PreGE2025 Paul Makonda: Msigeuze makanisa kuwa viwanja vya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Anawapa
Ngiaje viongozi wa dini? Wao wakipangiwa ohhh siasa. Siasa ni sehemu ya dini ndiyo maana inawafuasi na inasimamia imani/falsafa fulani.

Ukiona kiongozi wa siasa anawalaumu viongozi wa dini ujue huyo kwake haki haipo moyoni mwake.

Yupo tayari kufanya lolote ili tu anufaike mwenyewe.
 
Pumbavu zenu. Ukifuata imani ni lazima ukemee maovu including mateso mnayowafanyia watanzania wasio na hatia. Huwa inawafaa sana viongozi wa dini wakiisifu serikali? Sasa wataendelea kukemea maivu yenu. Labda mtakamata hao wa makanisa madogomadogo. Mnaogopa machafuko wakati tayari mnaua watu? Si tufe wote sasa
 
Yeye kaongelea hayo maneno?

Ni nini hiyo aliyofanya kama sio siasa
 
Amani ni tunda la haki. Viongozi wakihubiri haki ambayo ndiyo msingi mkuu wa dini zote mnasema wanaleta siasa. Mnataka mtunyime haki zetu na mtuue tu bila kukemewa. Nyie ni nani?
 
Hauko sawa kichwani. Wanaongooza kupeleka siasa makanisani ni matapeli wa kijani.
 
Kama kuteta haki sio sehemu ya mafundisho ya mungu basi huyo mungu atakuwa kiumbe katili sana.
 
Huyu si ndo anashinda kwenye makanisa au Mwingine Bible toka mwanzo mpaka mwisho inakemea Uovu Manabii wengi wamekua wakipiga tawala katili dhalimu ukiona nabii hakemei Uovu haongelei mambo ya haki ujue ni tapeli MUNGU ni haki
 
Hivi mbona akina shehe mwaipopo na wenzake hawakukemewa wakati ule wanafanya siasa kipuuzii kabisa misikitini. Sasa ule ndiyo upuuzi wa kukemewa sio hawa wanaohangaika na haki za watanzania wasio na hatia. Huwaga sielewi amani yenu hii mnayoihubiri. Ni ya kutesa kundi fulani ili nyinyi mpate utulivu au ni nini? Hii nchi ilipofika kuna kitu kinatakiwa kitokee ili mjue kuna kukosa wote labda ndiyo mtapata akili ya kukaa chini na kuanza upya kulijenga taifa kwa pamoja. Mnafanya mambo ya kipumbavu sana ndugu yangu na mnaona ni sawa tu.
 
H Makonda ni mzalendo kwa nchi yake.
 
Ukiwakemea wanasiasa madhabahuni utaambiwa unavuka mipaka,

Ukiwasifia madhabahu hakuna tatz🤔

Hata John the Baptist alimkemea mfalme kuteka mke wa kakake, akaundiwa kesi kuwa amevuka line, matokeo John was beheaded na mfalme pia alikufa.

Funzo: Politicians jueni kuwa mnatawala kwa niaba na idhini ya kanisa, na Mkuu wa kanisa ndiye Mungu YESU KRISTO Yeshua Hamashiach.

Hivyo jueni kuwa mamlaka ya kumpangia Mungu KUPITIA vinywa vya watumishi wake manabii, Nini aseme, Nini aache hamnayo!
 
Halafu hata wewe ChoiceVariable ndiyo bingwa wa kukejeli wapinzani wakinyimwa haki. Unaogopa machafuko? Si huwa unasema watanzania bado sana? Nchi siyo ya CCM hii.
 
Hapana ila ukishinda korido za EU na kupigania haki faragha ndio unakuwa mzalendo.
Corridor za EU utashinda unadhani ni corridor za wapiga majungu kama za watumishi wa umma hapa bongo?
 
Corridor za EU utashinda unadhani ni corridor za wapiga majungu kama za watumishi wa umma hapa bongo?
Bora hata hao wapiga majungu kuliko watu wanaotangaza uasi kwa taifa hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…