Paul Makonda ni Nani? Ni yule Mchimba mchanga, mkata mkaa

Paul Makonda ni Nani? Ni yule Mchimba mchanga, mkata mkaa

Kwangu mm Kutoka Mchimba mchanga na mkata mkaa mpaka RC is a very inspirational journey.

Concern yangu ni akumbuke tu alikotoka, dhamana aliyopewa isimfanye asahau alikotoka.

Dhamana aliyopewa na kauwezo alikonako kiuchumi kwa sasa visimfanye ajione kama kashushwa Kutoka mbinguni.
Shida nikwamba anajikuta analewa madaraka anazingua sana anasahau alipotoka
 
Hakika nampongeza Makonda kwa hatua aliyoifikia kutoka hapo alipokuwa hadi alipo hivi sasa.Nampongeza pia kwa kuanzisha vita vya madawa ya kulevya hata kama hakufuata utaratibu maana kupitia kwake sasa vita inapiganwa kihalali. Maneno na kejeli visimkatishe tamaa ila aendelee kusimamia kile anachokiamini.
 
Kuchimba mchanga,kukataa mkaa,kupiga debe,kupasua zege,n.k hizo zote ni harakati tu za kukufikisha unakotaka kufika..basi makonda yuko vizuri sana kama alifanya hayo mambo...

Mbona rais wa Ghambia alikua kuli mbeba mizigo huko ulaya.

Kwenye maisha usipende kuangalia ulikotoka angalia unakoenda

Ila usisahau ulikotoka
 
Katika siku ambazo gazeti la raia mwema limeandika mambo ya kijinga ni leo..

Kwahiyo kama mtu unachimba mchanga wanataka uishi maisha ya kinyonge daima..

Mbona binadamu wote tunazaliwa na tunapita sehemu ya hovyo inayotoa uchafu mwilini...mbona sijawahi kusikia wakisema "hivi huyu naye alipita sehemu hii ya hovyo wakati wa kuzaliwa"

Kila mtu ana mipango yake kufika pale anapopataka..
 
Japo simpendi huyu dogo ila hii habari ni ya kipumbavu sana,historia ya mtu haimzuii kupata mafanikio ama uongozi
Habari hii haiwezi kuwa ya kipumbavu, upumbavu unaweza kuwa ni tafsiri ya mtu kadri atakavyojipa tafsiri yake kuhusu habari yenyewe. Gazeti limefanya kazi yake, na ni miongoni mwa kazi zinazopaswa kufanywa na chombo cha habari!
 
good
 
Kila mtu ana histora yake
Hata Obama aliishi maisha ya dhiki sana utotoni hadi kutegemea chakula cha bure cha seikali!
Lkn what you make is what you get
Apongezwe kwa hili la kubadili maisha yake ya dhiki kuwa ya faraja kuu
Ugomvi wangu kwake ni ULEVI WA MADARAKA ambao ni mbaya hata kuliko ULEVI WA MIHADARATI
Akijirekebisha kwa hili,Makonda will go down as the one of the best leader TZ to produce
Aheshimu utawala bora!
 
Kam alipitia huko ameonyesha njia ya kufanikiwa ukiwa na malengo,,,ameonyesha hakuna kinachoshindikana chini ya jua ukiamua kuwekeza muda,akil,nguvu na mungu akikusimamia

Sio mbaya kama historia, ni mfano mzuri wa kuigwa, kutokufa moyo au kukata tamaa, ''IKO SIKU YANGU'' imefanya kazi. Ila kama kafika hapo kwa FITNA/HILA ndio mbaya
 
Japo simpendi huyu dogo ila hii habari ni ya kipumbavu sana,historia ya mtu haimzuii kupata mafanikio ama uongozi
Hii yote ni kwa sababu dogo kawashika pabaya ndo maana wanaanza kuongea vitu visivyo hata na maana
 
Habari wakuu!

Gazeti la RAIA mwema Leo limetoka na habari kuu yenye kichwa cha habari Makonda ni nani? Yule mchimba mchanga, mkata mkaa?

