Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Paul Makonda amtaka Gwajima afike ofisini kwake kutolea ufafanuzi juu ya kumkashifu Pengo

Muvi inaendelea wakuu,

Wakati Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa amejisalimisha kwenye Jeshi la Polisi kwa mahojiano hali iliyopelekea Askofu huyo kupoteza fahamu; naye Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemtaka Askofu huyo aripoti ofisini kwake keshokutwa kutoa maelezo kuhusiana na tuhuma za kumkashifu kiongozi mwenzake wa dini.

Makonda amemwandikia barua Askofu Gwajima akimtaka kufikia ofisini kwake kutoa ufafanuzi juu ya maneno makali dhidi ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Katika barua yake, Makonda alisema ofisi yake inataka kufahamu kama uhuru wa kuabudu kikatiba ni kutokuheshimu watu wengine. "Hatuamini kama imefika wakati kwenye nyumba za ibada kumegeuka sehemu ya kutukana na kuwasema watu badala ya kuhubiri habari njema. Tunataka kujidhihirisha malengo hasa ya kutumia maneno hayo ni nini."

11081016_360745177443838_2390948105818373976_n.jpg

makonda kawakamate waislam wa pale mbagala maana kila siku wao ni kusema wakristo makafir na mengine ambayo nashindwa kuyasema hapa.Achana na huyo askofu kuna kuna shtaka kafungue mahakamni,pengo mnafiki tu
 
Tatizo la Makonda ni kufanya kazi na vyombo vya habari.

Ni kijana anae penda sifa.
 
Ndio...kuhakikisha amani inatamalaki wilayani kwake.Gwajima ni hatari kwa usalama wa taifa.lazima uelewe kuna kundi kubwa hapo kiongozi wao wa juu ametukanwa

Alichokifanya Gwajima ni kumkumbusha Pengo kwamba Maaskofu wa Kikristo wamewaelekeza wakristo wote (wakiwemo wakatoliki) kuipigia kura ya HAPANA katiba inayopendekezwa kwa sababu haina Maslahi kwa wakristo.Hakuna amani inayovurugwa hapo na ndio maana hutasikia Jukwa la Kikristo wala Baraza la Maaskofu Katoliki(TEC) wakisema Pengo kaonewa wala kumlaumu Gwajima.
 
Atulie,kuna makosa ya kisheria ambayo yamefanyika mamlaka husika zinafanyia kazi na mlalamikaji mkuu Pengo akiona kuna haja anaweza kwenda mbali zaidi na kufungua shauri la madai huyu, baba anataka afafanuliwe kitu gani kila kitu kipo wazi swala kwa wakati huu limekaa kisheria zaidi kuliko siasa.
 
makonda kawakamate waislam wa pale mbagala maana kila siku wao ni kusema wakristo makafir na mengine ambayo nashindwa kuyasema hapa.Achana na huyo askofu kuna kuna shtaka kafungue mahakamni,pengo mnafiki tu

Thubuutu yake hamumpendi
 
Atulie,kuna makosa ya kisheria ambayo yamefanyika mamlaka husika zinafanyia kazi na mlalamikaji mkuu Pengo akiona kuna haja anaweza kwenda mbali zaidi na kufungua shauri la madai huyu, baba anataka afafanuliwe kitu gani kila kitu kipo wazi swala kwa wakati huu limekaa kisheria zaidi kuliko siasa.

Mlalamikaji katika hiyo kesi atakuwa nani?

Au ndio mwendelezo wa pengo kuwa askofu wa serikali?
 
Mkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani kwenye wilaya yake.Matamshi ya Gwajima yaweza letelea vurugu katika wilaya yake ya kinondoni kati ya wakatoliki wanaomheshimu Pengo na wafuasi wa Gwajima waliokuwa wakishangilia wakati Pengo akiporomoshewa matusi ya nguoni.

HIVYO KUMWITA NI SAWA

Acha propaganda za kizee wewe. Wakristu hawana hizo jazba zs kipuuzi hata siku moja. Yesu mwenyewe alitukanwa na hadi leo anatukanwa hadharani umeshaona mkristu akipigana kuhusu hilo? Itakuwa Pengo? Huyo Makonda kalewa madaraka na kutafuta cheap popularity.
 
Mkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani kwenye wilaya yake.Matamshi ya Gwajima yaweza letelea vurugu katika wilaya yake ya kinondoni kati ya wakatoliki wanaomheshimu Pengo na wafuasi wa Gwajima waliokuwa wakishangilia wakati Pengo akiporomoshewa matusi ya nguoni.

HIVYO KUMWITA NI SAWA

Na wewe jinga tu, kama ni hivyo tusinge hitaji vituo vya polisi
 
Huyu laana ata akiniita mimi siendi hana adabu na ajui wajibu wake kova amuite na dc amuite? dc kawa rpc sikuhizi kweli ccm ni virus kila mtu balozi, mwenyekiti, hakimu, jaji, polisi na mahakama mwisho wao September tena makonda atakuwa dc wa kwanza na wa mwisho kuwa dc kwa muda mfupi kuliko wote kama mjanja auze ma open space yote fasta kabla hakija mnukia

Paul Makonda huyu-huyu aliyemtandika makofi Jaji Warioba??
 
Mkuu wa wilaya ni mlinzi wa amani kwenye wilaya yake.Matamshi ya Gwajima yaweza letelea vurugu katika wilaya yake ya kinondoni kati ya wakatoliki wanaomheshimu Pengo na wafuasi wa Gwajima waliokuwa wakishangilia wakati Pengo akiporomoshewa matusi ya nguoni.

HIVYO KUMWITA NI SAWA

Basi angewaomba polisi wamwachie yeye ashughulikie suala hilo. Otherwise naanza kuamini maneno ya Gwajima kuwa suala hili lina msukumo wa mtu fulani mwenye interest nalo ndani ya wanasiasa
 
Gwajima ni Firauni mkubwa....mzinifu, ma.laya sana...kampiga miti sana Flora...leo hii anatoa maneno hata ktk uchungaji wa uchawi na nguvu za giza hayapo...maneno ya ushenzi na uhayawani...amini mchungaji huyo anatumia ushetani ktk kuendesha ktk lake...na ni mfanya biashara tu...wala sio mcha Mungu...!!

!

Wapendwa nawashauri tupunguze maneno ya kashfa. Mungu kamwe hazihakiwi apandacho mtu ndicho atakachovuna. Kama ni mdomo umemponza Ask Gwajima je wewe unayemtukana unatumia nini?

Huko kwenye KANISA lake nasikia watu wamefunga KAVU wanaporomosha maombi ya kutosha. Sasa tuwe waangalifu maana hukumu ni ya Bwana.

Baba Ask Pengo ni mtumishi wa Mungu, siamini kuwa Leo wakristo tunalipana ubaya kwa ubaya (Kama upo). Hata mafarisayo walipomtukana Yesu, neno la Mungu linasema hakufunua kinywa chake. Ask Pengo ni kiongozi mwenye kufuata mfano wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tena imeandikwa ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la pili...... Kesi ya wana wa Mungu lini ikaamuliwa na MATAIFA????? Eeeeee Mungu, nyosha mkono wako, wanadamu wanafanya ghasia juu ya watumishi wako. Eeeee Bwana ikikupendeza tuinulie mtumishi wako, nabii wa siku, kulimaliza kesi ya watoto wako ili injili iendelee kuhubiriwa. Kwa Jina la Yesu Kristo tumeomba. AMEN

Mwisho je,, Hawa wote wanaomshitaki Ask Gwajima wametumwa na Pengo (siamini). Kama wana vita yao na Ask Gwajima isipitie kwa baba yetu mpendwa Pengo. Anyway vita ya KIROHO siku zote humalizikia rohoni. Kwenye hili tuwe waangalifu sanaaaaaaaa!!!

Mwisho wale mnaojiita wakristo, tabia ya kukashifu dini ya mwenzio au kiongozi wa KANISA lingine sio nzuri kabisa. Mkumbukeni Mtume Paulo alipowajibu wale waliokuwa wamejimilikisha jina la Yesu kuwa... as long as Kristo anahubiriwa iwe kwa hila au..... jina la Bwana litukuzwe.

Tuendelee na maombi ya kuiombea nchi yetu changamoto ni nyingi, tuukomboe wakati, usiutie unajisi moyo wako.

Mungu atubariki na atusaidie.

Queen Esther
 
Back
Top Bottom