Naomba niwatakie mapumziko mema wale wenzetu waliotangulia mbele za haki kwenye maombezi ya bwana yule anayejiita nabii Mwamposa,baada ya hayo tujikumbushe juu ya swala la Mh .Paul Makonda kutuhumiwa kumiliki genge la waharifu ambapo kwa nchi yenye usalama uliotukuka na intelligensia dhabiti kama Marekani sidhani kama wamekurupuka au wamemuoneo Mh.Paul Makonda,katika swala hili naomba tuweke uchama pembeni na tujadili kwa mapana juu ya hatima ya nchi yetu .
Naomba nikili wazi kuwa kwa kashifa na tuhuma hizi juu ya RC .Makonda sidhani tena kama kiti anachokikalia cha U RC kinamfaa,Na kwa muungwana akivuliwa nguo huchutuma,Makonda ili kulinda heshima yake na kwa kujali masirahi mapana ya nchi yetu anapaswa kukaa pembeni/ kujiuzulu ili kulinda heshima yake
Naomba nimjulishe tuu kidogo kuwa huu mwezi hautapita bila kuvuliwa madaraka yake,sasa ili kuficha aibui hii namuomba Mh.aandike barua ya kujiuzulu ili kuepukana na aibu lakini pia kuisafisha twasira ya nchi yetu mbele ya mataifa ya ngambo,kama taifa na wananchi wa somi kwa dunia ya Leo hakuna namna utajitenga/ kujiweka mbali na mmarekani,kwa nyakati hizi mmarekani ni sawa na maji, usipo yanywa,utayaoga,usipo yaoga utakutana nayo chooni nk.,so hatuwezi kujitutumua kuwa Marekani hawezi kutupangia mambo yetu ili khali hata mataifa yaliyoendelea wana mpigia magoti mmarekani.
Rai yangu kwa Mh. Makonda ni kuwa ajiuzulu mapema kabla Mh .Rais hajamtumbua,lakini pia watanzania wote tuungane na kupaza sauti ili huyu bwana aenguliwe kwa mstakabali mpana wa taifa letu kwa maana yajao yatakuwa makubwa kuliko haya yaliyo mkuta Mh Makonda ,maana mmarekani amepania hasa kuiadhibu nchi yetu,so kabla mambo hayawa makubwa Mh paul ajitathimini zaidi ,hesabu zangu zinasema Makonda hatamaliza huu mwezi akiwa madarakani .
Sent using
Jamii Forums mobile app