Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi

Paul Makonda ateuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi


Ndugu Paul Makonda ameteuliwa na CCM kuwa Katibu Mwenezi.

===

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana leo tarehe 22 Oktoba, 2023 mjini Dodoma, katika kikao chake maalum, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Ndg. Dokta Samia Suluhu Hassan, pamoja na masala mengine, imeridhia kwa kauli moja na kuielekeza Serikali kuendelea na hatua ya utiaji saini mikataba ya uendelezaji na uwekezaji wa bandari.

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, imefanya mabadiliko madogo ya Sekreterieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kwa kumteua Ndugu Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Ndugu Sophia Edward Mjema ambaye ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais Masala ya Wanawake, Watoto na Makundi Maalum.

Halmashauri Kuu ya CM Taifa pia imemteua Ndugu Rabia Abdallah Hamid kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), akichukua nafasi ya Ndugu Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki.

Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dokta Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 - 2025.

===

Pia soma:

--

Ifuatayo ni historia fupi ya safari ya kisiasa ya Paul Makonda ambayo inaangazia baadhi ya matukio muhimu yaliyochangia kwenye kutengeneza historia hiyo.


Julai 29, 2011: Rais wa wanafunzi wa Chuo cha Ushirika Moshi (MUCCoBS) amteua Paul Makonda kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi. Uteuzi huu wazua mjadala mkali katika Bunge la Wanafunzi, huku baadhi ya wabunge wakionesha kutokuwa na imani naye kwa sababu ya kuhairisha mwaka wa masomo chuoni hapo.

Septemba 27, 2011: Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) wamchagua Paulo Makonda katika nafasi ya Mwenyekiti, akiwashinda wagombea wengine kutoka vyuo vikuu vinne.

Oktoba 1, 2012: Makonda ajiuzulu nafasi ya uenyekiti TAHLISO Taifa kwa kile alichodai ni kuepusha mgongano wa kimaslahi kwa kuwa alipanga kushiriki uchaguzi katika chama chake cha siasa, Chama cha Mapinduzi (CCM).

Oktoba 24, 2012: Paul Makonda agombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na kushika nafasi ya pili baada ya kupata kura 241 nyuma ya Mboni Mhita aliyepata kura 489 katika duru ya pili ya uchaguzi huo.

Februari 7, 2014: Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete amteua Paul Makonda kuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba, akiwakilisha kundi la watu wenye malengo yanayofanana linalojumuisha wajumbe 14 kutoka Tanzania Bara.

Februari 19, 2015: Rais Kikwete alimtua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Machi 13, 2016: Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli afanya mabadiliko na uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26. Katika uteuzi huo, amteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Machi 22, 2017: Kamati iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari Nape Nnauye kuhusu uvamizi katika kituo cha utangazaji cha Clouds yabainisha Paul Makonda alivamia kituo hicho mnamo Machi 17, 2017, majira ya usiku. Kufuatia taarifa hiyo, wadau mbalimbali, ikiwemo Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilimtaka Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Makonda. Makonda hakutenguliwa.

Januari 31, 2020: Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani yatoa taarifa ya marufuku kwa Makonda na mke wake, Mary Felix Massenge, kutoingia nchini humo kwa madai ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Julai 15, 2020: Rais Magufuli amuondoa Paul Makonda katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Utenguzi huo ulihusianishwa na hatua ya Makonda kutangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Kigamboni.

Julai 20, 2020: Makonda aibuka mshindi wa pili kwenye uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM kwa kupata kura 112, nyuma ya mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Faustine Ndugulile.

Juni 9, 2022: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni yatupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Makonda na Mkurugenzi wa Mashitaka juu ya matumizi mabaya ya madaraka wakati wakiwa viongozi wa umma. Kesi hiyo ilifunguliwa na Said Kubenea aliyewahi kuwa Mbunge wa Ubungo.

Oktoba 22, 2023: CCM yamteua Paul Makonda kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi.
3e763752-e46e-41d7-9271-a0fc48630061.jpg
2adec1f1-437e-47e2-bf7d-f184347e82d6.jpg
40e9d7e5-44c1-40fc-99e7-08d75d2eef80.jpg




Mama amelipa fadhila kumbe.
 
Na taarifa za chini chini ndani ya Chama ( CCM ) zinasema Uteuzi wa Paul Makonda umewakwaza wengi na huenda Mtu akaja Kuhujumiwa mazima kuelekea 2025.

Kazi ipo.....!!
 
Itakuwaje? Nauliza!

Kumbe ndiyo maana Wahenga walisema tuwe na akiba ya maneno! Usiongee yote!

Hakuna hakimu mzuri au mbaya Kama muda!
Screenshot_20231023-111240.jpg
 
Bloomberg wamenena hii sisi tuko busy na katibu mwenezi mpya
Screenshot_20231023-125009.png
 
Chadema walivoona taarifa Jamaa amerudi kazini tena nafasi nyeti wakapaniki Tunduma, nakuanza fujo!
 
Chadema walivoona taarifa Jamaa amerudi kazini tena nafasi nyeti wakapaniki Tunduma, nakuanza fujo!
 
Back
Top Bottom