Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Paul Makonda atishia kuwataja wanaolipa watu 'Kumtukana Rais Samia mitandaoni', wamo Mawaziri

Huyu ni mwehu wallah.
Yeye kila wakati anataka kutengeneza njia yake kwa kutia majani njia za wenzake.
Hatowataja maana hawapo sema tu amewaharibia wenzake. Samia atakaa kwa kuhisi hisi kitu kisichokuwepo.
Ni kama mchezo wa Nabii feki na waumini wake huwa hauishi. Kila siku anakujengea mazingira kuwa una maadui wengi na yeye ndiye msaada pekee
Samia naye anajua kuwa huyu jamaa ni chizi na wala hawezi kupoteza muda kuwaza kuhusu maneno yaliyotamkwa na chizi.
 
Endapo kama wateule wapo, basi hakika binaadamu hawana jema, wallahi wa bilaahi.
Kaka haya mambo sio mapya kwenye serkali hii! Kwani kipindi cha JPM Makamba na Nape mbona walimsema na kumsengenya vibaya sana Magufuli pamoja na kuwa walikuwa Wateuliwa wake! Wakamsema Mshamba, Mwoga na maneno kibao ya kejeli kwenye mawasiliano yao ya simu yaliyo leak!
Hata Chalamila alisema kuwa kuna Mawaziri wako ndani ya serkali wanatafuta hela ya kutaka kugombe Urais japo Kikwete alionekana akimponda Chalamila kuwa ni uongo na ujinga tu hakuna kitu kama hicho lakini leo imejirudia tena kwa Makonda!
Sema wabongo tuna tabia ya kuchukulia mambo juu juu na wengi pia sio wasomaji wazuri wa habari!
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha.

Akizungumza wakati wa Kumbukumbu ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, amesema "Kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia mnanijua na mimi nawajua, wengine ni Mawaziri leo tarehe 12 iwe mwisho"

Aidha Makonda amemwomba Rais Samia kutoa Fedha za ujenzi wa Kilomita za 20 za Lami Jijini humo na kueleza kuwa Wananchi wamemtuma amuombe Mama yake na wanampima kama ni Mama yake kweli
=========

Akitoa salaam za mkoa kwenye kongamano la kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine leo hii 11 April 2024, amesema kuna watu, wakiwemo mawaziri wanawatuma watu kumtukana Rais Samia mitandaoni.

Makonda kasema anawajua na wao wanamjua. Amewataka waache kufanya hivyo leo hii. Ameonya wasipoacha atawataja majina yao siku ya Jumatatu tarehe 14 April 2024.

Unaweza kubashiri ni mawaziri gani wanafanya hujuma hizi dhidi ya bosi wao? Au Makonda anatafuta kiki?

Maana hata jiwe alimdanganya kama hivi, ndiyo maana jiwe akawa karibu sana na Makonda. Jiwe alipokuja kugundua kuwa aliingizwa chaka akamtema.

View attachment 2961639

Source:. Kumbukizi ya Edward Moringe Sokoine

Pia, soma=> Rais Samia akiashiriki Misa Maalumu ya miaka 40 ya kumbukizi ya Kifo cha Hayati Sokoine
Huyu tangu katimuliwa kwenye uenezi karukwa na akili
 
Mimi naamini samia atakuwa analijua hilo sasa nani wa kulisema hadharani naamini katumwa aliseme hili
Kwahiyo mtoto katoka chumbani na siri za familia kazisema mbele ya wageni ? Mama mwenye nyumba ameshindwa kulisema?
Kishafanya rotation ya mawaziri mpaka basi , sasa sijui labda akina Babu Tale sasa wapewe uwaziri.
 
Baraza la mawaziri limechafuka!! livunjwe maana mawaziri wanatuma watu kumtusi Mh. Rais!!
Huu Sasa ni uhujumu na uhaini wawazi nasisi raia hatuwezi kuvumilia Baraza lisilo na nidhamu kiasi hiki.
Rais anazidiwa intelijensia na mkuu wa mkoa!! yaani mkuu wa mkoa anamwambia rais hajui kuchagua hata viongozi kunanamna anamwona hayupoo serious ama hajui kazi😞😞
 
Kwahiyo mtoto katoka chumbani na siri za familia kazisema mbele ya wageni ? Mama mwenye nyumba ameshindwa kulisema?
Kishafanya rotation ya mawaziri mpaka basi , sasa sijui labda akina Babu Tale sasa wapewe uwaziri.
Makonda ni speaker ya Mama sema speaker hiyo inakiuka maagizo na kuongea sana kupitiliza siunajua mtu akitumwa na Mama!
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ikifika Aprili 15, 2024 atawataja kwa majina Watu wakiwemo Mawaziri wanaotoa fedha za kuwalipa Watu ili wamtukane Rais Samia mitandaoni kama hawataacha...
Mama aanze na Makonda vinginevyo serikali itakuwa inapenda na kufurshia ubuyu.
 
Nani huyo aliyetukana mtandaoni, hebu naomba kuona.
Hahaha tulia muda si mrefu mambo yatakuwa uchi maana ndani ya chama adui wa Samia sio team JPM ni team iliyompambania kuingia hapo sasa inadai kiti maana aliambiwa kaa tu 2025 utapisha malizia miaka ya mwenzako alotangulia mbele ya haki!

Ila sasa Mama naona kibuyu cha asali kishakuwa kitamu na hapoaalipo lile kundi anajua kabisa nguvu yake ilivyo kwa hiyo hawezi kukurupuka kuwatoa kwenye circle yake!

Wajuba tuanikumbuka sana kauli ya mwamba mmoja iliyosema Mama endelea maana 2025 utakuwa ni wewe labda mambo yaharibike sana!

Sasa kauli ya mzee vijana wanaifanyia kazi ili mambo yaharike ili Mama awapishe maana mahesabu yanagoma kabisa maana pia ule utamaduni wa akitoka Mwislam anaingia Mkisto ndo inaumiza sana kichwa cha wakongwe!
Nadhani mpaka hapo umenielewa!
 
Back
Top Bottom