Pre GE2025 Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sakata la Makonda na wanaharakati linanikumbusha mambo mawili.

La kwanza ni kwa viongozi kuwakemea subordinates wao hadharani ama moja kwa moja (directly) au kwa njia nyingine (inderectly). Kwa Tanzania, Magufuli aliongoza sana kwa kukemea moja kwa moja kwa vile alikuwa hatunzi kitu lakini viongozi wote huwakemea subordinates wao kwa njia moja au nyingine; inaweza kuwa verbal au kwa matendo mwngine. Ni sehemu ya majukumu ya vongozi kuwakememea subordinates wao; mtu anapokemewa na kiongozi wake huo siyo udhalilishaji, ingawa yeye binafsi atajiskia vibaya. Naliona sakata hili la Makonda likifanya jitihada za kuondoa hilo jukumu la kiongozi kukemea subordinates, na sijui mwisho wake utakuwa ni nini iwapo subotrdinatees watakuwa wanajua kuwa kiongzi ni mshikaji tu, hata nikifanya makosa hatanifanyia chochote kwani utakuwa ni udhalilishaji.

La pili ni presha kwa Rais kutengua uteuzi kutokana na hisia za watu juu ya mteule wake. Hii inanikumbusha wakati wa Mkapa, Waziri Mramba aliposema kuwa hata kama wau watakula nyashi kazima serikali inunue ndege ya Rais. maneno yale yalikuwa ni matusi kwa watanzania. Kukawekwa pressure kubwa sana ya kumtaka Mkapa atengue uteuzi wake, lakini Mkapa alisme atu kuwa alipoteua mawaziri hakushinikizwa na hata anapytaka kuwatengua hatafuat mashinikizo. Mkapa ni rais pekee ambaye mawaziri wake wengi walidumu miaka kumi yote ya utawla wake pamoja na kuwa kulikuwa na pressure sana kutokan na zoezi la ubinsfshiaji lilivyokuwa na rushwa wakati huo.

Kwa Tanzania siasa hizi za kuweka pressure kwa rais ili atengua mtu tusiyemtaka kutokana na maneno aliyesema wakati anamkemea mtu hazisaidii sana. Kupiga kelele kila siku kuwamudhalilishaji ni kukosa kazi kwani Rais mwenye pia anajua kilichotokea kwa hiyo kelele za nje haziongezi lolote labda pressure tu.
 
Hivi huko chadema kuna mtu hata mmoja anaakili kweli??
Punguza mazoea, CHADEMA imeingiaje hapa?. Mimi nilisikiliza mahojiano yao mpaka mwisho yule dada hakuwa na kosa la kinidhamu lolote.
 
Hivi uzuri wa mke na ubaya wa sura unakujaje kwenye mkutano wa kazi? Haya endeleeni kumpa kichwa
 
Uzuri mara nyingi, kama siyo zote; huwa anawadhalilisha wanawake. Siku akiingia kwenye 18 ya watu waliokata tamaa na kujichokea na maisha, ndiyo akili itamkaa sawa.
 

Hilo utafanya wewe siku ukiwa mkuu wa mkoa. Hiyo ni staili yake hupendi jiue.
 
Ila kwa hizi kelele Makonda atajirudi la sivyo akirudia.
 
Ukitazama utaona kabisa kamtaja rais ili wapiga mapambio wenzake wamuogope. Rais ametukanwa na mkuu wa mkoa gani? Yeye ametukana kama sehemu ya kumtetea rais? Rais anahusika vipi na kejeli yake kwa yule dada
Alichosema Makonda kwa taratibu za utumishi ni makosa. Maneno yale akiyatumia mtumishi mwingine ''HR' ana kila sababu ya kumchukulia hatua mtumishi huyo. Ni popote duniani Duniani ! hiyo ni taratibu ya utumishi

KBashite kumtumia Rais kama kinga ni kumwingiza katika mjadala bila sababu. Ikiwa Rais alitukanwa haitoi ticket kwa yeye kufanya hivyo, ni issue ni mbili tofauti . Anatakiwa ajibu hoja zinazomhusu

Kusema 'mimi si mchumba wako' ni kumkosea mtumishi adabu. Yule ni Mwanamke , ni Dada, ni Shangazi na 'mke wa mtu' akiwa ni mama wa watoto. Alichosema Bashite ni matusi kwa Familia na jinsia na Umma kwa ujumla

Kusema '' nina mke mzuri' anamaanisha yule ni mbaya . Hivi mtumishi na kiongozi wa Umma anafikiaje mahali pa kudhalilisha mtu namna hiyo. Again, uzuri au ubaya wa mtu ni jambo lisilohusiana na utumishi wa umma

Jambo linalosumbua Umma ni jinsi Viongozi anavyo ogopwa Bashite. Tulidhani ni JPM tu lakini ni zaidi

' Kuna kitu ' hatujui ni nini . Yuko wapi Waziri Mkuu ? Yuko wapi Makamu wa Rais? hivi hili nalo limsubiri Rais!

Lakini pia Rais ameyasikia kutoka UWT na sijui kama Bawacha wamesema, je, kimya chake kinaeleza nini kuhusu udhalilishaji tena wa Wanawake!

Kesho viongozi hao watakuwa na ''moral authority' gani ya kukemea udhalilishaji ikiwa hili wamelifumbia macho

Madam President, Hon Vice President, Hon Prime Minister! please hili si la kufumbia macho! ikiwa hamuwezi basi japo kemeeni tu kwa kujiuma uma la sivyo siku mkiongelea udhalilishaji msijeshangaa tukicheka mkidhani mumesema la maana kumbe tunamaanisha kicheko cha yale yale
 

Na bado! Atafanya zaidi.
 
Soma kitabu Cha Hitler na alivyoingia madarakani, kisha fuatilia ni Nini alifanya baada ya kupata madaraka.
Propaganda za US na washirika wake hizo,wachana nazo,dunia ya leo hii utamdanganya nani.China ,Korea,Russia tumekuwa tukiambiwa zinatawaliwa na madikteta,sisi wenye democrasia mbona umaskini umetamalaki?
 
Samia katukosea heshima sana kumrudisha kwenye uongozi huyu majinuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…