PreGE2025 Paul Makonda: Msigeuze makanisa kuwa viwanja vya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Watu wa kwanza kujirekebisha wawe wanasiasa! Siyo wakipewa mic wanatoa matamko ya kisiasa!
 
Angemwambia magufuli kipindi kile kuwa aache kutumia kanisa Kwa maslahi ya kisiasa
 
Wao ndio wenye makosa wanaenda kufanya nini kwenye dini na hawataki haki,waanzishe ibada zao za kisiasa wasalishane wenyewe kwa katiba ya chama chao kama hawataki kukemewa!!
 
Sijaona neno Haki hata mara Moja! Ila anasisitiza Amani.
 
Na vipi pale siasa inapogeuzwa kuwa machinjio,mahakama namagereza ya Wantanzania wazalendo wanao hurumia taifa lao linavyoangamizwa na kikundi cha wahuni wachache?
 
Ni wapuuzi gani hao wameyageuza makanisa kuwa viwanja vya siasa, na ni makanisa gani hayo yaliyogeuzwa kuwa viwanja vya siasa?
 
Huyu si alikua anashinda makanisani na kwenye misikiti kuombewa na picha zinatumwa akiwa Mkuu wa Mkoa Daslm.
 
Kwamba kutekana, kuuana, kusingiziana ni siasa? Hayo ndio yanapaswa kuhubiriwa kwa watu ili amri kuu ya Upendo itawale
 
Kazi ya kulinda amani ni ya sisi sote, ma askofu wapo sahihi kutangaza amani kwani ndiyo kazi Yao waachwe huru
 
..yote hayo ni kwasababu hakuna HAKI nchini.

..viongozi wa Kidini kuingilia siasa ni dalili za watawala kufilisika kifikra na kukengeuka kiuongozi.

..kuna OMBWE na viongozi wa dini wameamua kuliziba.

The other way around. Viongozi wa kidini hawakufanya kazi yao ya kuandaa waumini wao wawe na hofu ya Mungu. Kwa vile hawana hofu hiyo, tutaendelea kushuhudia mengi. Siyo kwa siasa tu hata maadili kwa ujumla, yajayo ndiyo yenyewe
 
Viongozi wa awamu ya 5 na 6 ndiyo chanzo Cha yote haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…