Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Paul Makonda Special Thread: Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Paul Makonda; Make Arusha Great Again

Unadhani kulalamika 'live'' kwenye vyombo vya habari kutaondoa matatizo? Ile case ya yule mfanyabiashara wa Kariakoo ambaye inasemekena alijiua kwa kujipiga risasi huko Tabora ni funzo kwa mnaodhani kuwa kulalamika tu kunatosha.
Kulalamika hadharani ni njia bora zaidi kama mifumo imesinzia!! Inamuumbua mhusika lakini pia inaziamsha mamlaka!! Unawezaje kuiona kwamba hii siyo njia sahihi bila kuwa hata na suluhisha kama wewe pia SIYO TAPELI?? Sisi mnaotutapeli kila siku anatufariji sana Makonda
 
Kweli kabisa mkuu. Hii njia anayotumia Makonda itasaidia mambo mengi kubadilika.
 
Kulalamika hadharani ni njia bora zaidi kama mifumo imesinzia!! Inamuumbua mhusika lakini pia inaziamsha mamlaka!! Unawezaje kuiona kwamba hii siyo njia sahihi bila kuwa hata na suluhisha kama wewe pia SIYO TAPELI?? Sisi mnaotutapeli kila siku anatufariji sana Makonda
Watu wameanza kulalamika leo? Mbona wakati wa Magufuli ndiyo ilikuwa ni kilele cha malalamiko? Makonda kaanza kusikiliza malalamiko leo? Huoni kuwa sisi matapeli tunaendelea kudunda huku ninyi wajinga mkipigwa ''mental masterbation''?
 
Mkuu wa mkoa wa Arusha katika kile kinachoitwa kusikiliza kero za wananchi jana akiwa amevalia kinadhifu mavazi ya kofia na tisheti vyenye maneno "Jesus did it" amezungumzia mambo mawili muhimu sana,

1. Wakuu wa mikoa hawapewi maelekezo yoyote ni kero za aina gani wanatakiwa kushughulikia kusikiliza au kutokusikiliza!

2. Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa mwenendo wa nidhamu/maadili wa mahakama za mwanzo katika mkoa wake, jaji mfawidhi ni mjumbe katika kikao chake.

Sheria namba 4 ya mwaka 2011 ya uendeshaji mahakama inamfanya mkuu wa mkoa kuwa mpokeaji malalamiko dhidi ya uamuzi wa kesi wa hakimu.

Wanaweza kukaa kikao na jaji mfawidhi kumuambia achukue hatua kwa baadhi ya mambo. Mwenyekiti wa nidhamu kitaifa wa mahakama ni Rais!
Kwa hiyo makonda kagundua Hilo??

Hii inatofauti Gani na yule mzungi aliyedai kugundua mlima Kilimanjaro wakati kina meku wako nao tangu kuubwa kwake

Punguzeni sofa za kijinga
 
Makonda anajua. Sio msomi ila amewakalisha/atawakalisha wengi TUNATAKA UTHUBUTU basiii
Ccm waliopotea akitokea kichaa moja akajaribu kufanya mambo ya kawaida sana wanamwona kama mungu

Hakuna jipya analofanya ambalo wengine hawajawahi fanya

Sema Huyu muhuni analipa waandishi njaa watangaze Kila upuuzi anaofanya
 
Ni kweli. Sifa zote za udikteta, uuaji, uporaji na upigaji watu risasi alizokuwa nazo jiwe na Makonda anazo
Na unadhan kwamba hayo uliyosema hayapo kwa viongozi? Kenedy ilikuwaje?John Fitzgerald Kennedy.
 
Mkuu yule alijiua baada ya maelekezo ya Rais kutokuheshimiwa na kwa bahati mbaya Rais aliyetoa maelekezo alifariki na kuliacha Jambo bado halijatekelezwa. Sasa Kama Mtu alifikisha kesi yake kwa Rais wa Nchi utamlaumu Nini?. Its unfair tu jamaa akaona hawezi kuhimili msingi akaona ajiue.