View attachment 470671

Na mimi nauliza ndiye yule au mwingine?

chanzo: gazeti la RAIA mwema

Kila mtu ana historia yake, kuna Biblia inatufundisha sana, Kuna wakina Daudi Mchunga Kondoo Mpaka kuwa mfalme mwenye Nguvu, Kuna kina Yusufu, kutoka kuwa Mfungwa hadi kuwa Waziri Mkuu kwenye nchi kubwa ya kigeni. Vilevile kuna kina Goliati wenye nguvu sana wakaishia kukatwa kicha, kuna wakina Sauli/ paulo makatili sana lakini wakawa watakatifi mpaka leo . Wandugu Maisha ni safari, weka malengo, kusanya nguvu, Mtegemee Mungu, jikite kwenye Imani. Nani alijua Magufuli angekuwa hapa na sio Lowasa, sio Membe, sio Mwigulu nk.
 
nawe acha kuandika jambo usilolijua hayo ni magazeti lete stor kamili au ndo uchochezi
 
Habari wakuu!

Gazeti la RAIA mwema Leo limetoka na habari kuu yenye kichwa cha habari Makonda ni nani? Yule mchimba mchanga, mkata mkaa?

View attachment 470671

Na mimi nauliza ndiye yule au mwingine?

chanzo: gazeti la RAIA mwema

Sioni tatizo lolote. Kila mtu anahistoria. Kikubwa ni wapi tunaelekea!
 
Kuchimba mchanga,kukataa mkaa,kupiga debe,kupasua zege,n.k hizo zote ni harakati tu za kukufikisha unakotaka kufika..basi makonda yuko vizuri sana kama alifanya hayo mambo...

Mbona rais wa Ghambia alikua kuli mbeba mizigo huko ulaya.

Kwenye maisha usipende kuangalia ulikotoka angalia unakoenda
Usiangalie ulikotoka ndio lakini ni muhimu Kukumbuka ulikotoka ili uendelee kuyaona maisha katika uhalisia wake ili usije kuwa limbukeni wa madaraka ambayo ni dhamana, mali na anasa za kupita tu!
 
Habari wakuu!

Gazeti la RAIA mwema Leo limetoka na habari kuu yenye kichwa cha habari Makonda ni nani? Yule mchimba mchanga, mkata mkaa?

View attachment 470671

Na mimi nauliza ndiye yule au mwingine?

chanzo: gazeti la RAIA mwema
OH Gosh. Hata na mimi nilikuwa nakojoa na kunya kwenye nappy nilivyokuwa mchanga. Should this need to be appeared on headline?
 
Kila mtu ana historia, sijaona mantiki ya hii habari chochezi!!!

Hivi huyu jamaa ndie yule walimtoa picha anamfunga Riz kamba za viatu? Kama ndie kweli ana historia ndefu. Labda ndio maana anatenda kwa jinsi anavyotenda.
 
Japo simpendi huyu dogo ila hii habari ni ya kipumbavu sana,historia ya mtu haimzuii kupata mafanikio ama uongozi
Habari hii sio ya kipumbavu kwa sababu imekufikirisha na kukukumbusha historia yako nyeusi! Hii habari ni fundishi na fikirishi!
 
Katika siku ambazo gazeti la raia mwema limeandika mambo ya kijinga ni leo..

Kwahiyo kama mtu unachimba mchanga wanataka uishi maisha ya kinyonge daima..

Mbona binadamu wote tunazaliwa na tunapita sehemu ya hovyo inayotoa uchafu mwilini...mbona sijawahi kusikia wakisema "hivi huyu naye alipita sehemu hii ya hovyo wakati wa kuzaliwa"

Kila mtu ana mipango yake kufika pale anapopataka..
wamenukuu nunua gazeti ujue nani kazungumza hayo maneno
 
Anayway, hatushangai. Kuwa RC sio lazima uwe msomi. Hicho ni cheo cha kisiasa hata darasa la saba unaweza kuwa RC. Sia kubwa ni kuwa mkereketwa, kujipendekeza kwa wakuu na kufanya mambo yanayokifurahisha chama tawala, hata kama hayana logiki na yanapingana na mashauri ya wataalamu.

Ila tungependa kuona CV yake
 
Back
Top Bottom