Hili suala la viongozi kujipendekeza kwa Raisi Samia sasa limeanza kupita kiasi, na lisipodhibitiwa litaleta mtafaruku nchini.
Mfano ni hili suala la Raisi Samia kutukanwa. Siamini kabisa kwamba Raisi Samia anatukanwa, kwamba maneno ya kumkosoa na kumpa majina kama Mama Tozo sijui ni jambo jipya kwa raisi wa Tanzania ambalo halikuwahi kutokea kwa maraisi wengine. Kina Nyerere waliitwa Haambiliki; Mwinyi Koti; Mkapa Fisadi; Kikwete Dhaifu; Magufuli Dikteta Uchwara. Hakuna alieimba eti raisi anatukanwa.
Ninachoona kikitokea hapa ni viongozi kama Makonda na wengine kama yeye kutafuta kila namna ya kujipendekeza kwa Raisi Samia na kujifanya wana uchungu sana na yale wanayosema Watanzania dhidi ya Raisi Samia, na kuyakuza sana kuwa ni matusi, kama vile Raisi Samia ndie raisi pekee nchini kupitia vitu kama hivyo.
Ninamtahadharisha Raisi Samia asiache watu hawa kuanza kuingia kichwani kwake, kwa kukubali huruma zao fake na kuanza kuwaona kama watetezi wake waaminifu. Asichoelewa Raisi Samia ni kwamba hawa watu wameshaiona saikolojia yake, kwamba anapenda kusifiwa kama ilivyo silka ya wanawake (maana sijawahi kumsikia akikemea kusifiwa kwa kufanya kazi yake) na sasa, zaidi ya kumsifia, wameamua kumwonyesha kuwa wanaumizwa sana na yanayosemwa dhidi yake.
Rais Samia, hawa watu wanakuchezea tu, kwa sababu wameshakusoma. Kukubali kwako yale wanayofanya inaweza kuwa ni kuonyesha udhaifu kwa namna fulani. Wakemee wao, waambie uraisi ni ukubwa na ukubwa ni jaa. Kuna kukosolewa na hata kutukanwa, nk.
Usipofanya hivyo, unaweza kufikia kuwa na mentality ya kudhani watu wanaosemwa wanakutukana wanakufanyia hivyo kwa sababu wewe ni raisi mwanamke, au la labda kwa sababu ni raisi toka Zanzibar, au labda kwa sababu ni raisi mrithi wa Magufuli, nk. Once unaweka mindset kama hiyo kichwani mwako basi itakuwa ndio anguko lako, kwa kuwa utakuwa tegemezi kabisa wa hawa watu wanaoimba eti raisi anatukanwa. Siku zote utataka wakutetee, na kama sehemu ya kukutetea utataka kusifiwa kila wakati, zaidi ya ilivyo sasa. Na wewe utakuwa ukifanya kazi na kuongea kwa namna ya kutafuta sifa. Angalia sana juu ya hili.