Kuhusu Jambo langu tumeenda mpaka polisi Tena Hadi ngazi ya RCO wa Mkoa kupeleka ushahidi na baadae kufungua jalada. Nimepeleka ushahidi Hadi kwa mbunge wangu amfikishie Waziri Mkuu aone jinsi wananchi wanavyoteswa ila hola. Kila mtu kimya. Nimepeleka ushahidi kwa ofisi nyeti ya upelelezi wakakimbia kwa kumuogopa huyo tapeli.
Kilichobakia ni nini? Kama umechukua hatua zote na bado vyombo vya Dola havichukui hatua. Ni Bora kuweka mambo wazi ili seriklia ijisahihishe.
Mkuu ndiyo maana nikauliza ''kulalamika kunasaidiaje? Yaani umekiri kabisa kuwa alikosa msaada japo alisikilizwa! Kwani Tanzania ni Magufuli ndiyo tuseme kwa sababu alifariki basi kila kitu kilisimama?
 
Unadhani Makonda atakomaa na hilo jambo la huyo tapeli mpaka lini??
Mkuu anachofanya Makonda ni kujipa umaarufu kwa vitu vidogo ambaya sio rahisi yeye kuvimalizia.

Atawajaza kwa maneno makali kuzikoromea hizo mamlaka zilizowapuuza, huyo tapeli ataswekwa ndani kwa siku moja, baada ya hapo inabidi mrudie hatua zilezile mlizofeli mwanzo.
Na mpaka hapo Makonda hamtompata tena ili awadaidie tena.
 
Kwa mfano wanawake waliotelekezwa na waume zao na kuachiwa watoto bila kuhudumiwa mahitaji ya msingi.

Unafikiri nani source ya tatizo? Je kila tatizo ni CCM?
Hayo ni maigizo tu tena ya kijinga.Hapo utawasikia wadada wanaanza kuwataja watu kama ilivyokuwa kipindi kile et lowasa,gwajima ndo amenipa minba! Hah kweli ujinga mzigo
 
Unadhani kulalamika 'live'' kwenye vyombo vya habari kutaondoa matatizo? Ile case ya yule mfanyabiashara wa Kariakoo ambaye inasemekena alijiua kwa kujipiga risasi huko Tabora ni funzo kwa mnaodhani kuwa kulalamika tu kunatosha.
Kuandamana napo ni njia moja wapo ya kulalamika live. Kama njia zote unafata na bado hakuna muhafaka ni hatua gani zaidi? Kumloga au kumpiga lisasi
 
Kuandamana napo ni njia moja wapo ya kulalamika live. Kama njia zote unafata na bado hakuna muhafaka ni hatua gani zaidi? Kumloga au kumpiga lisasi
''lisasi'' ni nini jombi! Lakini hapa wanazungumzia kulalamika!
 
Watu wameanza kulalamika leo? Mbona wakati wa Magufuli ndiyo ilikuwa ni kilele cha malalamiko? Makonda kaanza kusikiliza malalamiko leo? Huoni kuwa sisi matapeli tunaendelea kudunda huku ninyi wajinga mkipigwa ''mental masterbation''?
Mkuu kulalamika inakuja Kama last resort. Kama haki yako inaminywa na umefuata all due process. Wananchi wengi wanakimbilia kwa Makonda kwasababu haki zao zinaminywa.
 
Mkuu ndiyo maana nikauliza ''kulalamika kunasaidiaje? Yaani umekiri kabisa kuwa alikosa msaada japo alisikilizwa! Kwani Tanzania ni Magufuli ndiyo tuseme kwa sababu alifariki basi kila kitu kilisimama?

Nadhani jamaa alijiua baada ya msingi wa mawazo. Maana wamekaa vikao na Waziri Mkuu zaidi ya kimoja na hakuna hatua zilizochukuliwa. Nadhani kulalamika kwake kujifanya taifa lijue kinachoendelea na kuweka record straight.
 
Pamoja kwamba Mimi ni mfuasi wa CHADEMA na mwanachama wa CHADEMA, ila Kuna jambo moja linanifanya nimuunge mkono Makonda. Kusikiliza kero za wananchi ambazo serikali imeshindwa kuzishughulikia.

Mimi simkubali CCM na Wala simkubali Makonda kwa sababu nyingi tu, ila nakubali kwa hichi alichokifanya. Hata Mimi ningepata nafasi ningeenda kupeleka malalamiko yangu.

Kuna jambo tumelipigania sana. Kiasi cha kufikia kwa polisi. Lakini inaonekana polisi wanamuogopa muhusika. Tumepeleka malalamiko na ushahidi Hadi ofisi ya Waziri lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. Wapelelezi wa serikali wamefika sehemu wanakimbia njiani na kuacha mtuhumiwa akijigamba.

