Pre GE2025 Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti

Pre GE2025 Paul Makonda: Kwa umri huu nitishike na kauli za Watu? Mtapata watu wengine watakaowapetipeti

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ila kusemakweli, nyota njema huandamwa sana. Hivi hakuna wakuu wengine wa mikoa kwenye nchi hii?
Mbona mnamuandama sana huyo kaka?
 
Uko sahihi, anasema rais anatukanwa, Sasa yeye ndio analipiza rais kutukanwa kwa kutukana? Je rais ametukanwa na mtu mwenye nafasi rasmi ya kiutawala, au wahuni wa mitandaoni? Halafu anamtaja rais ili ionekane ana uchungu sana na rais, kumbe ni utetezi wa kichawa.

Huyo dogo alipata madaraka atatawala kama alivyotawala Magufuli. Na hata hiki anachokifanya ni carbon copy ya alichokuwa anakifanya Magufuli.
Kwamba unamtabiria...
 
Ila kusemakweli, nyota njema huandamwa sana. Hivi hakuna wakuu wengine wa mikoa kwenye nchi hii?
Mbona mnamuandama sana huyo kaka?
Kwq lipi sasa?

Ata wewe ikianza kutukana watu na kuvimba kichwa utakuwa mashuhuri kama Tyson?
 
Africa haihitajin vongozi imara bali taasisi imara
Watajulia wapi haya basi?

Watanzania wengi akili ndogo kama za panzi, ni watu wa kufagilia viongozi wanaofanyia maigizo lukuki mbele ya camera dizaini ya Makonda na Magufuli halafu wakitoka kwenye mamlaka hakuna warithi wala mwendelezo wa drama hizo.

Binafsi nitamkubaki kiongozi atakayeondoa mfumo wa kipuuzi wa uongozi katika nchi hii wa utegemezi wa mtu mmojammoja kwenda katika mfumo wa uongozi wa kitaasisi. Bila hivyo hatuwezi kutoboa, huyu anakuja na sarakasi zake, anatoka mwingine anaingia na za kwake, and the chain goes on. Tunajikuta tukizunguka mulemule katika vicious cycle miaka nenda miaka rudi.
 
Uko sahihi, anasema rais anatukanwa, Sasa yeye ndio analipiza rais kutukanwa kwa kutukana? Je rais ametukanwa na mtu mwenye nafasi rasmi ya kiutawala, au wahuni wa mitandaoni? Halafu anamtaja rais ili ionekane ana uchungu sana na rais, kumbe ni utetezi wa kichawa.

Huyo dogo alipata madaraka atatawala kama alivyotawala Magufuli. Na hata hiki anachokifanya ni carbon copy ya alichokuwa anakifanya Magufuli.
Halafu katika waenezaji wa matusi dhidi ya mama naye anaplay part kubwa, ni aidha hajui kwa akili yake kisoda ama anafanya makusudi.

Watu walishaanza kusahau yale matusi mabaya, yeye anawarejesha! Binafsi hata mwanzo nilikuwa nasikia juujuu tu kuwa bimkubwa katukanwa hadi alipozungumza yeye hadharani ndipo screenshot zikaanza kutembea mitandaoni ndipo nikaelewa. Na hakika watu wengi walijua/walifuatilia zaidi baada ya yeye kuweka wazi

Bimkubwa naye anamtizama tu mwanaye 'wa pekee' akimdhalilisha kwa mgongo wa kumtetea, hata kumuonya tu asiyazungumzie hapana. Tuna viongozi ambao hata kufikiri mambo madogo tu ni tatizo.
 
Chapa Kazi MH Usikubali kuyumbishwa Na Wahuni. Watu wasiopenda uchapakazi.

Nitashangaa sana kama Mama Samia Atawasikiliza hawa wasiopenda utendaji wa MH Makonda.

Makonda Amegusa kwenye Mfumo wa wazembe Na walarushwa ndio hawa wanajitokeza maana Amewagusa kwenye mirija yao.
 
Akitumia ile salute ya LISSU atapaa juu sana kisiasa kwa msimamo wake huu.
 
Yule madam alikosea wapi?. Mbona hakuna na kosa mpaka mwisho. Shida aliongea sauti ndogo ndio kudhalilisha.
Kuongea si kupitia kutamka maneno tu kuna lugha ya vitendo/body language na wajuzi wa saikolojia wanasema..body language does not lie..kiongozi aliyekamilika anajua kusikia kupitia lugha ya vitendo..kwa hivyo Makonda alisoma lugha ya vitendo ya huyu mtumishi na kufahamu, kwanza alikuwa anasema uongo, pili alikuwa anaonyesha hakustahili kuulizwa na Makonda pengine kwa sababu yeye ni mzuri, na tatu alionyesha dharau na kutojali uwepo wa hadhara ambayo wengine wana umri sawa na wazazi wake..alivyojibiwa alistahili! wengi wanaomtetea mtumishi huyu hawajui binadamu anaongea kwa vitendo pia, wakati mwingine picha haiwezi kukuonyesha dhahiri lugha ya vitendo sawa na yule anayemsikiliza ana ka ana.
 
Back
Top Bottom