Pamoja kwamba Mimi ni mfuasi wa CHADEMA na mwanachama wa CHADEMA, ila Kuna jambo moja linanifanya nimuunge mkono Makonda. Kusikiliza kero za wananchi ambazo serikali imeshindwa kuzishughulikia.
Mimi simkubali CCM na Wala simkubali Makonda kwa sababu nyingi tu, ila nakubali kwa hichi alichokifanya. Hata Mimi ningepata nafasi ningeenda kupeleka malalamiko yangu.
Kuna jambo tumelipigania sana. Kiasi cha kufikia kwa polisi. Lakini inaonekana polisi wanamuogopa muhusika. Tumepeleka malalamiko na ushahidi Hadi ofisi ya Waziri lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. Wapelelezi wa serikali wamefika sehemu wanakimbia njiani na kuacha mtuhumiwa akijigamba.
Nimeleta ushahidi hapa JF kuhusu tapeli moja anajiita Generali Mwamwega, kwa jina sahihi Macegeron Rweyemamu. Huyu ni tapeli mkubwa analiza watu kupitia kampuni ya One 2 One Focus Limited. Kupitia hiyo kampuni ameitumia kuwahujumu watanzania wengi kiasi Cha wengine kufilisika.
Niliuleta ushahidi hapa JF ukafutwa, tumepeleka ushahidi polisi wamekimbia nao, tumehusisha ofisi za serikali ila wanadai wanamuogopa huyo tapeli.
Inapofikia serikali inamuogopa raia mmoja na hata kumuacha atumie majina ya Viongozi kuibia wananchi unategemea nini?. Kama polisi wanamuogopa tapeli na kuacha kumkamata au kumchunguza raia waendelee wapi?
Generali Mwamwega hagusiki, anatumia cheo Cha jeshi wakati sio mwanajeshi na hakuna Mtu anayemkamata au kumuonya. Anatumia jina la Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi kuibia watu na hakuna anayemkamata au kumuonya. Na emefikia hatua anatumia jina la Waziri Mkuu ila hakuna anayemkamata au kumuonya.
Hivyo basi inapofikia hatua serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi vinamuogopa Generali Mwamwega ambaye wala sio Mwanajeshi aendelee kuumiza raia, basi anachokifaanya Makonda kuita raia na kuwasililiza kero zao nakiunga mkono maana kinaweka hadharani uchafu wa serikali na vyombo vya Dola ambavyo vipo kulinda raia lakini vimegekua kulinda wahalifu.
Kwa nilioyaona kwa Generali Mwamwega na jinsi serikali ilivyomkingia kifua nadhani wananchi wapewe platform ya kuongea haya mambo hadharani Tena live kwenye TV ili uchafu wa vyombo vya Dola uwekwe wazi na wahusika wajue kumbe wanafahamika.
Wakuu wamikoa wengine igeni mfano wa Makonda maana wananchi wa kawaida wananyanyaswa sana na vombo vya Dola vikishirikiana na wahalifu akama akina Generali Mwamwega au kwa jina halisi Osward Macegeron Rweyeyemamu.