Please get it. Mwandishi hakuuliza hilo swali kama habari ngeni, mpya. Alikuwa anamfikishia Makonda tuhuma nzito kumhusu ambazo tayari zimewasilishwa kwa jamii (public) na mhanga Tundu Lissu kupitia vyombo vya habari.
It is already public knowledge. Hakuna kujidanganya. Kila anapopita na kuongea hadharani ajue kuna jamii kubwa inajiuliza kuhusu uhusika wake katika risasi za Lissu na, hivyo, usafi wake kisiasa. Ni swali ambalo bado linaning’inia katika jamii hasa kwa vile miaka imepita bila serikali (polisi, DPP) kuchukua hatua yoyote ya kisheria kuondoa utata.
Aidha, Tundu Lissu aliyeweka tuhuma hizo hadharani hajawahi kuchukuliwa hatua kwa upotoshaji wala kuchafua watu binafsi na serikali kwa kauli zake mubashara. Na ni kauli ambazo ziko kwenye kumbukumbu za maandishi na sauti na picha rasmi.
Kwa vile anayetuhumiwa ni mwanasiasa active, taaluma ya uandishi wa habari inadai mtuhumiwa anapopanda katika majukwaa ya kisiasa lazima aulizwe hilo swali ili kuondoa shaka kuhusu usafi wake kisiasa kiasi cha kustahili kupewa nafasi ya kitaifa kwenye fani hiyo. Hiyo huwa fursa maalum ya yeye kujiswafi kisiasa. Ni moja ya kanuni kuu za professional journalism.
The guy needs to be advised to just play humble and apply a bit of wisdom.