Nimeleta ushahidi hapa JF kuhusu tapeli moja anajiita Generali Mwamwega, kwa jina sahihi Macegeron Rweyemamu. Huyu ni tapeli mkubwa analiza watu kupitia kampuni ya One 2 One Focus Limited. Kupitia hiyo kampuni ameitumia kuwahujumu watanzania wengi kiasi Cha wengine kufilisika.

Niliuleta ushahidi hapa JF ukafutwa, tumepeleka ushahidi polisi wamekimbia nao, tumehusisha ofisi za serikali ila wanadai wanamuogopa huyo tapeli.

Inapofikia serikali inamuogopa raia mmoja na hata kumuacha atumie majina ya Viongozi kuibia wananchi unategemea nini?. Kama polisi wanamuogopa tapeli na kuacha kumkamata au kumchunguza raia waendelee wapi?

Generali Mwamwega hagusiki, anatumia cheo Cha jeshi wakati sio mwanajeshi na hakuna Mtu anayemkamata au kumuonya. Anatumia jina la Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi kuibia watu na hakuna anayemkamata au kumuonya. Na emefikia hatua anatumia jina la Waziri Mkuu ila hakuna anayemkamata au kumuonya.

Hivyo basi inapofikia hatua serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi vinamuogopa Generali Mwamwega ambaye wala sio Mwanajeshi aendelee kuumiza raia, basi anachokifaanya Makonda kuita raia na kuwasililiza kero zao nakiunga mkono maana kinaweka hadharani uchafu wa serikali na vyombo vya Dola ambavyo vipo kulinda raia lakini vimegekua kulinda wahalifu.

Kwa nilioyaona kwa Generali Mwamwega na jinsi serikali ilivyomkingia kifua nadhani wananchi wapewe platform ya kuongea haya mambo hadharani Tena live kwenye TV ili uchafu wa vyombo vya Dola uwekwe wazi na wahusika wajue kumbe wanafahamika.

Wakuu wamikoa wengine igeni mfano wa Makonda maana wananchi wa kawaida wananyanyaswa sana na vombo vya Dola vikishirikiana na wahalifu akama akina Generali Mwamwega au kwa jina halisi Osward Macegeron Rweyeyemamu.
Serikali inaruhusu wahujumu na matapeli nchini na wale mikopo kaush damu kama Platinum,Bayport n.k!

Eti ni sehem ya intelligence ya kuwatawala watz waendelee kuwa chini kiuchumi!!

Huyo unaemwita tapeli ni sehemu ya mpango kazi wa kitapeli kama Deci vile!!

Unakuta ni mtu ambae system inamtambua kabia na yupo Kwa malengo maalum!

Ukiona mtu mwovu hachukuliwi hatua ujue ni sehemu ya system tu ndivyo ilivyo!!

Hii nchi Kuna vitu vya ajabu sana vinaruhusiwa kwa sababu maalum!!

Unafikiri kwanini Rama was kariakoo alijipiga risasi Kwa kutapeliwa fedha !!?

We achana nae huyo jamaa!!kama hachukuliwi hatua ni dhahiri shahiri analindwa na mfumo kabisa!!

Hats hizi deals zinazopigwa plus wizi vinalindwa na na system kwa ujumla!kama havilindwi kwanini vipo!!?

Ndivyo ilivyo!
 
Unadhani Makonda atakomaa na hilo jambo la huyo tapeli mpaka lini??
Mkuu anachofanya Makonda ni kujipa umaarufu kwa vitu vidogo ambaya sio rahisi yeye kuvimalizia.

Atawajaza kwa maneno makali kuzikoromea hizo mamlaka zilizowapuuza, huyo tapeli ataswekwa ndani kwa siku moja, baada ya hapo inabidi mrudie hatua zilezile mlizofeli mwanzo.
Na mpaka hapo Makonda hamtompata tena ili awadaidie tena.
Mkuu nakubali unachosema. Ila kwa Sasa tupo desperate hivyo ni Bora atakaye tusaidia hata robo au nusu kuliko ambaye hawezi kutusaidia.
 
UWONGO!! Mhimili wa Mahakama hauingiliwi na paka yoyote kama Makonda
Soma sheria aliyozungumzia Makonda utaelewa vizuri, kwenye maelezo yake amesema lazima kuwepo na "checks".
 
Back
Top Bottom