Pre GE2025 Paul Makonda ameagiza Waziri wa TAMISEMI kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Pangani Haraka Sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nenda mahakamani kama una malalamiko.
MahakamaCCM??

Ngoja nikukumbushe tu huyu alikua ni jaji mkuu wa Tanzania Marehemu Augustino Ramadhani hapo ni akichukua fomu ya kugombea urais kupitia CCM 2015!

Sasa kama jaji mkuu ni kada wa CCM kuna uhuru wa mahakama chawa/kiroboto wa Samia?

THINK THINK THINK!!!
 
Kwani ninyi CHADEMA si huwa ni kwenye mahakama hizo hizo ambazo hushinda kesi?

Tatizo lenu ninyi ni kuwa mahakama inakuwa huru pale tu mnaposhinda kesi zenu.lakini mkishindwa kesi mnaanza vimaneno maneno tu
 
Kwani ninyi CHADEMA si huwa ni kwenye mahakama hizo hizo ambazo hushinda kesi?

Tatizo lenu ninyi ni kuwa mahakama inakuwa huru pale tu mnaposhinda kesi zenu.lakini mkishindwa kesi mnaanza vimaneno maneno tu
Jaji mkuu CCM..

Rais CCM..

Spika CCM..

Unazungumzia kesi za kubumba kame ile ya Mbowe kuwa ni gaidi?
Ile ilikua ni suala la muda serikali ingejivua nguo ndio maana DPP akaweka mpira kwapani.
 
Kwani si wangepigiana simu na Waziri, kuna sababu gani ya kupayuka majukwaani ili tuone kuwa wanafanya kazi wakati CCM = Serikali tu....
Wanatuona wajinga kutufanyia maigizo.
 
Chama na serikali yake vipo kazini zidi ya wote wanaofanya kazi kwa mazoea.
 
Haangaliwi mtu sura yake katika kumuwajibisha. Kinachoangaliwa ni utimizwaji wa majukumu na kuwajibika.ukishindwa kutimiza majukumu yako ni lazima uwajibishwe Bila kuangalia wewe ni nani.
Mbona mwenyekiti wa ccm amefeli majukumu ya Urais na hachukuliwi hatua!?
 
Mbona mwenyekiti wa ccm amefeli majukumu ya Urais na hachukuliwi hatua!?
Acha kuropoka ropoka kama mlevi wa gongo. Unaanzia wapi kusema amefeli wakati unaona namna uchumi wa nchi unavyoendelea kufanya vizuri,kugusa maisha ya watu.kijenga miradi ya kimkakati kwa wingi,kujenga miradi ya huduma za jamii kila kona ya Taifa letu.kuvutia wawekezaji na mafuriko ya watalii kuja nchini.kuongeza makusanyo ya kodi bila habari za kufungiana biashara n.k.
 
Kwahiyo makonda anakuwa juu ya mama ambaye ndiye mamlaka ya uteuzi
 
Jaji mkuu CCM..

Rais CCM..

Spika CCM..

Unazungumzia kesi za kubumba kame ile ya Mbowe kuwa ni gaidi?
Ile ilikua ni suala la muda serikali ingejivua nguo ndio maana DPP akaweka mpira kwapani.
Kwa hiyo mnaposhindaga kesi zenu huwa mnakuwa na jaji mkuu wenu? Tangia lini spika wa bunge ameenda mahakamani kusimamia kesi na kutoa uamuzi wa kesi?
 
Wewe ndio unaropoka ropoka. Watu hawafanyi kazi sababu ya ukosefu wa UMEME wewe unaleta Nyenyenye!
 
Kwa hiyo mnaposhindaga kesi zenu huwa mnakuwa na jaji mkuu wenu?
Aina za kesi ndio kama hizo nilizokutajia za kubumba , mbona husemi Bob Chacha Wangwe alipeleka kesi ya kuzuia wakurugenzi kusimamia uchaguzi ikatupiliwa mbali?

Wakurugenzi wanateuliwa na rais , Magufuli akawaambia "Nikupe nyumba , gari na bado umtangaze mpinzani utanijua vizuri" au hii ilikupita kiroboto wa Samia
Tangia lini spika wa bunge ameenda mahakamani kusimamia kesi na kutoa uamuzi wa kesi?
Mimi nimesema wapi spika anaenda mahakamani ?

Au na wewe uraia ulipata F kama Nape?

Hao ni wakuu wa mihimili 3 (Executive, Judiciary, Legislature kwa kimombo)

Jielimishe uachane na kupewa script za kuja kusifia humu.
 
Kwa hiyo unaposema kesi ya mtu fulani ilitupwa je kwa akili yako ulitaka mlalamikaji apewe ushindi hata wakati kesi yake haina kichwa wala miguu? Mahakamani kinachoshinda na hoja za kisheria na siyo blaa blaa au kwenda kujazana mahakamani kama ambavyo huwa mnafanya ninyi CHADEMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…