Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 22 Oktoba, 2023 mjini Dodoma, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Dokta Samia Suluhu Hassan, pamoja na masala mengine, imeridhia kwa kauli moja na kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji na uwekezaji wa bandari.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua Ndugu Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Ndugu Sophia Edward Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.


Halmashauri Kuu ya CM Taifa pia imemteua Ndugu Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), akichukua nafasi ya Ndugu Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.

Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dokta Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.

View attachment 2789088
Mleteni na Saa Baya!!!
 
Makonda hakuwahi kufanya kazi ccm , huyu amezoea mabavu ya kutumia dola kwenye vyeo serikalini .
Pitia tena kumbukumbu zako, Makonda ametokea UVCCM. Ila nafikiri UVCCM ya kipindi fulani haikupika watu vizuri.
 
Tusigombane na MA X zetu pindi tukiachana uwezi jua atakuja kua nani.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Nice and interesting move. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji1531][emoji1531]
 
Binafsi uteuzi huu nausherekea sana. Paul Makonda anastahili sana kuwa kiongozi. Ni nani asiyejua kuwa Paul Makonda kichwa chake kinafanya kazi vizuri? Paul anauthubutu. Paul anandoto. Paul ana authority.

Kitu kimoja ninachoweza kumshauri Paul ni matumizi ya lugha na kujikweza. Aache!!!

[emoji120][emoji120]
 
"Siasa ni ngumu kuliko Fikizia" 😁
Naamini Paul amejirekebisha na amekua. He's a good guy off course.
 
Hatimaye mama Abdul asalimu amri kwa Sukuma Gang,siku si nyingi Luhaga Mpina ndani ya cabinet.
 
Hongera kwake.
Benchi aliyosugua bika shaka ameshajifunza mengi.

Ila hana buni kuomba msamaha kwa wote aliyowaumiza...Kaumiza na Kujeruhi wengi.
 
Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua Ndugu Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,
Kazi ya ukatibu si inahusu uandishi, sasa huyu ndugu tunaambiwa hana elimu atatuandikia nini kwenye chama chetu
 
Back
Top Bottom