Pre GE2025 Paul Makonda: Arusha hawakupata barabara kwa muda mrefu kwa sababu waliendekeza majungu, ushirikina na siasa uchwara!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ndio maana nikasema ulitaka kufanya hivyo kwenye maendeleo uwe chama kimoja. Ukiwa vyama vingi peleka maendeleo kote na sio kwa chama chako tu. Ukifanya hivyo unavunja katiba .
 
Maamuzi ya kujenga barabara ni ya Serikali, hivyo staki kuamini kuwa Serikali ilizuiwa na majungu kujenga hizo barabara.
 
Tuletee clip inayoonyesha Lema akionyeshe mkakati ya ujenzi wa barabara maenro husika?

Hata hujui mchakato wa barabara inaanzia wapi. Hilo swali ungemuuliza TANROADS, Waziri wa Fedha na Waziri wa Miundo mbinu.
 
Mfumo wa Vyama vingi ni kuja na sera mbadala,Kwa hapa Tanzania Wapinzani wamefeli vibaya.

Chama chako kina sera zipi mbadala kwenye Kilimo?
 
Rome haikujengwa siku moja Mangi,jiji la Arusha limeanza kupiga hatua siku nyingi na hawa wenzetu pia watafika huko.Si umeona Iringa na Songea wako wapi ukilinganisha na miaka kumi iliyopita?
Shinyanga na Geita ni majiji ya utalii!?....Geita ni halmashauri, shinyanga ni town council...ng'ombe na Mchele haihitaji barabara kihivyo🤣🤣
 
Notajie mbunge mmoja wa CCM aliyejenga barabara kwa pesa zake Yani kilomita kuanzia 10. Kutoka kwenye mifuko wake.
Wabunge wanajenga kutoka kwenye Serikali za Vyama Vyao ,Sasa hamna Serikali mnategemea nini? 😆😆
 
Kwenye kampeni Huwa mna nadi nini? Na mnatekeleza nini?

Kama ni serikali,kazi ya Mbunge ni ipi?

Kazi ya mbunge ni kusimamia serikali kuhakikisha matatizo ya wananchi yaliyo Chini ya serikali yanatatuliwa. Kama maji, afya, barabara etc
 
Punguza ukabila.
hujaishi nao hao watu wanamambo ya kijinga sana kuzungukazunguka na kupinga miradi kama mabarambara wanatabia ya kuifuata wakati wa kutanua ili kumwaga lami wananza kuzungukazunguka wewe fikiria mtu anaotesha mgomba mpaka karibu na nguzo ya umeme hovyo sana
 
Kazi ya mbunge ni kusimamia serikali kuhakikisha matatizo ya wananchi yaliyo Chini ya serikali yanatatuliwa. Kama maji, afya, barabara etc
Wapinzani mkubwa wachache mtasimamia vipi uwajibikaji wa Serikali wakati hamna tool hiyo ambayo inawahitaji muwe wengi Ili mpate Nguvu ya maamuzi?

Mfano Serikali ikiwa inajibu tunatafuta hela miaka inaenda mtawafanyaje?

Hiyo ndio hasara ya kuchagua upande usio sahihi ambao hauwezi kuunda Serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…