi kubwa nk
3. Mawasiliano - makampuni yanalipa kodi inavyostahili,airtel wanatoa gawio,rada Kadhaa nk.
4. Uchukuzi - Reli zinajengwa na kufufuliwa,ndege na viwanja vyake vinajengwa na kupanuliwa,madaraja,vivuko,meli,barabara zinajengwa,flyover nk
5. Maji na umeme vinasimamiwa kikamilifu na kusambazwa vyema.
6. Biashara ndogondogo bila karaa na biashara kubwa kodi stahili inalipwa hamna janjajanja.
7. Mwananchi wa kawaida anasikilizwa,anasaidiwa na watumishi wa umma wanawajibika kwa wananchi ipasavyo.
8. Wizi,urasimu na ubadhilifu umedhibitiwa kwa kiwango kikubwa.
9. Uwiano wa maendeleo,kwasasa nchi inajengwa bila ubaguzi hakuna sehemu inapendelewa na nyingine kuachwa.
10. Rais amekalia kiti vyema,ofisi inaheshimiwa hata na mataifa tapeli,anashiriki nyumba za ibada,mkewe hafanyi biashara za ujanja ujanja Bali anatulia kumsapoti mumewe.
Hatuna mgombea angeyeweza kufanya haya tuache ushabiki wa kijinga,kwenye ukweli tuweke mbele ukweli