Paul Makonda kufikishwa Mahakamani Februari 3, 2022 katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka

Paul Makonda kufikishwa Mahakamani Februari 3, 2022 katika kesi ya matumizi mabaya ya madaraka

Hivi jinai mshtakiwa anaombwa kufika mahakamani tarehe tajwa au anatakiwa atokee mahabusu ndani ya karandinga? Sijaelewa.
aise kweli unakichwa kizito makonda kashitakiwa nakubenea na mahakama imeamuru makonda kufika kujibu mashitaka mahakama inautaratibu wa samaz(summos).....Sasa ukitaka akashikwe na polisi unavotaka akae lupango akatae huo wito....ukiwa hujaelewa uulize
 
Pia tunaomba ajibu haya

1. Nani alimuua Ben, Azory, Mawazo Lwajabe.

2. Nani alimteka, Roma, Nondo, Mo,

3. Waliookotwa kwenye viroba ufukweni walikuwa akina nani

Kumbukeni huyu ndiye aliyekuwa anatoa taarifa kuwa Fulani atapatikana siku Fulani.
Mfano akisema hayo yote uliyoandika hajui mhusika!

Una ushahidi wa kumlink na hizo hatia?
 
Makonda aliharibu biashara ya ngada ya Dj na vijana wa mitaa ya Manyanya na kinondoni yote wakaimarisha afya zao
 
Ukiangalia kwa jicho la kawaida unaweza fikiri kama Kubenea jasiri ila kwa wanao juwa this is deep state....
Nania yao wala sio hii tunaiyona ila kumbukeni Sababu za USA kumuekea vikwazo bishite.... Tunasafari ndefu sana as nation....
Ujuavyo ACT inaunga mkono kwakilakitu kinachofanywa kazi na ccm naserikali ya awamu ya 6 ,......hivyo hata Kama umeota inaweza kua ndoto yakweli
 
Kwa kushitakiwa na kubenea?

Ingekua jamhuri, hapo mtu unaweza kuwaza!

Vipi clouds wakigoma kutoa ushirikiano! mutawalazimisha?

Maana huo ndio ushahidi pekee kila mjinga anashabikia!

Kuhusu mauaji hata USA wameshindwa kutoa ushahidi!
Kwahiyo unakubali kwamba ana jinai yakujibu ila tu anaweza kuwalaghai clouds wakagoma kutoa ushirikiano?

Hivi uvamizi ule wa hadharani bado kuna mtu anataka kumtetea Makonda?

Hata kama mtu ungekuwa unalipwa na Makonda kumtetea mitandaoni inabidi uwe na roho ngumu kutetea uhalifu wa Makonda.
 
Kwamba jinai wasiione clouds uione wewe?
 
Makonda aliharibu biashara ya ngada ya Dj na vijana wa mitaa ya Manyanya na kinondoni yote wakaimarisha afya zao
Nikikubaliana nawewe kwenye hilo utakubaliana na mimi pia kwenye uhalifu alioutenda hadharani mfano pale clouds hadi tume ikatoa majibu ya kuhisika kwake na uhalifu.
 
Basi itabidi aieleze mahakama kwanini alikuwa anasema fulani atapatikana siku fulani na kweli inakuwa hivyo baada ya kutekwa.

Roma alitekwa Makonda akasema atapatikana siku fulani wakati yeye sio msemaji wa polisi.
Unajua mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoani kwake?
 
Pia tunaomba ajibu haya

1. Nani alimuua Ben, Azory, Mawazo Lwajabe.

2. Nani alimteka, Roma, Nondo, Mo,

3. Waliookotwa kwenye viroba ufukweni walikuwa akina nani

Kumbukeni huyu ndiye aliyekuwa anatoa taarifa kuwa Fulani atapatikana siku Fulani.
Ume sahau na kupigwa risasi kwa Tundu Lissu ,Pamoja na kwamba T Lissu kureport kwenye vyombo vya dola kwamba ana fatiliwa na gari flani ha dar na kwingineko lakini Makonda Kama Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa wa daresalaam hakuchukuwa hatua yeyote.
 
Khilo gazetin la raia mwema Ni ungo tu nimewambiwa watu kila siku Ana guess tu
 
Kwamba jinai wasiione clouds uione wewe?
Ama kweli ukipenda chongo utaona kengeza tu. Yaani uhalifu uliofanyika clouds kila mtu aliuona na tume iliyoundwa kuchunguza ikaja na majibu kwa Makonda kuhusika bado huoni ni jinai?

Kwakweli kuna baadhi ya watu mna asili ya ubishi unaweza kusema kubisha kwamba Dodoma haipo Tanzania na ukaamini hivyo wakati unajua kabisa ipo Tanzania.
 
Unajua mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoani kwake?
Ambae anajua fulani atapatikana lini hadi saa?

Jeshi la polisi lina taratibu zake na lina msemaji wake kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi kitaifa. Na ndilo linalohisika na uchunguzi na kutoa taarifa sio mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.
 
Ama kweli ukipenda chongo utaona kengeza tu. Yaani uhalifu uliofanyika clouds kila mtu aliuona na tume iliyoundwa kuchunguza ikaja na majibu kwa Makonda kuhusika bado huoni ni jinai?

Kwakweli kuna baadhi ya watu mna asili ya ubishi unaweza kusema kubisha kwamba Dodoma haipo Tanzania na ukaamini hivyo wakati unajua kabisa ipo Tanzania.
Ni kweli huenda wote tuliona hiyo video lakini kwanini uumie wewe zaidi?

Kwanini uwashinde maumivu clouds ambao wao wametamka wazi hawana nia ya kufungua kesi?
 
Back
Top Bottom