Paul Makonda arejea, aibukia Uwanja wa Ndege Arusha uliopo eneo la Kisongo

Paul Makonda arejea, aibukia Uwanja wa Ndege Arusha uliopo eneo la Kisongo


View: https://www.youtube.com/live/IHztQrYAF0g?si=aTpKZrIJOrQWndNq

Updates...

Kumepita ukimya wa takribani mwezi mmoja huku swali kuu likiwa yupo wapi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, RC Paul Makonda lakini leo Agosti 16, 2024 swali hilo limejibiwa baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza akikagua ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Arusha uliopo eneo la Kisongo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Mkoa Arusha na kukagua Ujenzi huo unaondelea kutekelezwa leo Agosti 16, 2024 ameeleza chanzo cha utanuzi wa Uwanja huo.

RC Makonda amelezea kuwa itakuwa chanzo cha utanuzi kwa Uwanja huo wa ndege ni kuongeza kundi kubwa la Watalii wanaoingia nchini kupitia mkoa wa Arusha kwa uwepo wa vivutio mbalimbali vya utalii ambapo itaongeza Uchumi kwa taifa letu na kujitangaza zaidi kupitia utalii.

Mkandarasi
Moja ya Miradi ambayo itafanyika katika uwanja huyo wa ndege ni kufunga taa za kuongozea Ndege kwa sababu uwanja wa ndege uwe kufanya kazi masaa 24.

"Tumeshapata Mkandarasi tayari na tumeshamkabidhi na sasa yupo katika hatua ya kufanya usanifu wa mfumo wenyewe".

"Lakini tatizo ambalo tunalo ni hile ardhi ya kufunga hizo taa za aproch ya kutua ndege, kwa sababu kiwanja chetu kutoka pale mwisho tuna mita 200 na lakini tunahitaji mita 500".

Kuna watu watakataa kama ni Makonda, watasema ni mzuka, watasema amekonda, watasema atatangazwa amekufa ndani ya muda mfupi na wengine watasema huyo ni Makonda feki
 
Mikono yako ikijaa damu za watu ni lazima tukuombee kifo kama yule shetani mkuu aliyetwaliwa kuzimu.
Aah unasemea yule mtakatifu sio.......angekua kama mnavyotaka kuaminisha watu wakina Makonda wasingerudi.....,,,,tunashangaa kambi ya wazuri hawafi ndo inasambaratika
images.jpeg-90.jpg
 
Back
Top Bottom